TBC: Huduma hospital Dar zaendelea kuimarika

TBC: Huduma hospital Dar zaendelea kuimarika

wakiripoti kutoka hospital za temeke, ilala na mwanyamala, wakiongea na wagonjwa waliokwenda kupata matibabu wengi wao wamekiri kupata tiba kwa wakati ila katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo huduma ilikuwa ya kusuasua.
Mdini naona upo hewani mmeshaanza ile sensa yenu? kwi! kwi! kwi! au mnaifanyia kwenye vijiwe vya kahawa
 
lakini wadau si tulikubaliana kwamba tusiendelee kuitazama TBC mana inatupotosha ila mbona maoni yenu yanaonesha kama vile bado munaitazama vile au?
 
wewe ndio wale wale cdm mnaochochea mgomo km ilivyodhihirika Leo bungeni na kutaka kumuua ulimboka

And that is your party's excellent move,! huh!? yaani mnajidanganya wenyewe afu mnafikiri mnawadanganya watanzania,watanzania wa sasa wanajua kupambanua pumba na mchele,haihitaji propaganda kuwaaminisha kile wanachoamini sicho!!
 
Tatizo ni kuchanganya taaluma na siasa na daraja ni haohao wanyonge ndio wanaolipa gharama na pia kodi zao ndio zinalipa mishahara yao .kunakitu kipo gizani . kwa manufaa ya kikundi fulani .
swala la taaluma ya udakitari. Kama ni kwa maoni yangu ni vema isitumike kama ni chombo cha kudhofisha upande moja au mwingine kisiasa. Bila kujali umuhimu wa taaluma yenyewe. Labda watanzania tunadhulumika kwa haki zetu mbali mbali. Tungetafuta namna nyingine kisiasa! Na wala si kwa taaluma hii.pia labda ndani ya madakitari kuna wana siasa au pia nje nako wapo.hivi ni kweli kuwa ni madakitari tu wenye madai serekalini? Waalimu?vyombo vya usalama police magereza wanainchi wa kawaida.kiujumla kote kuna mapungufu sasa tukigoma wote ni serekali ya chama kipi? Ita weza kutimiza yote hayo au sasa ni ule usemi wa bora ya mbaya unaye mjua kuliko malaika usiye mjua.wanainchi kazi kwetu sasa kutofautisha kipi? ni kipi?
 
ni ujinga kuendelea kuangalia TBC ukitegemea taarifa za kweli.

Nimeona TBC hawaoneshi na kutangaza matukio kwa uhalisia wake. Sielewi kama hawapati habari au hawaruhusiwi kutangaza kwa uhuru au wanakusudia kuficha ukweli ambao kwa kweli haufichiki.
Nimeshuhudia watu wengi wakiacha kutazama TBC na kutazama TV zingine ili kupata habari zenye ukweli na uhakika.
TBC mtarudishaje imani kwa watazamaji?
 
Ni ujinga na upuuzi kuendelea kuitazama TBC,hao ni vibaraka wakubwa wa mafisadi wote hao wanakufa rasmi 2015 TBC,COMMEDY,CCM,marine hassan
 
Kwa kuwa JF ni pahali pa kupeana taarifa, ziwe sahihi au za uongo,
Kwa kuwa kuna vyombo vingi vya habari zaidi ya TBC,
Kwa kuwa kuna watu wanaolifuatilia hili kwa undani na umakini,
Kwa kuwa kuna dhana kuwa TBC ni chombo cha propapaganda za serikali,
hivyo, ikiwa taarifa za TBC tunaona sio sahihi, ingekuwa busara kuleta taarifa mbadala, za upande mwengine; vyenginevyo wananchi wataamini "propaganda" za TBC ikiwa hakutakuwa na taarifa mbadala.
 
Serikali ndiyo iliyoanzisha mgoma kwa kugomea maboresho katika sekta ya afya. Kinachotokea kwa madaktari ni wao kushindwa kufanya kazi kutokana na mgomo wa serikali. HUDUMA BORA TUTAZIPATA SERIKALI IKIACHA MGOMO
 
Sio kituo cha kusikiliza wala kuangalia, nyie subirini tu ipo siku yatatokea kama yaliyotokea mali!!! tutalia na mmoja baada ya mwingine
 
TBC...Ukweli na uhakika!!!!!!!!
Kuna haja ya kutafuta maana ya maneno hayo kwani yanakanganya ukiangalia uhalisia wa tbc!!!
 
Mbona habari za saa itv wanasema hali inazidi kuwa mbaya kwenye hospitali za serikali especially muhimbili taarifa ya saa nane mchana
 
Breaking Nuuuuuuuuuz:





JULAI 2, 2012


Huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012.


Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.


Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizo


Upande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.


Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.


Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.


Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji..


KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.


Imetolewa na;




Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 2, 2012
4.jpg

Uongo hauwasaidii wananchi!!Hili ni tangazo la tar 2 July,madaktari bingwa MNH wameanza rasmi mgomo jana tar 3 July.Unaleta tangazo hli kwa faida ya nani??
 
tunashukuru madakatari wetu kwa kurudi kazini kuendelea na kazi kutibu watanzania wenzetu.
asante kwa kuwa mjinga we unaangalia wangapi wamesaini jiulezi utapewa huduma inayostahili wakati umewashikia kiboko wasaini ili upate data za kuonyesha amka ndugu yanhu
 
.CHADEMAAAAA,Mnatafuta Ikulu kwa udi na uvumba, .yaani hum ndani ukiandika taarifa hata ya ukweli ikiipinga CDM utashambuliwa tu. .Hawa wanataka kuwasifia hata vitu vya kijinga. .Munashinikiza migomo wakati mama dada,kaka,na jamaa wanakufa kwa kukosa matibabu. .hivi mnafikiria kweli au mnafuata mkumbo tu.
kumbe chadema ndo wamegoma!
 
Watu wengine huwa wanaudhi sana CDM inahusika vipi na mgomo wa madaktari? Ukiwa mwendawazimu siku zote utatangulizwa chini, kauli hizi ni za kichochezi. Waacheni wafe na ujue zamu yako kesho. Vibaraka wa serikari dhaifu mnakera sana.
Watu wanakufa kwa sababu yenu, mmejaa uongo, unafiki, mnadanganya taifa!! Mjue uongo unamwisho na hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho

Mkuu kuna watu wengine hawawezi kuona mambo ktk uhalisia wake, mtu anapimwa na kukutwa na vvu anaenda kwa mganga wa kienyeji kupiga lamli analidhika kuambiwa jirani yako ndo kakuloga,
 
Haya mambo ya madakatari, sasa inabidi yawe kama ya mtu na mke waka. Maana kila mtu anazungumza lake. Si wakae watoe tamko?
 
Back
Top Bottom