TBC yadanganya, hatua stahiki zichukuliwe

TBC yadanganya, hatua stahiki zichukuliwe

Hii TV ya TBC na ile radio ya wahuni clouds muda mrefu wanatakangaza mambo ya hovyo na hawa Idara ndogo ya Lumumba TCRA wapo kimya kama kingekuwa kituo kingine cha tv basi wangeshakipiga faini au kufungiwa.
 
Hii Idara TCRA inaongozwa kutoka Lumumba, wanatumika na ccm kama idara nyingine za umma kama Polisi, Jeshi na NEC lakini mwisho wenu utakuwa Oktoba na sisi tutawasulubu na kuwafundisha jinsi ya kufanya kazi kwa uadilifu
october 25 i love you
 
CCM Wanaitumia Tbc Vibaya
Na wanaitumia TCRA, tunasema tunataka katiba ya wananchi hivi vyeo vya kupeana fadhila vina madhara yake. Tuna taka vyeo kama hivi viwe wanaomba sio vya kuteuliwa watu wengine hawana uwezo. Cheo cha IGP, TRA, TCRA, CEO wa TV wote wawe waombaji
 
Yaan huyu bibie haoni hata aibu..?! kalishwa noti huyu si bure.., takukuru mhojini haraka iwezekanavyo..!
 
Vipi kuhusu gazeti la Uhuru maana nao walipotosha habari siku Edward Lowassa alipochukua fomu ya kuwania urais kwa kusema watu waliporwa, kulikuwa na vurugu wakati habari hizo zilikuwa tofauti na zilizotolewa na waziri wa mambo ya ndani Mh. Chikawe, Makamanda wa polisi Carmilius Wambura na Kova kuwa maandamano yalikuwa ya amani na hakuna uporaji wowote. Tunaomba hili mlishughulikie kama mlivyoshughulikia ITV.
Ahsante
Hawana ubavu wa kulipiga faini au kulifunga, ofisi za TCRA zipo Lumumba
 
TBC inaweza kuchochea vurugu na machafuko Tanzania, ikiwa itaendelea na tabia hii ya kuwa wakala wa chama tawala ilhali inaendeshwa kwa kodi za Watanzania wote. Kuna hili la kuita Watanzania (wanaohudhuria mikutano ya UKAWA) vibaka, nadhani gazeti la Uhuru lilipaswa kuwa limefungiwa kwa hili.

TCRA tunakutazameni, na tunafahamu mnachopaswa kufanya katika hali kama hii. Simamieni sheria, bila woga.
 
TBC inaweza kuchochea vurugu na machafuko Tanzania, ikiwa itaendelea na tabia hii ya kuwa wakala wa chama tawala ilhali inaendeshwa kwa kodi za Watanzania wote. Kuna hili la kuita Watanzania (wanaohudhuria mikutano ya UKAWA) vibaka, nadhani gazeti la Uhuru lilipaswa kuwa limefungiwa kwa hili.

TCRA tunakutazameni, na tunafahamu mnachopaswa kufanya katika hali kama hii. Simamieni sheria, bila woga.
 
tcra na tbc1 mtu na mwenzie sidhani kama wanatenda haki
TCRA tunawaomba huku mtuambie mmechukua hatua gani kwa TBC kufuatia upotoshaji wa makusudi wanaposoma magazeti kwa habari zinazohusiana na Lowassa/ Ukawa
 
Last edited by a moderator:
TCRA tunawaomba huku mtuambie mmechukua hatua gani kwa TBC kufuatia upotoshaji wa makusudi wanaposoma magazeti kwa habari zinazohusiana na Lowassa/ Ukawa
tena watangazaji kabisa wanaruka kwa makusudi taarifa... kama hii TBC1 ni ya ccm waseme mapema iwezekanavyo
 
Nashauri ianzishwe thread itakayokuwa inaweka wazi mambo yote ya BIASNESS tena kwa ushahidi wa picha hasa wakati huu wa kuelekea kampeni na Uchaguz mkuu. Yale Masharti ya habari kutoka TCRA, Msajili wa Magazeti lazima yaheshimiwe. Habari itendewe haki. Pale CCM inapofanya vizuri au vibaya ipewe haki yake na pale Upinzani wanapokosea au kufanya vizuri wapewe haki yao.
 
Na TCRA ituambie kinachofanywa na gazeti la UHURU mali ya CCM ni sahihi kuupotosha UMMA???

Na kama hiyo ni ndogo kwanini hawamchukulii hatua Nape kwa maneno yake mengi yenye utata na ambayo mwisho wa siku yataweza kuleta MACHAFUKO hasa wakati huu wa UCHAGUZI?

Au watueleze kama na wao ni tawi dogo la CCM baada ya lile la NEC????
 
Ila kwa kweli hata aibu hawaon kwa sababu wanachokifanya ni kuzalilisha taaluma yao ya habar
 
Mwanafunzi akienda mafunzo kwa vitendo hapa ni lazima akirudi chuoni kwake ataanguka mtihani wa mwisho, yaani habari iliyopewa kipaumbele ni kama hiyo !!!!!!
 
TCRA ni taasisi inayoongozwa kwa mujibu wa Sheria ya EPOCA 2010, Kanuni za Utangazaji pamoja na masharti ya leseni za Utangazaji.

Upo utaratibu unaofuatwa katika kushughulikia ukiukwaji wa Kanuni au Masharti ya leseni ikiwa ni pamoja na kumtaka mwenye leseni kujibu tuhuma na kuitwa kwenye Kamati ya Maudhui.

Hatuwezi kutoa hukumu bila kumsikiliza mwenye leseni na shauri kufikishwa katika Kamati ya Maudhui.

Tunawasihi wananchi kuwa Na subira suala hili linafanyiwa kazi na taarifa kwa umma itatolewa juu ya maamuzi yatakayotolewa.

Asante

Achaa upuuzi wewe nani hajui mpo kisheria?!

Hata TBC pia ipo kwa mujibu wa sheria pia so kama inakiuka mbona mwachukua muda sana kuwawajibisha?! ITV haikupita hata siku moja...ila TBC ni muda gani sasa umepita?!

Hayaa mashinikizo ya kisiasa kwa manufaa ya wachache huua hata taaluma za watu...!!

Ni heri ungekaa kimya kuliko kuja andika huu upupuz hapa ati "linafanyiwa kazi" ni aibu hii si kwenu tu bali mwalitia aibu Taifa zima.
 
TCRA hawafanyi haki kabisa. Hiki chombo kivunjwe.
 
Nami nimeona nina video nimerekodi kabisaaa du TBc CCM DU mtangazaji huyo afungiwe kabisaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom