TBC Kufunga matangazo yake wakati wowote kutoka sasa

Samahani naomba kuuliza tu. Wanatishia kufunga matangazo au kufuta matangazo. Mi' naona waachwe wafutike.
 
Kuna katamdhilia kamoja nilipenda kukaangalia nilipokuwa nimetoka kazini napumzika. MAU DOUDOU NA WAKWEZE. Mara gafla wakakatiza bila taarifa wala sababu. Matangazo tu yale ya bango wanarudia wk nzima means no new advtsmt. Vipindi karibuni vyote ni marudio. Marudio tuuuuu! Wafunge kabisa hii kitu.
 
Haitafungwa abadan kwa vile serikali lazima ibaki na chombo cha propaganda!
Teh teh teh Wanajikopa wenyewe ndo tatizo lao wamesahau kabisa sasa hivi hata kukilisha chombo chao cha propaganda, unajua ATC pia ilikuwa hivihivi walijikopa mpaka imekufa yaani inakuwa na -ve budget kiasi kwamba inachujkua muda kuirudisha kwenye +ve umesikia walipewa kiasi gani? huwezi amini ni zilitosha umeme tu, Umesikia hiyo tanesco yenyewe? Hoi bin taabani ya leo ya kesho! Sijui DAWASCO labda wao wana nafuu, Bima ndio haoooooo sijui hata kama mazishi yalisha fanyioka, nani tena....
 
Dua la kuku halimpati mwewe....hizo ni zilezile siasa za domo kaya! kwani mmeshasahau kilio cha wabunge..'mshahara na marupurupu yetu ni madogo kulingana na kupanda kwa maisha ya mjini dodoma, na kiasi kikubwa cha vijisenti vyetu tunavitumia kuwapa wapigakura wetu wenye matatizo'. Kwa taarifa yako TBC1 wana zana nyingi na za kisasa za utangazaji kuliko vituo vingine..tatizo watumiaji na ubunifu ni zero!
 
Chonde chonde wakuu. Kufungwa tu hakutasaidia kujua kodi zetu zimepotelea wapi. Ni wakati wahusika wote wasulubiwe kwa kushindwa kazi. Hiki ni kituo kilichopata misaada mingi kutoka kwa hisani nje kwa sababu imebeba jina la tv ya taifa. Wameshindwa vipi na wengine ambao hawapati hizo ruzuku wamesimama vizuri tu ingawa kwa taabu.
 
Nkamia ni wakala wa shetani, mimi sijui hata anawakilisha masilahi ya nani. Nilianza kumsikia akimponda Zito kuwa mnafiki kwa kupinga posho, katika muda wote sikusikia hata hoja moja aliyotoa iliyokuwa na manufaa kwa wapiga kura wake kama posho hizo zingeongezwa, yeye yuko kimasilahi zaidi nadhani anajua akiendelea kujipendekeza anaweza kupewa hata ukurugenzi
 
Adhabu ya dhambi ni moto.
TBC ilipaswa kuwa chombo cha umma, kama ambavyo vilipaswa kuwa vyombo vyengine vya umma kama vile polisi na mahakama. Badala yake vipo kutetea chama tawala na kuwanyanyasa (mara nyengine hata kuwaua) wale waliowafanya wawepo hapa. Hata mbwa hatafuni mkono unaomlisha, lakini vyombo vya CCM vinautafuna, vinatafuna kodi zetu, vinatafuna jasho letu.

Licha ya kuwa wanapewa ruzuku za jasho letu na kama nyongeza, wanashindana kibiashara na TV/Radio binafsi, bado hawana pesa za kuviendesha, kunani? Srikali (ya/na CCM) ni kama gunia lililotoboka m.at.ak.on.i, kila ukitiacho kinavuja. Hakuna atakayeombolezaTBC ikifungwa (isipokuwa wale wanaofaidika na kuwapo kwake).
 
Ninashindwa kuelewa TBC pamoja na kupata ruzuku serikalini na kurusha matangazo ya biashara.. Inakuwaje wanakosa hela..? Lazima kuna ubadhirifu.. Maana TBC walikuwa wanalamba matangazo kibao.. Nakumbuka private tv stations walisha-raise issue ya TBC kurusha matangazo ya biashara huku wakiwa wanapewa ruzuku na kuomba either wapewe ruzuku tu au wasipewe ruzuku na kushindana na vyombo binafci kwa matangazo.. Serikali ikakataa.. Laana imewakuta..
 
Ifungwe tuu ili savings zitokanazo na kufungwa uko zitumike kununua madawati.
Tangazo moja la pre-news ni zaidi ya laki 4 sasa izo ela wanapeleka wapi?
Kuna haja ya kuwapiga chini
 
Back
Top Bottom