Taarifa ya habari saa mbili,
Nkamia akimwombea mwajiri wake wa zamani fedha toka serikali amesema TBC itafunga matangazo yake wakati wowote kuanzia sasa, akithibitsha hali hiyo amesema hawana kamera, vifaa vya kuchanganya matangazo hawana na kwamba 1.2 bilioni waliyopewa ni kwa umeme na millioni 500 ni ndogo walizopewa za uendeshaji
My Take:
Ni heri TBC ifungwe kwani haitusaidii kitu wanaendekeza libeneke la kuminya demokrasia
kwani TV zingine zinazojiendesha kibiashara zinawezaje?
Si wawaombe ushauri wengine.
Kuna vitu vingine huwa sielewi kabisa.
its like nightmare,TBC wana gharama kubwa za matangazo kuliko TV zingine iweje wao washindwe wakati wengine wana make money.Au matangazo ya serikali ni free na ya CCM.
Mkuu, hilo waliloomba TV binafsi ndilo ambalo lilipaswa kufanyika na ndilo linalofanyika kwa kawaida kwenye vyombo vya habari vya umma - kwa kuwa wanapatiwa ruzuku na serikali vinapaswa kujitoa kwenye ushindani, hasa ukitilia maanani kuwa hivyo vyombo binafsi baadaye vinatozwa kodi.Nakumbuka private tv stations walisha-raise issue ya TBC kurusha matangazo ya biashara huku wakiwa wanapewa ruzuku na kuomba either wapewe ruzuku tu au wasipewe ruzuku na kushindana na vyombo binafci kwa matangazo.. Serikali ikakataa.. Laana imewakuta..
Ndoto za kichaa na mwendawazimu we Television ya taifa inawezaje kufungwa wakati ndicho chombo kikuu cha kiserikali
Wafunge Tu kwa kweli!
Ndoto za mchana tena za mwendawazimu, we tokea lini kituo cha taifa cha habari kikafungwa. Nchi yoyote inategemea media za serikali kama source ya kufikisha ujumbe wa kiserikali na kuzima propaganda mbali mbali. Mapinduzi yote ya kijeshi yatokeapo miongoni mwa mambo ya awali ni kuchukua vituo vya matangazo vya kijeshi kwa hiyo ni ndoto kusema kituo kama hiki chenye umuhimu wa aina yake KIFE.
Kweli JF kuna wafalme juha wengi wenye ndoto za abunuwasi