Nimeanziosha thread mpya kwa makusudi ili kuwajulisha kuwa TCRA wanachokifanya ni mchezo wa kitoto na kipuuzi, wote tumeshuhudia Mtangazaji wa TBC akisoma magazeti kwa udanganyifu mkubwa, tukategemea kwamba TCRA watatoa tamko, tukakaa kimya Jumamosi, Jumapili leo Jumatatu saa kumi na mbili kasoro jioni, hakuna tamko lolote lililotolewa. Mbona ITV mlikimbilia kuwashupalia? Tuwaeleweje?
Kumbukeni, TBC inaendeshwa kwa kodi za wananchi nikiwemo mimi ambaye kwa mmoja tu nakatwa PAYE zaidi ya laki tano za kitanzania. Whether nitaangalia TBC or not bado wanatakiwa wasome magazeti kadiri yalivyoandikwa. Tuepuke kuwa double standard kwa kipindi hiki kigumu. Kama hamtatoa tamko sitaacha kuandika na nitaleta barua hadi ofisini kwenu ya malalamiko binafsi.
Hili linatoa picha kwamba taarifa nyingi za TBC ni za uongo, sio reliable na kwamba huwa zinatengenezwa na hazina uhalisi. kama mlitudanganya kwa hili basi mmetudanganya kwenye mengi. hebu jaribuni kufuatilia link hizo muone TBC wanavyowadanganya Watanzania kila siku. Mimi nimeamua kusema HAPANA. Naomba tuwe wote
https://www.youtube.com/watch?v=dnRNQ0D1Iqs
https://www.youtube.com/watch?v=As64f45rjJQ