TBC Mnakera sana!

TBC Mnakera sana!

Sasa mtu anaongea live utahariri vipi hapo?!

Unajua maana ya kuhariri?

Soma hiyo post yangu ya juu hapo mkuu...habari inahaririwa hata kwenye live covarage

Linaweza kuwekwa tangazo fupi na mtu akapewa onyo nyuma ya pazia na kipindi kikaendelea
 
Mkurugenzi wa TBC anaogopa yaliyomkuta Tido Mhando yasije ya kamfika
 
Nilikuwa nawaangalia wakati wao ndo wanarusha bunge tu, sasa hivi Star na EATV wanarusha tena kwa picha murua!
 
Akiongea katika kipindi cha tuongee asubuhi kinachorushwa na Star tv,mh.Machali amekiponda kituo cha tetevision cha umma cha TBC 1 kuwa kina tabia mbaya ya kualika watu wenye mtizamo wa chama kimoja na hapa alikuwa akimanisha wafuasi wa CCM ndio wanaoalikwa.Mh machali ameongeza kuwa anakatwa kodi kuiendesha TBC na kile ni chomba cha umma.

Wakati huo huo,Machali ameisifu Star tv kwa kualika wageni bila kupendelea upande wowote,ambapo leo amealikwa yeye pamoja na mh.Assupter Mshana kutoka CCM kama wageni kujadili yanayojiri katika bunge la katiba na mada ya leo ikihusu uhakisi wa Tanzania kwenye Hati ya Muungano.

MY TAKE:
TBC kweli wana tabia mbaya.

Kama serikali ya CCM inaonekana kuitumia TBC kwa sababu za kisiasa,je huu si ushahidi wa kimazingira wa serikali ya CCM kutumia vyombo vya dola(polisi) kwa madhumuni hayo hayo?

tulishaachaga kuangalia tbccm
 
Labda CCM ya miaka hii ndiyo imekuwa OGA ya kukimbia midahalo yenye HOJA na KUFIKIRISHA akili. Mbona Nyerere alikuwa anakuja Nkrumah Hall (UDSM) na kutukabiri kwa hoja na sometimes kututoa nock out! Mbona BW Mkapa 1995 alimkabiri Mrema kwenye mdahalo wa wazi wa president candidates na kumpiga nock out Mrema!

Bobuk hii CCM imekuwa klabu ya fisi!
 
Siyo siri wengine tumepata tabu sana na hiyo TBC1 kwa tunaotumia ZUKU,Ila cha kushukuru tangu jana tumeingiziwa ITV ndani ya ZUKU,Imebakia hiyo STARTV TU kwa local channels za bongo.CONGRATULATION ZUKU,WELCOME ITV AND BYE BYE TBC1
 
Wanajiona kuwa wao ni Wana CCM na kusjisahau kuwa wao ni Watanzania.

Katika kipindi cha jambo wanapo ongelea Bunge Maalumu la Katiba, kila siku wanaleta makada wa Chama, nashindwa kufahamu ni ratiba au ni kwa makusudi. Busara yangu inanituma TBC kikiwa ni chombo cha walipa kodi, wajumbe wote wana haki sawa ya kukitumia. Huyu Mama Upendo Wela bora angeitwa Penda CCM!
 
Sasa hapo uzushi wangu upo wapi?

Pamoja na ubaya wote wa TBC lakini mtu au taasisi ikikiuka ethics tukae kimya na kutokumueleza?

Kutumia chombo fulani cha habari kukikandia chombo kingine cha habari tena vilivyo katika kada moja sio maadili sahihi na hata sheria inaweza kutumika kushtakiana...

Tbc inaendeshwa kwa kodi ambayo hata star tv wanakatwa hata mtangazaji wa star tv ana haki ya kuhoji acha raia
 
Toka lini mahijiano ya live yakahaririwa au zile f**k za kule bungeni zilizokuwa tinatemwa na kigwangala zilihaririwa na hao tbccm

Hayo ndio makosa tunayotakiwa kuyapoint out na kuwasema hawa TBC and the likes...

Habari ya moja kwa moja mtangazaji anaruhusiwa kuomba radhi kwa kitendo chochote ambacho violent
 
Uchambuzi wa magazeti wanachambua yale ya serikali ni CCM huwezi ona mwananchi,Mtanzania,----- na Tanzania Daima
 
Sijui 2gome kulipa kodi maana kodi ni kwaajili ya kuendesha serikali kinyume chake imekuwa kuendesha na kulinda chama kweli inauma sana!lakini mung yupo 2tafika 2 japo 2tafika 2mechoka mbaya.
 
Ulitaka kwenye hivyo vipindi vya asubuhi wahojiwe makada wa CHADEMA wasio na staha katika lugha zao? TBC ni chombo cha umma na kinalinda maslahi ya Umma, wengi wanaohojiwa sio tu ni makada wa CCM pia ni viongozi wa serikali. Sioni ubaya hapo!

yaani wewe ni choo? nakubali wewe ni msalan maana hata maneno yako ni aya huko huko
 
Unaangalia kituo hicho cha nini? Licha ya kutangaza pumba, pia watangazaji wake hawana MVUTO. Ulishawahi kuona wapi watangazaji wa TV wamenenepeana kama sanamu la MICHELIN?!
 
Katika kipindi cha redio cha ‘Leo Katika Bunge' ambacho katika bunge hili maalumu la katiba kinaitwa ‘Katiba Tuitakayo', kinachorekodiwa na kurushwa na TBCCM kuanzia saa 3:00 hadi saa 4:00 usiku, mtangazaji wa TBCCM anayerekodi kipindi hiki kutoka bungeni Dodoma ameacha kwa makusudi kabisa kurekodi michango iliyotolewa na Juma Duni Haji, pamoja na Eng. Habibu Mnyaa waliotoa maoni ya kundi la watu wachache! Lakini maoni yote yaliyotolewa na wabunge wa CCM, hata kama ya kipuuzi, yamepewa airtime ya kutosha.

Haya ni makusudi kabisa yanayofanywa na chombo hiki kilichopo chini ya CCM ambacho huendeshwa kwa kodi za wananchi. Wanalenga kuwanyima wananchi habari sahihi juu ya watetezi wa maoni yao waliyoyatoa kwenye rasimu ya katiba hii inayojadiliwa. Inaonekana ripota wa kipindi hiki amepewa maelekezo maalumu na CCM kuhusu michango ya wabunge anyopaswa kuirekodi na kuirusha hewani, lengo likiwa kuwapumbaza na kuwahadaa wananchi juu ya usaliti unaofanywa na wabunge wa CCM katika kusigina maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya katiba.

Haiingii akilini kuona kwamba CCM wanafanya makusudi kuwanyima wananchi habari na kuwaacha wabakie mbumbumbu ili waendelee kuwatawala, kuwakandamiza, kuwanyonya na kuwamasikinisha. Raia wanakosa huduma muhimu za kijamii kama vile huduma za afya, shule, maji, barabara, nk kwa kisingizio kwamba hakuna fedha, kumbe fedha zinatumika kuendesha kituo cha redio ambacho hakina manufaa yoyote kwa wananchi. Ni bora vituo vya redio na tv vya TBCCM Taifa na TBCCM1 vifungwe kwani havina faida yoyote kwa wananchi.
:yield:

umasikini ni kazi ya ccm.jpg View attachment 150745 bonge ya shule.jpg


CCM wataiua nchi.jpg darasa chini ya muti.jpg darasani.jpg

huduma safi.jpg maisha bora,.jpg picha.JPG
 
Mkuu, Laiti tu wangekusikiliza. Lakini wanasema; Sikio la kufa halisikii dawa. Hao wabunge wawili ni mwiba kwa ccm
 
Back
Top Bottom