TBC Mnakera sana!

TBC Mnakera sana!

TBCCM ni janga la Taifa, Mwakani CCM ikibwagwa wafanyakazi wote wafungashe virago tu. Ifungwe kwa muda wakati watawala wapya wanapanga safu zao. Halafu ndipo wakabidhi mitambo na ofisi na baadaye watafutwe wafanyakazi wapya wa kuendeleza gurudumu la maendeleo.

wewe ndio tatizo
 
What's the hell of TBC mbona mnakatiza hotuba ya Tindu Lissu kuhusu maoni ya wachache bunge? kumbukeni mpo hapo kwa kodi zetu wacheni tusukize zote mwishowe sisi wananchi ndio tutaamua sio kwa kulazimishiwa
 
Ninaangalia bunge live TBC ila TBC wamekata matangazo makusudi baada ya kuona Tundu Lisu anawachana live kuhusu muundo wa muungano. Source TBC na mimi mwenyewe!
 
kwanini TBC wanatuudhi kiasi hiki Watanzania wenzangu??? TELEVISION nyingine mko wapi mtuokoe na hili JANGA??
 
And they did it again this morning...wakati Mh Lisu anafafanua maoni ya wachache leo bungeni, TBCCM wamekatisha ghafla na kwa makusudi matangazo yao na badala yake wakaanza kupiga nyimbo zinazoisifu Tanzania na kuweka matangazo yanayopiga promo ya Muungano. Ni bora kabisa wasitishe matangazo ya moja kwa moja kuliko hivi wanavyokatisha maoni ya wachache.

Inavyoelekea kutakuwa na mtangazaji kaahidiwa kuzawadiwa ukuu wa wilaya kwa masharti ya kukata mawazo ya wapinzani yasisikike bungeni.

Tusisahau kwamba mauaji ya kimbari kule Rwanda yaliyochochewa na utangazaji wa kinazi na kizombi kama huu wanaoufanya TBCCM. Tuombe Mungu tusije tukafikishana huko kwa 7bu ya UPUMBAVU wa watu wachache.
 
Hao wa station zingine wakirusha matangazo ya bungeni ndio watafungiwa kabisa
 
Acha kuangalia kama wakuudhi kwani umelazimishwa? CDM wametangaza mgomo siku nyingi tu.
 
Nimechukia sana hiki kitendo cha tbc kukata matangazo makusudi kwani mi napenda nisikie hoja na maelezo ya kila pande ili nichuje chuya mwenyewe lakin sasa wananiaminisha zaid kwa wasemayo hawa wachache.
 
Kama leo tbc taifa wamepata aibu ya mwaka kwa kukata matangazo live bungeni

Napenda kutoa angalizo kwa TANESCO wasije kuibeba falsafa hii ya TBC siku ya jumatatu

TBC ni ya umma na TANESCO pia fanyeni kazi kwa manufaa ya watanzania
 
Eti wamekatisha kutoka na hali ya hewa...muda wote huo haliyahewa haikua kikwazo?..Stupid tu..------- kibisa..

Hata hilo la tanesco jumatatu wanaweza kulitumia kwa kukata umeme maeneo mengi ya mjini

Hawa jamaa hawana aibu kabisaa wamesahau watz wa sasa sio wale wa nyerere ujinga tu!
 
Mnajidai haimtazami TBC lakini utafiti unaonyesha nyie ndio watazamaji wakuu, kila mara mnakuja na malalamiko yasiyo na kichwa wa mguu humu!

Mkuu huwezi ikwepa TBC kutazama Bunge. ndo wanaorusha matangazo toka bungeni vyombo vingine vinarusha matangazo kupitia TBC
 
Nadhani mtawalaumu tu TBC (ijapo siipendi pia) kwani inaonyesha wao wanapokea maelekezo kuwa muda huu watoke hewani nk! Maana kabala ya TBC1 kutoka hewani, tayari Star Tv ambao nao wanarusha matangazo haya ya BMK walijiondoa hewani wakti Rev Msigwa akiongea...yakuwa wanalazimika kutoka hewani kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao! Hii nikuonyesha mpango mahususi uliopikwa na wapikaji ya taarifa gani zisiende kwa umma!

Wanaotengeneza hizi propaganda, wanashindwa kuelewa kuwa wanawapandisha hasira wananchi wengi wanaofuatilia hili bunge kwa kushuhudia upuuzi wao, tazama Lissu kuondolewa hewani leo, jana Mbatia akiwa anaongea (kama Lissu leo)...umeme ulikatwa karibu nchi nzima!
 
Ulitaka kwenye hivyo vipindi vya asubuhi wahojiwe makada wa CHADEMA wasio na staha katika lugha zao? TBC ni chombo cha umma na kinalinda maslahi ya Umma, wengi wanaohojiwa sio tu ni makada wa CCM pia ni viongozi wa serikali. Sioni ubaya hapo!

kwahyo makada wa MaCCM ndo wanastaha we ni pun'gu kweli.
 
Kusema ukweli leo nimesikitishwa saana na TBC.Kwa bahati mbaya hili sio tatizo la leo tu, limekuwa likijitokeza mara nyingi sana. Sasa leo Kamanda Msomi Mwanasheria Mh. Tundu Lissu ''Mnyampaa'' amekatiwa matangazo wakati akiwasilisha maoni ya wachache kamati namba 4. TBC hawakutoa taarifa yeyote kama kuna tatizo, tena kwa dhihaka wakaweka hotuba ya Kikwete ''Dr''. Haya ni matumizi mabaya ya chombo cha umma, huu ni uchochezi wa hali ya juu

Nimshukuru Mwenyekiti kwa kuona haja ya Mh.Tundu Lissu kuwasilisha tena jumatatu. Sasa basi, natoa onyo kwa TBC na mabwana zao, kwamba wakikata Jumatatu, tunang'oa mitambo yenu
 
Back
Top Bottom