TBC1 Inaipendelea CHADEMA na Kuihujumu CCM?

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
Jana saa mbili usiku nilikuwa nikiangalia taarifa ya habari ya TBC1 na habari kuu jana ilikuwa ni kutua kwa mahelkopita huko Igunga kwa ajili ya kutumika katika mikutano ya kampeni. TBC1 walionyesha helkopita ya CCM ikitua na Makamba akapokelewa na Mwigulu na watu wengine. Kisha ikaonyeshwa kwa UFUPI SANA Mwigulu akihutubia na kisha makamba akasikika akisema maneno mawili matatu tu basi. Pia TBC1 haikuonyesha UMATI wa watu ambao hao viongozi wa CCM walikuwa wakihutubia!! Kwa kifupi coverage kwa CCM ilikuwa kidogo sana.

Kisha nikashuhudia coverage ya CHADEMA. Walianza kuonyesha helkopita ikiwa angani na maneno CHADEMA yakionekana, kisha wakaionyesha helkopita ikiwa eneo fulani ambalo naamini ni kituo cha mafuta ikiwa inakunywa mafuta. Baada ya hapo helkopita ya CHADEMA ikaonyeshwa ikitua huko Nkinga na Mwenyekiti wao akashuka na kuhutubia. Kinyume na walivyo cover hotuba ya CCM, hapa Mbowe alipewa muda mreeefu akihutubia kuhusu mambo ya siasa na dini na wakati huohuo TBC1 ikionyesha umati wa watu ambao Mbowe alikuwa akihutubia. Baada ya hotuba TBC1 walionyesha helkpita ya CHADEMA ikituka kuondoka eneo la mkutano.

Kwangu mimi naona TBC1 hawakuitendea haki CCM kwa kuipa coverage kidogo sana hasa juu ya helkopita ambayo imegeuka kuwa ni kete ya kisiasa huko Igunga. Pia TBC1 hawakumuonyesha mpambanaji Magufuli wakati akiunguruma huko Igunga.
 
Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
Mimi niliacha kuiangalia hiyo stesheni muda mrefu sana. Wana tabia ya kuwapendelea sana Magwanda, sijui wamepewa hela na Mbowe?
 
figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
19,595
24,124
basi kama hukumuona magufuri leo utamuona kwenye magazeti.munakosa mambo ya kuwaumiza.2015 ccm itakapo toka madarakani utalia sana.uongo?mia
 
mwacheni77

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
763
209
Mnataka Tbc ioneshe idadi kubwa ya watu kwenye mkutano wa ccm wakati hawapo(wamefika idadi ndogo hiyo mliyoiona) Tbc wawatoe wapi watu kwa ajiri ya ccm,naamini uchaguzi huu ukiisha mkurugenzi ataMTIDO kama kawaida yenu
 
SEAL Team 6

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
655
118
Mimi niliacha kuiangalia hiyo stesheni muda mrefu sana. Wana tabia ya kuwapendelea sana Magwanda, sijui wamepewa hela na Mbowe?
Mnafiki utamjua tu. TBC1 ni CCM watu tulishaacha kuangalia hiyo TV siku nyingi sana kwa sababu ya kuipendelea CCM.
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,761
572
duh hapo kuna propaganda kama wanashindwa kuitii serikali inayowaajili basi kuna kitu
 
Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
Mkuu, jambo hilo hapo ni sawa na kusema CHADEMA ni sawa na usemi wa chanda chema huvishwa pete.
 
Nzagamba Yapi

Senior Member
Sep 1, 2011
167
70
Sina chama mpaka sasa,but cdm mkikosa coverage kwenye tbc1 mnalalamika etic hombo kinachoendeshwa na kodi za watz kinependelea chama tawala mkipata coverage tatizo,nahisi kama mkipata nchi mtalipiza kisasi sana,naomba kitokee chama chenye muunganiko wa ccm,cdm,cuf na tlp ntajiunga nacho..
 
MBURE JASHA

JF-Expert Member
May 7, 2011
200
46
Masaburi alikuwa na akili kuwashirikisha siri ya fikra zenu zinapotoka. Kila mtu anajua TBC1 ni wapambe wa ccm, sasa wamewasaidia kutoonesha idadi ndogo ya watu kwenye mkutano wenu alafu bado mnalalamika?
umeona eh. toka lini wezi wakaumbuana. TBS wanatumia kodi zetu vibaya kubeba vikojozi. mwizi mwenzao haku reach target. watamwonyesha kweli kumuumbua. Jiulize tu swali 1. Kuwa Magamba wanapata bilioni moja kama Ruzuku + miradi yao ya dhulma kama Mkwakwani stadium,KIrumba pengine nawe unajua kidogo lakini hazitoshi hata kushusha kwenye wilaya na kata zao. Lakini kwenye uchaguzi hata wa mwenyekiti wa kijiji sehemu ambayo ina upinzani utaona mbwembwe na matumizi makubwa ya Fedha. Je Fedha hizo zinatoka wapi kama si kwenye kodi zetu
 
WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
Jana saa mbili usiku nilikuwa nikiangalia taarifa ya habari ya TBC1 na habari kuu jana ilikuwa ni kutua kwa mahelkopita huko Igunga kwa ajili ya kutumika katika mikutano ya kampeni. TBC1 walionyesha helkopita ya CCM ikitua na Makamba akapokelewa na Mwigulu na watu wengine. Kisha ikaonyeshwa kwa UFUPI SANA Mwigulu akihutubia na kisha makamba akasikika akisema maneno mawili matatu tu basi. Pia TBC1 haikuonyesha UMATI wa watu ambao hao viongozi wa CCM walikuwa wakihutubia!! Kwa kifupi coverage kwa CCM ilikuwa kidogo sana.

Kisha nikashuhudia coverage ya CHADEMA. Walianza kuonyesha helkopita ikiwa angani na maneno CHADEMA yakionekana, kisha wakaionyesha helkopita ikiwa eneo fulani ambalo naamini ni kituo cha mafuta ikiwa inakunywa mafuta. Baada ya hapo helkopita ya CHADEMA ikaonyeshwa ikitua huko Nkinga na Mwenyekiti wao akashuka na kuhutubia. Kinyume na walivyo cover hotuba ya CCM, hapa Mbowe alipewa muda mreeefu akihutubia kuhusu mambo ya siasa na dini na wakati huohuo TBC1 ikionyesha umati wa watu ambao Mbowe alikuwa akihutubia. Baada ya hotuba TBC1 walionyesha helkpita ya CHADEMA ikituka kuondoka eneo la mkutano.

Kwangu mimi naona TBC1 hawakuitendea haki CCM kwa kuipa coverage kidogo sana hasa juu ya helkopita ambayo imegeuka kuwa ni kete ya kisiasa huko Igunga. Pia TBC1 hawakumuonyesha mpambanaji Magufuli wakati akiunguruma huko Igunga.

taifa na igunga vinahitataji sana maneno ya kujenga mshikamano badala ya udini,risasi na uchochezi vinavyopandikizwa na ccm ndio maana chadema ikapewa airtime kubwa hivyo
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,228
8,722
siyo kwamba wamefanya hivyo kwa bahati mbaya bali wana malengo yao lengo kuu nikuwapa nafasi ccm siku ya mwisho ya kampeni ilikuongeza mhemko..pili alicho kuwa anakiongea mbowe ni swala la kitaifa ambalo kila mtanzania angependa kulisikia kutoka kwa kiongozi wa juu hasa xhama tawala akiliongelea kwa hisia kali tofauti na wanavyofanya magamba wanalifanya mtaji wa kujiatia kura bila kujari madhara yatokanayo na kampeni zao hizo chafu..
 
Lamtongi

Member
Jul 6, 2011
38
7
Sina chama mpaka sasa,but cdm mkikosa coverage kwenye tbc1 mnalalamika etic hombo kinachoendeshwa na kodi za watz kinependelea chama tawala mkipata coverage tatizo,nahisi kama mkipata nchi mtalipiza kisasi sana,naomba kitokee chama chenye muunganiko wa ccm,cdm,cuf na tlp ntajiunga nacho..You must be out of your mind!
 
utantambua

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,367
319
Jana saa mbili usiku nilikuwa nikiangalia taarifa ya habari ya TBC1 na habari kuu jana ilikuwa ni kutua kwa mahelkopita huko Igunga kwa ajili ya kutumika katika mikutano ya kampeni. TBC1 walionyesha helkopita ya CCM ikitua na Makamba akapokelewa na Mwigulu na watu wengine. Kisha ikaonyeshwa kwa UFUPI SANA Mwigulu akihutubia na kisha makamba akasikika akisema maneno mawili matatu tu basi. Pia TBC1 haikuonyesha UMATI wa watu ambao hao viongozi wa CCM walikuwa wakihutubia!! Kwa kifupi coverage kwa CCM ilikuwa kidogo sana.

Kisha nikashuhudia coverage ya CHADEMA. Walianza kuonyesha helkopita ikiwa angani na maneno CHADEMA yakionekana, kisha wakaionyesha helkopita ikiwa eneo fulani ambalo naamini ni kituo cha mafuta ikiwa inakunywa mafuta. Baada ya hapo helkopita ya CHADEMA ikaonyeshwa ikitua huko Nkinga na Mwenyekiti wao akashuka na kuhutubia. Kinyume na walivyo cover hotuba ya CCM, hapa Mbowe alipewa muda mreeefu akihutubia kuhusu mambo ya siasa na dini na wakati huohuo TBC1 ikionyesha umati wa watu ambao Mbowe alikuwa akihutubia. Baada ya hotuba TBC1 walionyesha helkpita ya CHADEMA ikituka kuondoka eneo la mkutano.

Kwangu mimi naona TBC1 hawakuitendea haki CCM kwa kuipa coverage kidogo sana hasa juu ya helkopita ambayo imegeuka kuwa ni kete ya kisiasa huko Igunga. Pia TBC1 hawakumuonyesha mpambanaji Magufuli wakati akiunguruma huko Igunga.

Wee umetumwa na magamba. Haya kachukue posho yako kama unalipwa kwa post. Unaweza itenganisha vipi TBC na magamba wakati ni kitu kilekile? Ile TBC si ni idara ya uenezi ya magamba
 
utantambua

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,367
319
Kuna kituko nimesimuliwa na jamaa alikuwa zambia, anasema kuwa gazeti la serikali la zambia siku zote hadi siku ya uchaguzi na siku ile ambayo usiku wake matokeo ya uraisi yalitangazwa lilikua likimkandamiza na kumnyima coverage Satta. Satta aliitwa maneno yote maovu: mchonganishi, tapeli, mwanaharamu, msaliti, kibaraka, mchochezi na tahariri za kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake. Lakini asubuhi yake tu matokeo yalipotangazwa gazeti hilohilo lilipambwa na picha na habari kemkem na nzuri za Satta. Na TBC itakua hivo tu very soooon hapa bongo
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
Wee umetumwa na magamba. Haya kachukue posho yako kama unalipwa kwa post. Unaweza itenganisha vipi TBC na magamba wakati ni kitu kilekile? Ile TBC si ni idara ya uenezi ya magamba

Na wewe umetumwa na nani? Hizo ni akili mgando. Mbona wenzio wanachangia vizuri tu ila wewe unakimbilia kuwa mtu katumwa!!Acha mawazo mgando.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom