TBC na Vyama vya Upinzani kuna ugomvi gani, au ni maagizo toka juu?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Wakati wa Utawala wa Magufuli ilikuwa ni kawaida kuyasikia TBC wakimtangaza Mtawala Muda wote Alipo na kutoisikia TBC ikitangaza habari na matukio ya vyama vya Upinzani Watanzania.

Hatukushangaa kwani amri ilikuwa ya Magufuli tu, leo tupo Awamu ya 6 bado TBC wanaendelea na Kutokutangaza Habari na matukio ya vyama vya upinzani.

Je, kuna ugomvi au ni agizo la mtawala?

TBC ni chombo cha umma kinaendeshwa kwa kodi za Watanzania Wote bila kujali Vyama vyao.

Tafadhali kitende HAKI kwa vyama vyote
 
Wakati wa Utawala wa Magufuli ilikuwa ni kawaida kuyasikia TBC wakimtangaza Mtawala Muda wote Alipo na kutoisikia TBC ikitangaza Habari na Matukio ya Vyama vya Upinzani Watanzania hatukushangaa kwani AMRI ilikuwa ya MAGUFULI TU Leo Tupo Awamu ya 6 bado TBC Wanaendelea na Kutokutangaza Habari na MATUKIO ya Vyama vya UPINZANI Je kuna Mgomvi au Ni Agizo la MTAWALA? TBC ni Chombo cha UMMA kinaendeshwa kwa Kodi za Watanzania Wote bila kujali Vyama vyao Tafadhali kitende HAKI kwa VYAMA VYOTE
TBC wenyewe wnasemaje?
 
Ryoba naye hajifunzi kwa kina Kangi Lugola, MAKONDA,Chalamila,na SABAYA,Anafikili hicho cheo ni Cha milele.
Hajifunzi hata kwa Bashiru kabla ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM alikuwa na hoja za kujenga sana lakini baada ya kuwa katibu mkuu wa CCM akaota mapembe, sasa anajuta!
 
Tupo kwenye mfumo wa chama kimoja!
Ukiwa barua ya uteuzi kwa taasisi ya umma, unapewa na ilani ya CCM, kisha unapimwa kupitia ilani.
Hapo vp?
 
Inawezekana ikawa ndio masharti ya mikataba ya wafanyakazi. Ukitangaza/kuripoti habari za chama cha upinzani kibarua kimeota nyasi.
 
Kuna vipindi huwa anavisimamia kila jtano.
Huwa simuelewi nikuwakatisha wachangiaji halafu yeye anaongea mda mrefu hadi waalikwa wanakosa nguvu
 
Back
Top Bottom