TBC: Huduma hospital Dar zaendelea kuimarika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC: Huduma hospital Dar zaendelea kuimarika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Jul 2, 2012.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,520
  Trophy Points: 280
  Jamani huu upuuzi mpaka lini??
   
 2. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwamba huduma ya afya hospitali za serikali yaendelea kuimarika na huku tamko la madkatari bigwa ni kuendelea kugoma?
   
 3. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Katika taarifa yake tbc wanadai hali ya huduma katika hospitali zimeanza kutengemaa, wakati ktk tv station tukioneonesha madaktari bingwa wakitangaza mgomo.
   
 4. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,520
  Trophy Points: 280
  Unaweza kuchoma kituo hivihivi
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  wewe ndio wale wale cdm mnaochochea mgomo km ilivyodhihirika Leo bungeni na kutaka kumuua ulimboka
   
 6. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ni ujinga kuendelea kuangalia TBC ukitegemea taarifa za kweli.
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Madaktari walio kuwa likizo wamerudi kazini na wanachapa mzigo huko sio kuimarika? Acha kuwa kibaraka wa cdm wanaochochea mgomo na kutaka kumuua ulimboka
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Na yule dokta aliyekuwa anaongea Muhimbili nje aliyeoneshwa walimbandika maneno? huna haya?
   
 9. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Wanajaribu kuuficha moto wakati moshi unafuka...
   
 10. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Na ulaaniwe na akili yako hii ya kitumwa. Siku zenu zimekwisha na mtateseka sana na TBC yenu na hao watangazanji wenu vibaraka wa wauaji
   
 11. Mwananchi wa Kawaida

  Mwananchi wa Kawaida Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  we ndo kichaa na mjinga unayeamini TBC1,una hisa huko?Amka kifikra unaachwa na dunia
   
 12. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Madaktari bingwa wametoa tamko kwamba wamegoma, TBC1 wanadai hali imeimarika! Kweli Tanzania ya Dhaifu ni zaidi ya uijuavyo! Au wamemchukua yule aliyekuwa waziri wa habari wa Saadam, Alsahaf, a.k.a "Comical" Ally kuwa mkurugenzi mkuu wa TBC!
   
 13. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Watu wengine huwa wanaudhi sana CDM inahusika vipi na mgomo wa madaktari? Ukiwa mwendawazimu siku zote utatangulizwa chini, kauli hizi ni za kichochezi. Waacheni wafe na ujue zamu yako kesho. Vibaraka wa serikari dhaifu mnakera sana.
  Watu wanakufa kwa sababu yenu, mmejaa uongo, unafiki, mnadanganya taifa!! Mjue uongo unamwisho na hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho
   
 14. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Na ulaaniwe na akili yako hii ya kitumwa. Siku zenu zimekwisha na mtateseka sana na TBC yenu na hao watangazanji wenu vibaraka
   
 15. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hizi siyo enzi za kudanganyana. Kuna njia na namna nyingi za kupata habari. Ukiudanganya umma, utaumbuka tu!
   
 16. Jaffary

  Jaffary JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 758
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Wakati tukisikia kwamba madaktari bingwa wamegoma tbc bila aibu wanasema hali imezidi kuimarika, mnamdanganya nani na kwa maslahi ya nani?
   
 17. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Breaking Nuuuuuuuuuz:  [​IMG]


  JULAI 2, 2012


  Huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012.


  Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.


  Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizo


  Upande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.


  Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.


  Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.


  Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji..


  KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.


  Imetolewa na;
  Aminiel Buberwa Aligaesha
  Afisa Uhusiano Mwandamizi
  Julai 2, 2012
  [​IMG]
   
 18. Small Boy

  Small Boy Senior Member

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Najuuuuuuuuuta Kuangalia TBC1
  Yani kuimarika ni watu kutudi toka likizo? wangapi walikuwa lilizo? Nchi hii propaganda za DHAIFU zimezidi xana
   
 19. MANI

  MANI Platinum Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  TBC imepoteza weledi wa kuwa chombo huru cha serekali inajaribu kukinga upepo kwa wavu sijui kama itawezekana!
   
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  tbc ni janga la taifa
   
Loading...