TBC Mnakera sana!

TBC Mnakera sana!

Duh kumbe hili linagusa wengi, kwakweli TBC wanatuma kufanya kampeni za CCM kwenye mchakato wameenda mbali zaidi hata watu wanaojidai kuwahoji mitaani nao ni CCM. Kiukweli wanashindwa/kwa makusudi hawataki ku balance story. Hovyooo, tena bora yule cjui nani aliekuwepo mwanzoni kwenye kipindi cha jambo Dodoma alikuwa anahoji maswali ambayo CCM wanatakiwa kujibu.

Lakini huyu Mama ni kama sanamu kaletwa pale hana mbele wala nyuma, huu wizi wa kodi zetu kuna siku mtazilipa bila kupenda.

Wanajiona kuwa wao ni Wana CCM na kusjisahau kuwa wao ni Watanzania.
 
Nina miaka sasa sijawahi kuangalia TBC toka tulipoizika pale jangwani

Nasisitiza tuisusie tbccm waangalie wenyewe tu
 
POLE SANA, Mimi Binafsi siiangalii hata siku moja kwani ni kichefu chefu tosha. Hata hivyo subira yavuta heri ni mwaka na nusu umebaki nchi kuwa mikononi mwa wazawa mambo yote yatarekebishwa.
 
Jamani wengine ni wazalendo wa kweli na kituo chao cha uzalendo ni TBC,hivyo anaposema anachukizwa na hali iliyopo ni kweli ana hoja ya msingi,kituo hiki kinapata pesa kutokana na kodi zetu hivyo vipindi vyake yafaa vive na usawa kwa watanzania wote.
 
"Anayemlipa mpiga zumali ndiye achaguaye nyimbo"
 
Jamani hiki Chombo cha utangazaji kinachojiita Cha Umma kimepoteza sifa ni bora kiitwe chombo cha CCM.Nasema hivyo kwa sababu hakitendi haki kwa watanzania kwa mfano vipindi vingi vya mahojiano kama Jambo asubuhi wanaohojiwa ni makada wa CCM hasa ktk Mchakato wa katiba mpya.Wanachokifanya wanachukua kada wa CCM na wajumbe wale 201 ambao ni makada wa CCM mfano Kingunge na kuanza kuendesha mdahalo juu ya katiba mpya.Jambo ambalo linakuwa limeegemea upande mmoja.
Mie Sina chama lkn kitendo hiki kinachofanywa na TBC hakikubaliki kwani hili shirika linaendeshwa kwa kodi zetu ikiwamo kodi yangu.Mfano mzuri ni hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa kufungua bunge imerudiwa zaidi ya mara kumi,cha kushangaza hotuba ya jaji warioba haikurudiwa kama ya rais,wakati ya warioba ndiyo ilibeba sauti kuu ya watanzania. Hata taarifa za habari ziko katika mlengo wa CCM.Sikatai kuwa hotuba ya rais isirushwe bali ninachokisema ni kuwa kuwe na msawazo ktk kurusha habari.Igeni mfano wa STAR TV na ITV wanajitahidi kuweka check and balance ktk midahalo yao.
Napendekeza hiki chombo kibadilishwe jina na kisiwe Shirika la Utangazaji la Taifa maana hakibebi maudhui ya watanzania bali kinabeba maudhui ya kisiasa zaidi.

Bora umetambua hilo ila umechelewa sana!

Tido D Mhando alijaribu kulifanya Shirika la Utangazaji wakaona ana hatarisha ulaji wao!

FYI TBC ni moja kati ya jumuiya za CCM (yaani kama UVCCM, nk).
Wao nyeusi wanawalazimisha watazamaji waseme nyeupe! HOVYO SANA TBC
 
Clement Mshana ..Mkurugenzi wa TBC ..ni mtu asiyejiamini kama mwana habari ..Daima anategemea kulamba Miguu Ndio kunamweka pale ....,ila Siku atakapo retire au mikataba kwisha sijui ni nani atamkumbuka hata kumuamba Ushauri Kama mwanataaluma...
Hakuna mwenye mawazo tofauti anayeipewa nafasi ..kuanzia wageni hata WATUMISHI ..na ikitokea basi Siku ingine hataalikwaaa...
 
Waache kwanza kutukata kodi...
You are very right.....

Kama TBC wanataka kuendesha kituo chao kama radio Uhuru, wanapaswa kwanza wasitishe kupokea ruzuku toka Hazina kwa ajili ya kuendesha kituo chao, na badala yake watembeze 'bakuli' kwa makada na mashabiki na wapenzi wa magamba ali wakichangie kituo chao chá propaganda cha TBC1.......
 
Ngoja ikukere unaiangalia ya nini?mimi hiyo afadhali nizime tv kulko kuiangalia.
 
Mkuu utajipa shida tu na kujitafutia magonjwa yasiyo ya lazima bure achana nao haraka sana!
 
mie mara ya mwisho kuckia rtd ni 2002 ezekiel malongo akitangaza mpira....! what is tbc?
 
Ulitaka kwenye hivyo vipindi vya asubuhi wahojiwe makada wa CHADEMA wasio na staha katika lugha zao? TBC ni chombo cha umma na kinalinda maslahi ya Umma, wengi wanaohojiwa sio tu ni makada wa CCM pia ni viongozi wa serikali. Sioni ubaya hapo!
 
Akiongea katika kipindi cha tuongee asubuhi kinachorushwa na Star tv,mh.Machali amekiponda kituo cha tetevision cha umma cha TBC 1 kuwa kina tabia mbaya ya kualika watu wenye mtizamo wa chama kimoja na hapa alikuwa akimanisha wafuasi wa CCM ndio wanaoalikwa.Mh machali ameongeza kuwa anakatwa kodi kuiendesha TBC na kile ni chomba cha umma.

Wakati huo huo,Machali ameisifu Star tv kwa kualika wageni bila kupendelea upande wowote,ambapo leo amealikwa yeye pamoja na mh.Assupter Mshana kutoka CCM kama wageni kujadili yanayojiri katika bunge la katiba na mada ya leo ikihusu uhakisi wa Tanzania kwenye Hati ya Muungano.

MY TAKE:
TBC kweli wana tabia mbaya.

Kama serikali ya CCM inaonekana kuitumia TBC kwa sababu za kisiasa,je huu si ushahidi wa kimazingira wa serikali ya CCM kutumia vyombo vya dola(polisi) kwa madhumuni hayo hayo?
 
Leo tena TBC walikuwa na Mh
Nahodha na Bi Anna Tibaijuka. Hawasikii na wala hawakomi
 
Hivi hili haliwezi kuleta mkanganyiko hususani wa kimaadili ya vyombo vya habari?...

Maana kwa tafsiri ya haraka ni kuwa Star TV imetumika kuiponda TBC, hata kama Ndg Machali kaeleza ukweli
 
Back
Top Bottom