AdvocateFi
JF-Expert Member
- Jan 15, 2012
- 11,492
- 5,050
TCRA na tbc ni sawa na mboga na chumvi.
...inasikitisha sana kuona kuwa TV za private hapa TZ ndizo za kuaminiwa na pia hazina bias...wakati TBC yenye kuendeshwa kwa kodi yetu watanzania wote ikifanya kila iwezalo kuhadaa umma kila kukicha...kwa kuonyesha habari za kiupendeleo kwa chama tawala ccm na kuwapamba watu wa ccm kana kwamba imekua TV ya ccm....inasikitisha na ifike wakati TCRA wawaangalie na kuwadhibu hawa wezi wa kodi zetu mchana kweupe....hakuna chombo cha umma kinachowaibia wananchi wake kama TBC....na ningekuwa na uwezo ningewafungia ama kubadili management yao yote...mana hawa watu hawatufai....
...Kingekua chombo cha binafsi kinafanya hivi kwa maslahi ya wamiliki tungeelewa lakini TBC ni chombo cha umma....na wanalipwa mishahara kwa kodi zetu....iweje kila leo wanadanganya umma kwa bias zao kwenye information??alafu wezi hawa ndio walitaka eti TV zote zionyeshe taarfa za habari kupitia kwao saa 2 usiku????...NO NO pls.....hawa wamekosa nidhamu mno....Mimi na family yangu tulishaacha kuangalia TBC kwasababu ya ubovu wao ki weledi....Waende wajifunze BBC wanavyofanya kazi zao....maana kile ni chomb cha umma lakini hawako biased kama hawa makopo wa TBC....
..na tunapoelekea uchaguzi october TBC lazima wabadilike...wasipofanya hivyo watachangia kuchagiza machafuko hapa TZ....nawaambia wajitafakari matendo yao mbele ya umma...watanzania wanawaona....na hawapendi matendo yao...
Mi nadhani yule ni Mshana wa kuchovya, Washana hatuna akili za kushikiwa, nina wasi wasi na origin yake, pengine kachukua jina Ujombani. zumbemkuu njoo hapa na Kaka MANI ....waeleze huyu Mshana ni yupi anayechafua jina letu hivi???Yule msomaji awajibishwe tu kwa kweli maana hata kama ni maelekezo kutoka juu alitakiwa achanganye na za kwake. Huyu Mshana ni janga pale TBC, bad enough ni koda yangu mtanzania ndo inayowalipa mshahara.
Please TCRA kwa magnitude ile ile kwa ITV na Clouds kipindi cha nyuma do the needfull kwa hawa hata kama ni chombo cha Serikali msiwe wanafiki.
Inakera sana tena sana Mm nineshindwa kuendelea kutazama nahisi presha itanipanda bure kwa ujinga wanaofanyaKama ingekuwa CCM Tv hamna ambaye angelalamika kwa sababu ingekuwa ya chama kama ambavyo hatulalamiki kwenye gazeti la uhuru, lakini kwenye TBC chombo chs umma hili halikubaliki. Clement Mshana hebu lizungumzie hili.
Tunawaonea bure TBC1,jamani TIDO MHANDO alifukuzwa sababu tu ya kuwa FAIR kwa upinzani nani anataka kuweka UGALI wake MCHANGA?
wachangiaji wengi humu hawajui kabisa maana ya neno 'pekee'. Mtangazaji amesema kuwa habai iliyopewa uzito wa pekee na wala hksema habari ilyopewa uzito mkubwa She is a professional journalist. Asingeweza kusoma mafuriko wakati siyo mafuriko. Magazeti mengi yanaandika sensational news. Mafuriko,tsunami, kimbunga ni sensational. Mwandishi hawezi kurudia kusoma kichoandikwa na magazeti in a sensationa manner.
Waondoke hao wanaolazimishwa kufanya kazi au kutekeleza majukumu yao kinyume na utaratibu kwa shinikizo kama alivyoondoka Tido Mhando wakati ule.
Nchi inatakiwa iongozwe na iendeshwe kwa mujibu wa sheria sio utashi wa mtu.TBC ni televisheni ya taifa ,inatakiwa kuwajibika kwa hili hasa ukizingatia inaendeshwa kwa kodi za Watanzania wenye vyama na wasio kwenye vyama.Kupata habari kwa wananchi ni haki yetu kikatiba ,ilindwe na isimamiwe na tuone ikitendeka lakini sio kwa namna hii..
Siipendi CCM na viongozi wake kwa kuendesha nchi kwa matakwa yao ,polisi wanapovunja haki za raia wakiulizwa wanasema ni agizo kutoka juu ,ni nani alie juu ya Katiba ya nchi!!!????.Tukirusha ngumi mnasema tunapenda fujo ,wakati ninyi ndio wa kwanza kuvunja utaratibu...Hatupendi hizo ,hatupendi kugawanywa kihuni namna hii.