TBC 1 kwenye matukio ya LIVE mjirekebishe

TBC 1 kwenye matukio ya LIVE mjirekebishe

Wako ovyo sana halafu ajabu ndiyo wanapewa exclusive right ya kurusha yale matukio nyeti ya nchi!!
 
Hao watangazaji wao huwa wananiudhi sana linapokuja suala la Mubashara, yani MC wa shughuli husika anaongea na yeye anarudia yaleyale yanayozungumzwa na MC... sasa kwanini asikae kimya ili tusikie MC anasema nini.

Taarifa ya habari imekuwa kama KWAYA, yani wanaimba na kupokezana halafu wanaanza kujadili taarifa waliyoisoma, utasikia wanasema "unaonaje tukio hili alilolifanya Mh Rais?" mwenzake anaanza kumjibu..
Tutangazieni tutajadiliana wenyewe, msifanye uchambuzi wa habari wakati taarifa bado haijakwisha
 
Mudawote,

Nadhani jibu litakalo tegemewa ni fedha kiduchu shirika linapewa.

Inabidi atie ubunifu katika kusimamia TBC,basi hata miradi mbalimbali ili waweza kujiendesha vyema.
hilo nalo pia hadi JPM awaagize
 
Kuliko kuangalia TBC huwa natafuta nyimbo za Kimasai nasikiliza japo sielewi ila nahisi ni bora kufanya hivyo.
 
Mkuu acha tu hii ni aibu tena kubwa kabisa nilikuwa naangalia kupitia YOUTUBE nashangaa jamaa anafuta camera na tambala kwa kweli ni aibu sana!
i saw that nimecheka balaaa
 
Hii TBC 1 ya taifa ni janga sana.

Unakuta matukio muhimu ya kitaifa TBC inakwama kwama, picha mbovu.

Lakini pia TBC kwa ujumla wanakosa ubunifu kabisa.

Yaani anashindwa na JF inakuwa live kwenye mitandao, yaani TBC wao wanashindwa hata kuwa live facebook?

Mamlaka husika wamfute kazi, weka kijana mbunifu mwenye maono kama Mh. rais
TBC ni hewa sana, wafanyakazi wenyewe ilibidi waone aibu. Kila siku wao ndio wanalalamikiwa, maybe wawapeleke training
 
Kwenu UONGOZI wa TBC ,tokea mbadilishwe jina kutoka TVT hadi TBC ni zaidi ya miaka 10 sasa,lakini namna mnavyorusha matangazo yenu hamna tifauti kabisa na TVT,hakuna mlichobadilika hata kidogo.

Matangazo yenu ya LIVE au mubashara yanatia kichefuchefu,kwanza nadhani mnakuwa na kamera moja tu wakati wenzenu wanakuwa na zaidi ya kamera moja zinazokuwa katika angle tofauti tofauti,au kama mnakuwa na kamera nyingi,kuna haja ya kuachana na hao makamera wenu uchwara ambao hawajui namna ya kuchukua matangazo ya LIVE.

Au kama sio hao makameraman wenu,basi huyo mchanganya picha wenu hafai hata kidogo,maana haiwezekani tukio ambalo mtazamaji anahaki ya kuliona karibu ninyi bado mnalionyesha mbali.huo ni uzwazwa .

Lakini pamoja na hayo hao Watangazaji wenu wa matangazo ya LIVE warudi darasni,maana hawajui na hawana ethic za kurusha matangazo ya LIVE,haiwezekani kwenye tukio la LIVE kiongozi,au MC wa shughuli anaongea na yeye naye anaingiza sauti yake.

Hakika ,ndugu Ayoub Rioba kuna haja ya kuliangalia suala hili ili kujenga shirika bora naloendana na ushindani wa ukuaji wa kasi ya matangazo ya moja kwa moja,yaani LIVE.
Huyu Ayoub Rioba huwa anakuja humu jukwaani kweli?? Yaani natamani aje aone jinsi tunavyochukizwa na utendaji wake mbovu, yaani wanajiendesha utadhani RTD, yaani inakuwa ni bora enzi za akina jangala na akina Kihemba kuliko huyu anayejiita Dkt halafu ubunifu zero. Yaani hawana marketing strategy wala communication strategy, yaani Tido atakumbukwa sana tena sana.
 
Huyu Ayoub Rioba huwa anakuja humu jukwaani kweli?? Yaani natamani aje aone jinsi tunavyochukizwa na utendaji wake mbovu, yaani wanajiendesha utadhani RTD, yaani inakuwa ni bora enzi za akina jangala na akina Kihemba kuliko huyu anayejiita Dkt halafu ubunifu zero. Yaani hawana marketing strategy wala communication strategy, yaani Tido atakumbukwa sana tena sana.
kabisa yani
 
Tv za bongo zote ni vihiyo with exception to Azam.Wanashindwa ata kufanya live streaming online kwa kutumia Facebook live,YouTube live twitter periscope or Apps.Televisheni nowadays zipo kwenye viganja vya mtumiaji yani kwa kutumia simu kutokana na pirika za kimaisha.Kwa mfano mtu anatoka kazini jioni,anataka kurudi nyumbani kuwahi taarifa ya habari but unfortunately anakwama kwenye foleni.Hana window nyengine bali kukosa habari.

Hile App ya ITV na yenyewe chali.Haifanyi kazi tena.Clouds,EATV na TVE zenyewe ata azijiusishi tena na online streaming lakini wanavitengo vya digital na watu wanalipwa mishahara.Wanashindwa ata kutengeneza app.

Tv zote za Kenya na Uganda zipo kwenye digital platforms.Tanzania only Azam.Shame.
 
Back
Top Bottom