TBC Kufunga matangazo yake wakati wowote kutoka sasa

Jamani tuombe Mungu T.B.C ife kabisa kama kinavyo kufa ccm.kimekua kama dodoki la kusafisha uchafu na kuaribu demokrasia
 
Tatizo ilikuwa inabase mno kwa ccm hivyo kupoteza imani kwa wananchi/kutopenda kuitazama na kusababisha matangazo yakibiashara yaelekezwe kwenye tv zenye uzalendo.
Vipindi vingi vya kuonyesha mafanikio ya nchi ili kuonyesha ccm imefanya kazi sana ambavyo vilikuwa havilipiwi
naunga mkono kifo hicho ni mwanzo mzuri, bado tanesco, mamlaka za maji na baadae ccm
 
Kwani Mungu anabariki nini kati ya haki na udhalimu? Tbc+jk+wasira+kilango+EL+the like =UDHALIMU
 
Unamfukuza TIDO MHANDO unategemea nini katika ulimwengu huu wa sayansi na technologia? Hapo tbc ipo kama kopo tupu sasa tbc imekuwa mzigo usiobebeka. Tv imepoteza mvuto kabisa, ni bora utazame tv ya msumbiji hata kama wanazungumza kireno utapata faida sana kuliko tbc
 
Mmesema TBC au Tpc? Hilo ni shirika la sukari or? Maana huku kijijini tuna shida ya sukari!
 
Majungu, fitina na ubinafsi usiojali maslahi ya uma bali ya ushabiki na ujingaq wa viongozi wabinafsi unaliua shirika letu la utangazaji la TBC. Mnadhani TBC iliundwa hivyo itegemee rizuku tu? Unadhani uozo mlio nao mtauza chochote? Au mnadhani ni TV ya CCM hiyo? Mnakumbuka TBC ya Tido Mhando? Ndo mkombe kwa ujinga wenu viongozi, ngoja ife kama ATC ndon mtashika adabu halafu mkawapigie magoti akina Mengi... au labda CLOUDS watajilambalamba na kuwapa airtime kama wanavyofayna sasa hivi

TBC iliwahi kufika mahali ikawa juu kuliko vyombo vyote vya habari Tanzania nani anabisha? Je lilikuwa baya hilo? Inaniuma ndomana sichelei kuwatukana viongozi woooote waliohusika kumfukuza kiongozi na si mtawala aliyeleta mapinduzi ndani ya chombo cha uma. TBC 2 sasa hivi utumbo tupu hatuone documentary nzuri zilizotukumbusha historia yetu, mimi nilikuwa na TV ofisini kwangu kwa ajili ya TBC sasa hovi nimeitoa sioni cha kuangalia. Kwa TBC tuliyoifahamu hata bidhaa zangu na program nyingi nilikuwa napigania Airtime TBC sasa hivi hunishawishi hata kidogo kuepleka TBC ni kupoteza hela
 
Ngoja tu ife wajifunze. Chombo cha serikali wanakifanya cha magamba, nani apeleke matangazo pale?
 
TBCCM ndio mwisho na mtambue kuwa hatutaleta matangazo yetu hapo na tumegoma kuiangalia.mfunge mna boa!mna boa!mna boaaa
 
walivyo wabishi watakomaa hivyo hivyo na njaa yao..washenzi kabisa wale
 
Nafurahishwa na kufungwa kwa TBC kwani imepoteza mwelekeo ni aibu kwa taifa na mataifa mpaka sasa ni uozo mtupu unaofanyika hapo. Ila nawahurumia sana wafanyakazi wake pamoja na familia zao hali zao kiuchumi zitakuwaje ingawa siamini sana kwamba wengi wao walimudu kukidhi haja zao za kila siku za maisha.
 
Mbona sasa wanachelewa zaidi kuifunga, ningetamani sana kama taarifa hii ingesomeka kuwa "lililokuwa kuwa shirika la Utangazaji/utongazaji Tanzania limezikwa rasmi"
 
Back
Top Bottom