Katika kipindi cha redio cha Leo Katika Bunge ambacho katika bunge hili maalumu la katiba kinaitwa Katiba Tuitakayo, kinachorekodiwa na kurushwa na TBCCM kuanzia saa 3:00 hadi saa 4:00 usiku, mtangazaji wa TBCCM anayerekodi kipindi hiki kutoka bungeni Dodoma ameacha kwa makusudi kabisa kurekodi michango iliyotolewa na Juma Duni Haji, pamoja na Eng. Habibu Mnyaa waliotoa maoni ya kundi la watu wachache! Lakini maoni yote yaliyotolewa na wabunge wa CCM, hata kama ya kipuuzi, yamepewa airtime ya kutosha.
Haya ni makusudi kabisa yanayofanywa na chombo hiki kilichopo chini ya CCM ambacho huendeshwa kwa kodi za wananchi. Wanalenga kuwanyima wananchi habari sahihi juu ya watetezi wa maoni yao waliyoyatoa kwenye rasimu ya katiba hii inayojadiliwa. Inaonekana ripota wa kipindi hiki amepewa maelekezo maalumu na CCM kuhusu michango ya wabunge anyopaswa kuirekodi na kuirusha hewani, lengo likiwa kuwapumbaza na kuwahadaa wananchi juu ya usaliti unaofanywa na wabunge wa CCM katika kusigina maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya katiba.
Haiingii akilini kuona kwamba CCM wanafanya makusudi kuwanyima wananchi habari na kuwaacha wabakie mbumbumbu ili waendelee kuwatawala, kuwakandamiza, kuwanyonya na kuwamasikinisha. Raia wanakosa huduma muhimu za kijamii kama vile huduma za afya, shule, maji, barabara, nk kwa kisingizio kwamba hakuna fedha, kumbe fedha zinatumika kuendesha kituo cha redio ambacho hakina manufaa yoyote kwa wananchi. Ni bora vituo vya redio na tv vya TBCCM Taifa na TBCCM1 vifungwe kwani havina faida yoyote kwa wananchi.
:yield:
View attachment 150744 View attachment 150745 View attachment 150746
View attachment 150747 View attachment 150748 View attachment 150749
View attachment 150750 View attachment 150751 View attachment 150752