Things Fall Apart
Senior Member
- Jun 26, 2012
- 178
- 146
Habari wana JF,
Naanza na swali: Je, ni halali kwa televisheni ya taifa (TBC) kutangaza habari kwa kupotosha?
Hii imetokea leo katika uchambuzi wa magazeti kwani mtangazaji aliyekuwa akisoma habari za magazeti anashika gazeti na kusema "habari iliyopewa uzito wa kipekee..." lakini cha kustaajabisha anasoma habari ambayo siyo iliyopewa uzito wa kipekee na kuiacha kabisa habari iliyopewa uzito wa juu kisa tu kwamba inamzungumzia Edward Lowassa mgombea urais wa Ukawa kwa tiketi ya CHADEMA. Tizama mwenyewe hapa:
Hii ni wazi kabisa kuwa kanuni za huduma ya utangazaji (maudhui) ya mwaka 2005 zimekiukwa hadharani. Kanuni ya 6(2) inasomeka hivi:
"Kila mwenye leseni ni lazima ahakikishe anatoa taarifa kwa usahihi na uhakika; anaripoti habari bila upendeleo na kuzingatia mizani, bila kukusudia au kuondoka katika ukweli, ama kwa kuvuruga au kwa kutoa taarifa zisizo sahihi".
Ikumbukwe kuwa, ni majuzi tu Mamlaka ya Mawasiliano TCRA imekichukulia hatua za kinidhamu kituo cha ITV kwa kuripoti habari zisizo za kweli.
Hivyo basi; kwa kuwa sharia ni msumeno, basi na TBC nayo iadhibiwe vilevile kwa upotoshaji huu. La sivyo tutakuwa tuna "double standards". Kitendo hiki sio tu kinadhalilisha taaluma ya utangazaji bali pia kinalitia aibu shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) ndani na nje ya nchi ikizingatiwa kuwa serikali imekuwa ikijinasibu kuwa inafuata misingi ya uwazi na uwajibikaji.
Naomba kuwasilisha.
Update:
TCRA imeipa onyo TBC1. Habari zaidi, Soma=>TCRA yaipa onyo kali TBC1 kwa kosa la Ubaguzi wa kusoma habari Magazetini

TCRA ni taasisi inayoongozwa kwa mujibu wa Sheria ya EPOCA 2010, Kanuni za Utangazaji pamoja na masharti ya leseni za Utangazaji.
Upo utaratibu unaofuatwa katika kushughulikia ukiukwaji wa Kanuni au Masharti ya leseni ikiwa ni pamoja na kumtaka mwenye leseni kujibu tuhuma na kuitwa kwenye Kamati ya Maudhui.
Hatuwezi kutoa hukumu bila kumsikiliza mwenye leseni na shauri kufikishwa katika Kamati ya Maudhui.
Tunawasihi wananchi kuwa Na subira suala hili linafanyiwa kazi na taarifa kwa umma itatolewa juu ya maamuzi yatakayotolewa.
Asante
Update:
TCRA imeipa onyo TBC1. Habari zaidi, Soma=>TCRA yaipa onyo kali TBC1 kwa kosa la Ubaguzi wa kusoma habari Magazetini
Last edited by a moderator: