Ikonda Hospital vs Hospital ya Rufaa (Zonal) Mbeya

IamChasulwa

Member
Joined
Jan 3, 2026
Posts
12
Reaction score
17
IKONDA HOSPITAL VS HOSPITAL YA RUFAA (ZONAL) MBEYA

Habari ya wakati huu watubwa Mungu!!
Ni tumaini langu mko poa sana.

Naleta uzii huu kuuliza juu ya nini kinafanya hospitali hizi zinazopatika nyanda za juu kusini.

Ikonda kwa jina maaru ila inaitwa CONSOLATA HOSPITAL IKONDA,ipo huko mkoani Njombe.

Lakini Mbeya ZONAL Referral hospital (MZRH) hii hospitali ipo mkoani na katika jiji la Mbeya pale Greencity (Vumbi City kwa mujibu wa MC Mboneke) ni hospitali kubwa ya kanda kwa nyanda za juu kusini.

Sababu ya uzi huu ni kwamba naona wengi wanaitambua sana hospitali ya Ikonda kuliko Zonal Hospital

Nimeuliza kama watu 5 majibu yao kuhusu Ikonda yalikuwa kama haya:-

  • Mapokezi; kwamba ukifika Ikonda(Hospital) kuna watu wamevaa nguo zilizoandikwa NIULIZE MIMI. Jambo hili linamfanya mteja(mgonjwa) kutopata usumbufu
  • Utaratibu wa foleni. Wanasema,ukiwa pale kwenye foleni ya kusubiri kuonana na mtoa huduma(daktari) kuna mtu(daktari( anapita kutoa maelekezo kwamba fulani utaingia mlango namba fulani kwa ajili ya kupata huduma). Na ikipita muda bado haujaitwa anaenda kuona changamoto nini iliyopelekea kuchelewa kisha anakuhamisha chumba kingine cha daktari mana wana vyumba vingi vya madktari.
  • Muda wa kusubiri. Kwa wale waliopatiwa huduma/vipimo hawachukui muda mrefu kwani yupo mtoa huduma anapita mara kwa mara kuona kama watu wanapata huduma kwa haraka bila upendeleo.
  • Malazi, Ikonda wanalo bweni ambalo wagonjwa na wanao wahudumia wagonjwa (sio madaktari) wanaishi kwa gharama nafuu ya buku kwa siku na hii ji kwa wanaume na wanawake.

Hizi ni sababu ambazo wao wametoa,nkajaribu kuuliza kuhusu kuijua Zonal Hospital Mbeya,wengi hawaijui hasa watu kutoka nje ya Mbeya.

Wenye uelewa wa mambo haya naomba mje mnambie nini kinapelekea Mbeya ZONAL Referral hospital kutokuwa na jina Kubwa ikilinganishwa na Ikonda
 
hiyo nyingine unafia kwenye foleni ila nawewe kwann uchelewe usability usukumwe kwenye machela
 
N
Ikonda ni ile hospitali ya wamisionari wakonsolata? Ni hospitali nzuri sana labda kama siku hizi wameiharibu.
Ndio hiyo
Kuna ndugu amesema kwa sasa wako vibaya sababu wana-ubia na serikali ety
 
Wewe nenda unapoona panakufaa kulingana na imani yako bila kusahau hadhi yako na mfuko wako, wacha mbambamba.
 
Ikonda nasikia imeingia ubia na serikali imeanza kuharibika
MOU ilikuepo tangu zamani,Pale serikali inapeleka baadhi ya watoa huduma tu na sio issues za management.
 
Hao watoa huduma ndio wanafanya hospitali za serikali zinanuka rushwa
 
IKONDA HOSPITAL VS HOSPITAL YA RUFAA (ZONAL) MBEYA

Habari ya wakati huu watubwa Mungu!!
Ni tumaini langu mko poa sana.

Naleta uzii huu kuuliza juu ya nini kinafanya hospitali hizi zinazopatika nyanda za juu kusini.

Ikonda kwa jina maaru ila inaitwa CONSOLATA HOSPITAL IKONDA,ipo huko mkoani Njombe.

Lakini Mbeya ZONAL Referral hospital (MZRH) hii hospitali ipo mkoani na katika jiji la Mbeya pale Greencity (Vumbi City kwa mujibu wa MC Mboneke) ni hospitali kubwa ya kanda kwa nyanda za juu kusini.

Sababu ya uzi huu ni kwamba naona wengi wanaitambua sana hospitali ya Ikonda kuliko Zonal Hospital

Nimeuliza kama watu 5 majibu yao kuhusu Ikonda yalikuwa kama haya:-

  • Mapokezi; kwamba ukifika Ikonda(Hospital) kuna watu wamevaa nguo zilizoandikwa NIULIZE MIMI. Jambo hili linamfanya mteja(mgonjwa) kutopata usumbufu
  • Utaratibu wa foleni. Wanasema,ukiwa pale kwenye foleni ya kusubiri kuonana na mtoa huduma(daktari) kuna mtu(daktari( anapita kutoa maelekezo kwamba fulani utaingia mlango namba fulani kwa ajili ya kupata huduma). Na ikipita muda bado haujaitwa anaenda kuona changamoto nini iliyopelekea kuchelewa kisha anakuhamisha chumba kingine cha daktari mana wana vyumba vingi vya madktari.
  • Muda wa kusubiri. Kwa wale waliopatiwa huduma/vipimo hawachukui muda mrefu kwani yupo mtoa huduma anapita mara kwa mara kuona kama watu wanapata huduma kwa haraka bila upendeleo.
  • Malazi, Ikonda wanalo bweni ambalo wagonjwa na wanao wahudumia wagonjwa (sio madaktari) wanaishi kwa gharama nafuu ya buku kwa siku na hii ji kwa wanaume na wanawake.

Hizi ni sababu ambazo wao wametoa,nkajaribu kuuliza kuhusu kuijua Zonal Hospital Mbeya,wengi hawaijui hasa watu kutoka nje ya Mbeya.

Wenye uelewa wa mambo haya naomba mje mnambie nini kinapelekea Mbeya ZONAL Referral hospital kutokuwa na jina Kubwa ikilinganishwa na Ikonda
Fr. Sandro apewe maua yake
 
Nenda Ikonda ya Mbagala mission,al maarufu Kwa Buruda,ndo haohao,huduma bomba sana.
 
Nilienda Ikonda Mei mwanzoni...pako vyema...Ila nilishangaa watu wanaota moto saa Saba mchana.
 
Back
Top Bottom