TBC 1 kwenye matukio ya LIVE mjirekebishe

TBC 1 kwenye matukio ya LIVE mjirekebishe

AKILI TATU

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2016
Posts
2,666
Reaction score
2,841
Kwenu UONGOZI wa TBC ,tokea mbadilishwe jina kutoka TVT hadi TBC ni zaidi ya miaka 10 sasa,lakini namna mnavyorusha matangazo yenu hamna tifauti kabisa na TVT,hakuna mlichobadilika hata kidogo.

Matangazo yenu ya LIVE au mubashara yanatia kichefuchefu,kwanza nadhani mnakuwa na kamera moja tu wakati wenzenu wanakuwa na zaidi ya kamera moja zinazokuwa katika angle tofauti tofauti,au kama mnakuwa na kamera nyingi,kuna haja ya kuachana na hao makamera wenu uchwara ambao hawajui namna ya kuchukua matangazo ya LIVE.

Au kama sio hao makameraman wenu,basi huyo mchanganya picha wenu hafai hata kidogo,maana haiwezekani tukio ambalo mtazamaji anahaki ya kuliona karibu ninyi bado mnalionyesha mbali.huo ni uzwazwa .

Lakini pamoja na hayo hao Watangazaji wenu wa matangazo ya LIVE warudi darasni,maana hawajui na hawana ethic za kurusha matangazo ya LIVE,haiwezekani kwenye tukio la LIVE kiongozi,au MC wa shughuli anaongea na yeye naye anaingiza sauti yake.

Hakika ,ndugu Ayoub Rioba kuna haja ya kuliangalia suala hili ili kujenga shirika bora naloendana na ushindani wa ukuaji wa kasi ya matangazo ya moja kwa moja,yaani LIVE.
 
Alafu wanapewa ruzuku ya serikali wakati wenzao wengine hawapati kitu na kodi wanalipa.

ife mi naomba ifeee kabisa nayo TBC taifa redio nayo majanga nasema ifee haiwezekani
 
Mkuu acha tu hii ni aibu tena kubwa kabisa nilikuwa naangalia kupitia YOUTUBE nashangaa jamaa anafuta camera na tambala kwa kweli ni aibu sana!
 
Ivi TBC bado ipo [emoji23] isije kua kama channel ten tv special kwa matangazo tu
 
yani siku hizi imekuwa kerooo naangalia hapa LIVE yao ya kutua kwa ndege,kameraman akijua kabisa tukio lipo live anachukua kitambaa anafuta kamera,yani ni uboya sijapata kuona
Ha ha ha eti anafuta waaatt
 
Sikio La Kufa Halisikii Dawa
Ndiyo Tbc
🙁😡
 
Hii TBC 1 ya taifa ni janga sana.

Unakuta matukio muhimu ya kitaifa TBC inakwama kwama, picha mbovu.

Lakini pia TBC kwa ujumla wanakosa ubunifu kabisa.

Yaani anashindwa na JF inakuwa live kwenye mitandao, yaani TBC wao wanashindwa hata kuwa live facebook?

Mamlaka husika wamfute kazi, weka kijana mbunifu mwenye maono kama Mh. rais
 
World cup sasa inayoonyeshwa na TBC uchafu uchafu tu,

Television ya Taifa inasikitisha sana.

Nilimtazama Ayoub Rioba siku kadhaa zilizopita akadai wako mbioni kuboresha kilakitu ndani ya TBC.
 
Jiweke kwny nafasi yake alaf usome ulichokiandika..
 
World cup sasa inayoonyeshwa na TBC uchafu uchafu tu,

Television ya Taifa inasikitisha sana.

Nilimtazama Ayoub Rioba siku kadhaa zilizopita akadai wako mbioni kuboresha kilakitu ndani ya TBC.
Anakosa ubunifu. Kuna gharama gani kuwa live facebook? au Youtube?? Yaani Rioba is not creative
 
Mudawote,

Nadhani jibu litakalo tegemewa ni fedha kiduchu shirika linapewa.

Inabidi atie ubunifu katika kusimamia TBC,basi hata miradi mbalimbali ili waweza kujiendesha vyema.
 
Mudawote,

Nadhani jibu litakalo tegemewa ni fedha kiduchu shirika linapewa.

Inabidi atie ubunifu katika kusimamia TBC,basi hata miradi mbalimbali ili waweza kujiendesha vyema.
Fedha kidogo kwa haiyo shirika haliingizi
 
Back
Top Bottom