TBC Mnakera sana!

TBC Mnakera sana!

Hivi hili haliwezi kuleta mkanganyiko hususani wa kimaadili ya vyombo vya habari?...

Maana kwa tafsiri ya haraka ni kuwa Star TV imetumika kuiponda TBC, hata kama Ndg Machali kaeleza ukweli

Machali ametoa maoni yake, na kwa vyovyote si maoni ya STAR TV. Hata hao wasimamizi wa maadili ya vyombo vya habari wanajuakuwa TBC wana TABIA MBAYA.
 
TBC ni tarumbeta refuuuu wapulizaji wapo Magogoni.
 
Anataka kualikwa akatie shombo? Kama mtu haipendi TBC1 asiangalie
 
Swali la kujiuliza hivi ni kwanini TBC1 wanakwepa kuwakaribisha wazungumzaji wenye mitazamo tofauti (Wanaotaka serikali 2 v wanaotaka serikali 3). Je ni kweli kwamba TBC1 wameshagundua kwamba wanaotaka serikali 2 hawa HOJA bali VIOJA, hivyo kuwashindanisha kwa HOJA na wanaotaka serikali 3 itakuwa ni kumvua nguo MFALME? Hivi katika zama hizi za TEHAMA ki/viongozi wanaweza kuficha UDHAIFU wao kwa njia hii? Just thinking aloud
 
Hivi hili haliwezi kuleta mkanganyiko hususani wa kimaadili ya vyombo vya habari?...

Maana kwa tafsiri ya haraka ni kuwa Star TV imetumika kuiponda TBC, hata kama Ndg Machali kaeleza ukweli
Acha uzushi wewe!Tena mtangazaji alifanya juhudi kumkatisha Machali asiendelee kuiponda TBC lakini Machali alikomaa.
 
JAMANI INAITWA TBC-CCM; TBC AMEONDOKA NAYO TIDO MHANDO SIKU NYINGI SANA,mm tbc naifungua kulitazama bunge tu baada ya hapo nahamia ITV,ila kuna taarifa kuwa hujuma hizo hazina tija mbele ya maoni ya wananchi maana huo ndio msingi wa katiba duniani kote
 
Akiongea katika kipindi cha tuongee asubuhi kinachorushwa na Star tv,mh.Machali amekiponda kituo cha tetevision cha umma cha TBC 1 kuwa kina tabia mbaya ya kualika watu wenye mtizamo wa chama kimoja na hapa alikuwa akimanisha wafuasi wa CCM ndio wanaoalikwa.Mh machali ameongeza kuwa anakatwa kodi kuiendesha TBC na kile ni chomba cha umma.

Wakati huo huo,Machali ameisifu Star tv kwa kualika wageni bila kupendelea upande wowote,ambapo leo amealikwa yeye pamoja na mh.Assupter Mshana kutoka CCM kama wageni kujadili yanayojiri katika bunge la katiba na mada ya leo ikihusu uhakisi wa Tanzania kwenye Hati ya Muungano.

MY TAKE:
TBC kweli wana tabia mbaya.

Kama serikali ya CCM inaonekana kuitumia TBC kwa sababu za kisiasa,je huu si ushahidi wa kimazingira wa serikali ya CCM kutumia vyombo vya dola(polisi) kwa madhumuni hayo hayo?

Kila chombo na idara ya serikali hapa nchini kinatumika kisiasa....
Na kwa miaka mingi sasa CCM wamekuwa wakitumia muungano kisiasa vile vile!
 
Swali la kujiuliza hivi ni kwanini TBC1 wanakwepa kuwakaribisha wazungumzaji wenye mitazamo tofauti (Wanaotaka serikali 2 v wanaotaka serikali 3). Je ni kweli kwamba TBC1 wameshagundua kwamba wanaotaka serikali 2 hawa HOJA bali VIOJA, hivyo kuwashindanisha kwa HOJA na wanaotaka serikali 3 itakuwa ni kumvua nguo MFALME? Hivi katika zama hizi za TEHAMA ki/viongozi wanaweza kuficha UDHAIFU wao kwa njia hii? Just thinking aloud

CCM daima ni waoga kuukabili ukweli!
Hawapendi wapingwe hata kama wanapotosha....
Hili halijaanza leo... fuatilia hata kwenye midahalo mbali mbali
Wakijua kuna hoja nzito zinapingana na zao basi wanaingia mitini! (Ref: Kikwete, mchakato majimboni, BMK, n.k)
 
Acha uzushi wewe!Tena mtangazaji alifanya juhudi kumkatisha Machali asiendelee kuiponda TBC lakini Machali alikomaa.

Sasa hapo uzushi wangu upo wapi?

Pamoja na ubaya wote wa TBC lakini mtu au taasisi ikikiuka ethics tukae kimya na kutokumueleza?

Kutumia chombo fulani cha habari kukikandia chombo kingine cha habari tena vilivyo katika kada moja sio maadili sahihi na hata sheria inaweza kutumika kushtakiana...
 
Swali la kujiuliza hivi ni kwanini TBC1 wanakwepa kuwakaribisha wazungumzaji wenye mitazamo tofauti (Wanaotaka serikali 2 v wanaotaka serikali 3). Je ni kweli kwamba TBC1 wameshagundua kwamba wanaotaka serikali 2 hawa HOJA bali VIOJA, hivyo kuwashindanisha kwa HOJA na wanaotaka serikali 3 itakuwa ni kumvua nguo MFALME? Hivi katika zama hizi za TEHAMA ki/viongozi wanaweza kuficha UDHAIFU wao kwa njia hii? Just thinking aloud

Ndugu yangu jambo hilo haliitaji elimu ya chuo kikuu, TBC ni chombo cha serikali, serikali iliyopo madarakani inataka muungano wa serikali mbili, hivi kweli hata kama ungekuwa wewe ungeleta watu wanaounga mkono serikali tatu kwa ajili ya kupiga propaganda hiyo? sual la kuwa tbc inaendeshwa kwa kodi za wananchi ni kweli kabisa lakini utambuzi huo si kwa TANZANIA ambayo Rais na makame wake wanashiriki kampeni za uchaguzi mdogo kwa gharama za kodi za wananchi wakati chama chao kina fedha magari na kila uwezo wa kutumi raslimali za chama kufanikisha kampeni zao.
 
CCM daima ni waoga kuukabili ukweli!
Hawapendi wapingwe hata kama wanapotosha....
Hili halijaanza leo... fuatilia hata kwenye midahalo mbali mbali
Wakijua kuna hoja nzito zinapingana na zao basi wanaingia mitini! (Ref: Kikwete, mchakato majimboni, BMK, n.k)

Labda CCM ya miaka hii ndiyo imekuwa OGA ya kukimbia midahalo yenye HOJA na KUFIKIRISHA akili. Mbona Nyerere alikuwa anakuja Nkrumah Hall (UDSM) na kutukabiri kwa hoja na sometimes kututoa nock out! Mbona BW Mkapa 1995 alimkabiri Mrema kwenye mdahalo wa wazi wa president candidates na kumpiga nock out Mrema!
 
Hivi si unafahamu kuwa kuna Uhariri wa habari?

Umenishangaza kwa kiwango kikubwa! Wewe ulitaka "mhariri" aingie kichwani mwa Mh. Machali na kumkataza asiseme alichosema? Jamani tusiwe wepesi wa ku-criticize bila kutafakari hoja za wenzetu!
 
Umenishangaza kwa kiwango kikubwa! Wewe ulitaka "mhariri" aingie kichwani mwa Mh. Machali na kumkataza asiseme alichosema? Jamani tusiwe wepesi wa ku-criticize bila kutafakari hoja za wenzetu!

Kama ni live coverage mwandishi anayefanya mahojiano huwa anaomba radhi moja kwa moja na wakati huo huo anatoa angalizo kwa yule anayemuhoji...

Hapa si suala la kufanya criticism bali ni kuelezana ukweli, hizi thics zipo na zimeandikwa ni suala la kukumbushana tu...

Ndio hatuipendi TBC kwa kuwa inatumiwa na serikali kama ilivyo magazeti ya Uhuru nk lakini tusisahau katika kukosoa tujaribu kujenga hoja...
 
Back
Top Bottom