Chikwangara
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 685
- 939
Wasoma magazeti asubuhi ndo kabisa sijui hawaoni headlines za muhimu kwan wanarusha sana habari za Chadema,ovyo kweli!
......Leo kwenye kipindi chao kinachorushwa kuanzia saa saba mchana kinachoitwa Dira ya mchana,TBC1 wametangaza habari ambayo naweza sema kuwa ni propaganda chafu zinazotumiwa na CCM kudhoofisha nguvu ya vyama vya upinzania hasa CHADEMA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kule Arumeru Mashariki.
......Akiripoti mwandishi wao amedai kuwa kuna wanachama wa CHADEMA na TLP wamejiunga CCM akiwepo M/kiti wa jumuiya ya wazazi wa TLP..cha kushangaza huyu mwandishi ameonyesha kadi ameonyesha kadi zisizopungua 10 za TLP na KUSHINDWA KABISA KUTUONYESHA KADI ZA WANACHAMA WA CHADEMA..Hii naweza sema ni mchezo mchafu na wakitoto tena unaorushwa na kituo chenye dhamana ya kulinda maslahi ya UMMA bila kulalia upande mmoja...napata taabu kufikiri kuwa mbona huyu mwandishi akutoonyesha kadi za CHADEMA? na mtu atahitwaje mwanachama wa CHADEMA bila kuwa na kadi?
......Ombi langu kwa chumba cha habari TBC1 wanapaswa kujua kuwa habari zao tunazisoma na kuzisikiliza na kuziona..utumbo wanaofanya kuna siku utawagharimu..na niwakati wa hawa waandishi wa hiki kituo cha habari kuzingatia weledi badala ya kuendelea kulalia CCM utadhani kuwa CCM watatawala milele.
achana nayo hiyo tbc1,kazi kubwa umbeya tu.lini utakuta cnn au bbc wanaonyesha kitchen party?
Like any other state-owned media, TBC is bound by the Constitution to act in favour of the present goverment. Bear in mind that the government is being responsible for the corporation's running costs starting from payment of workers' salaries to day-to-day financial needs and one should not expect TBC to repay this by promoting the anti-government side Magw.anda. Chadema should either learn to come to terms with TBC bias or gather funds from supporters to set up their own TV facility that would promote and praise Chadema 24-7.
Hii ni hatua ya amani ya kuonyesha kupinga njama mbovu za serikali za kuendelea kukandamiza wananchi. TBC ni chombo cha umma kinachotumia fedha za walipa kodi bila kujali ni wanachama wa chama gani. Kama ilivyo kwa vyombo vingine vya habari kama mahakama na polisi, serikali imeendelea kwa muda mrefu kuitumia TBC kukandamiza wasioishabikia CCM
Najua kuwa wanapata ruzuku yao kutoka kwenye kodi zetu hivyo hawalaji hata kama hatuiangalia TV au kusikiliza redio zao. Hata hivyo mafisadi hawa wameendelea kujikusanyia fedha nyingi za kifisadi kwa kulipisha matangazo mbalimbali katika vituo vyao. Natoa wito kwa mtu yeyote ambaye sio mshabiki wa CCM, asitazame wala kupeleka tangazo likatangazwe CCM.
Mbinu ya kususia ushirika wa namna yeyote kwa mafisadi imekuwa ikitumika katika nchi nyingi na sehemu nyingi imesaidia sana katika kuwaadhibu mafisadi.