Hizi ni propaganda chafu na ni aibu kuona raisi dhaifu anadiriki kudanganya umma kuhusu mgomo wa madarakani. Bila aibu raisi anadiriki kusema kuwa madaktari wasiotaka kazi waondoke? Je, anayepata hasara katika hili ni nani? Si ni Tanzania ambayo inapoteza maisha ya Watanzania wasio na hatia na vilevile kupata hasara kwa pesa ilizotumia kusomesha madaktari hao? Kiongozi wa nchi mwenye uzalendo angaliona hilo lakini huyu hana uzalendo na ndiyo maana yeye kila siku ni kiguu na njia. Yeye na serikali yake hawana uwezo wa kutatua matatizo bali kuongeza matatizo na kutugawa Watanzania katika misingi ya udini, ukanda, ukabila, rushwa na ufisadi. Ni lazima tuamke na kudai kuwajibika kwa serikali hii. Madaktari wana haki ya kudai masilahi bora na hakuna aina yoyote ile ya vitisho itakayoweza kubatilisha haki ya madaktari. Propaganda chafu za TBC na magazeti udaku ya Daily News, HabariLeo na Uhuru hazitafanikiwa.