TB Joshua kiboko!

TB Joshua kiboko!

Siku Ukijitambua Utamjua Tb Joshua Ni Mtumishi Wa Mungu, Kama Hujawahi Kumsikiliza Na Kusoma Bible Utapga Porojo Najua Kwakua Unaongozwa Na Mapepo, Tangu Lini Jambazi Akamsapoti Mtumish Wa Mungu
 
Emmanuel TV nimekuwa naiangalia kwa muda mrefu sasa, nadhani kabla watu wengi wa humu jamvini hawajaanza kuitazama. Je unakumbuka siku moja hiyo TV ilitoa kioja eti mwanamke aliyepimwa hospital kuwa ana uvimbe kwenye tumbo la uzazi na alipokuja kwa maombi basi ule uvimbe ukaanza kumtoka kupitia sehemu zake za siri na TV ikawa inaonyesha live. Naona anaona alifanya kioja siku hiyo ndio maana siku hizi anasema huo uvimbe unayeyuka kwa jina la Yesu. Mbona wakati ule haikuwa hivyo? Amejifunza kuwa watu walimshangaa. Kuna maswali machache kuhusiana na huduma ya TBJ ambayo hakuna mfuasi wake anawezakutoa jibu . Maana yake ni kwamba hata hao wafuasi wake wana mashaka. Inaelekea wafuasi wengi wa TBJ hawajasoma Bible kwanza na wanakuja moja kwa moja kukutana naye ndio maana wanashindwa kuhoji anayoyafanya. Ufahamu kuwa hata kama kweli kuna mijuiza inayofanyika kwenye sinagogi lake SIO LAZIMA ITOKE KWA MUNGU, HATA SHETANI ANAFANYA MIUJIZA VILEVILE. Petro na Yohana wlipofika mlangoni mwa hekalu wakakuta kiwete anaomba pesa walimponyesha, lakini huyu jamaa watu wanakuja kwenye sinagogi lake wakiwa viwete anawapa mchele na pesa. Haya wafuasi wa TBJ kwa nini asiwatibu kama wale mitume wa Yesu? Wale viwete anaodai kuwaponyesha wanaonyeshwa kwenye TV kuanzia wanapoanza kuingia mlangoni mpaka wanapokaa na hata muda unaoitwa wa uponyaji, kama sio fix ni nini? Biblia inasema imani huja kwa kusikia Neno la Mungu sio kusikia shuhuda. Sasa huyu mtaalam TBJ muda mrefu ni shuhuda na unabii neno linasomwa chini ya 5% ya muda wa TV. Na hata anapofafanua neno la Mungu, kwa mtu aliyeisoma hiyo Bible kisawasawa anabaki na maswali mengi ya kujiuliza kuhusu uelewa wa huyo anayejiita nabii. Yesu alipoponyesha watu aliwaambia wasimweleze mtu, mbona TBJ muda wote ni testimony? Toeni majibu. Anointing water ya zamani na ya sasa zina tofauti gani, ni katika maombi au ni katika materials? Sisi Wakristo tumeonywa kuwa ukimwona mtu anaangamia ukamwacha bila kumpa tahadhari basi ujue damu yake itakuwa juu yako. Wale wafuasi wa TB Joshua nawapa tahadhari kuwa mnayemfuata hana uhusiano na utumishi wa Mungu aliyeainishwa katika Bible, labda mungu mwingine ambaye Amri ya kwanza ya Mungu wa Bible inakataza kabisa kumwabudu.

Wewe ni mkristo...I second you.
 
Nasikia ametabir nchi inayoanza na C na kuishia na N ndo bingwa wa dunia fifa lkn inayosemwa tayar imeondoshwa
 
Ndo maana hua waandishi wa Tz mnaitwa makanjanja toka asubuhi umeunga mkono ajira kwa watoto mererani eti wanatafuta rizik wakati wanatakiwa kua wako shuleni hua nakueleza wewe unaandika bila tafiti na kama ni tafiti unafanya ukiwa kifua wazi basi.
 
Yesu Kristo, ndiye kiboko na siyo T.B Joshua !
Yesu alitabiri kusulubiwa,kufa,kuzikwa, kufufuka;HALELUYA !
[MT 16:21-23]
 
TB joshua ni msanii kama wacheza mazingaombwe wengine
 
Siku Ukijitambua Utamjua Tb Joshua Ni Mtumishi Wa Mungu, Kama Hujawahi Kumsikiliza Na Kusoma Bible Utapga Porojo Najua Kwakua Unaongozwa Na Mapepo, Tangu Lini Jambazi Akamsapoti Mtumish Wa Mungu

Nasikia eti Gwajima anafufua misukule.....Ni kweli...???
 
kwaiyo unataka kusema ata mzee wa upako nae noma sana maana nae katabiri mengi kama vile marehemu sheikh yahaya
 
Emmanuel TV nimekuwa naiangalia kwa muda mrefu sasa, nadhani kabla watu wengi wa humu jamvini hawajaanza kuitazama. Je unakumbuka siku moja hiyo TV ilitoa kioja eti mwanamke aliyepimwa hospital kuwa ana uvimbe kwenye tumbo la uzazi na alipokuja kwa maombi basi ule uvimbe ukaanza kumtoka kupitia sehemu zake za siri na TV ikawa inaonyesha live. Naona anaona alifanya kioja siku hiyo ndio maana siku hizi anasema huo uvimbe unayeyuka kwa jina la Yesu. Mbona wakati ule haikuwa hivyo? Amejifunza kuwa watu walimshangaa. Kuna maswali machache kuhusiana na huduma ya TBJ ambayo hakuna mfuasi wake anawezakutoa jibu . Maana yake ni kwamba hata hao wafuasi wake wana mashaka. Inaelekea wafuasi wengi wa TBJ hawajasoma Bible kwanza na wanakuja moja kwa moja kukutana naye ndio maana wanashindwa kuhoji anayoyafanya. Ufahamu kuwa hata kama kweli kuna mijuiza inayofanyika kwenye sinagogi lake SIO LAZIMA ITOKE KWA MUNGU, HATA SHETANI ANAFANYA MIUJIZA VILEVILE. Petro na Yohana wlipofika mlangoni mwa hekalu wakakuta kiwete anaomba pesa walimponyesha, lakini huyu jamaa watu wanakuja kwenye sinagogi lake wakiwa viwete anawapa mchele na pesa. Haya wafuasi wa TBJ kwa nini asiwatibu kama wale mitume wa Yesu? Wale viwete anaodai kuwaponyesha wanaonyeshwa kwenye TV kuanzia wanapoanza kuingia mlangoni mpaka wanapokaa na hata muda unaoitwa wa uponyaji, kama sio fix ni nini? Biblia inasema imani huja kwa kusikia Neno la Mungu sio kusikia shuhuda. Sasa huyu mtaalam TBJ muda mrefu ni shuhuda na unabii neno linasomwa chini ya 5% ya muda wa TV. Na hata anapofafanua neno la Mungu, kwa mtu aliyeisoma hiyo Bible kisawasawa anabaki na maswali mengi ya kujiuliza kuhusu uelewa wa huyo anayejiita nabii. Yesu alipoponyesha watu aliwaambia wasimweleze mtu, mbona TBJ muda wote ni testimony? Toeni majibu. Anointing water ya zamani na ya sasa zina tofauti gani, ni katika maombi au ni katika materials? Sisi Wakristo tumeonywa kuwa ukimwona mtu anaangamia ukamwacha bila kumpa tahadhari basi ujue damu yake itakuwa juu yako. Wale wafuasi wa TB Joshua nawapa tahadhari kuwa mnayemfuata hana uhusiano na utumishi wa Mungu aliyeainishwa katika Bible, labda mungu mwingine ambaye Amri ya kwanza ya Mungu wa Bible inakataza kabisa kumwabudu.

Sasa Yupi ni wa Kweli. . AU hawapo Duniani?
 
jamani yanayofanywa na hao wakina TBJ na wenzanke yaliandikwa kwenye biblia kuwa baada ya yesu watakuja watu wa aina hiyo?
 
Acha kusikiliza maneno ya watu watakupoteza, kama una tv yako tafuta channel inaitwa emmanuel.tv , angalia kisha tafakari.
 
Mbona mimi nilitabiri timu za Africa hazitafika robo fainali kombe la dunia na kweli hazijafika...! Basi mimi kiboko
 
Mtu anaona mawingu yametanda afu anatabiri mvua itanyesha..! Ni kiboko pia?
 
Afanye maombi jamana mabinti waliotekwa warudishwe.
 
yesu alishasema kutakuja kuwapo na manabii wa uwongo( T B JOshua) nao wataonesha ishara za maajabu
cshanga kuona mkristo akiangukia kwa mpuuz ka tb josh coz najua aidha ni mvivu kusoma bible au hafuat mafundisho ya bble
 
Ok ila Pia Yesu hakusema kuwa Wote ni Manabii wa Uongo... ila alitupa Sharti kuwa Tutawatambua kwa Matendo yao..
sajumo

Maana kama Tutaendelea kusema kuwa Yesu alisema watakuja manabii wa Uongo na sisi Kila Tumuonapo Mtumishi anahubiri na kufanya miujiza Tukasema waongo basi Duniani hakutakuwa na Ukombozi wowote ule alioleta Kristo maana kuna Mambo ambayo Binadamu hatuwezi kuponya Au kuyatatua ila Yesu Kristo Pekee. Sasa kama wote ni Wa uongo basi hakuna Ukombozi au Ishara ya Kuwa Bado Yesu Yu hai nasi.

Kwahiyo inabidi tusikurupuke tu na Kusema kuwa ni Nabii wa Uongo ila tuchunguze kuwa kama Yatoka kwa Mungu wa ukweli ambaye ni Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa Kuangalia Matendo yao na Kuuliza baadhi ya Waumini wa karibu na kusikiliza Testimonies mbalimbali na kuzichunguza kama ni za kweli au ni maigizo tu..

MFANO

Nabii wa Uongo siku zote hadumu. Utamjua tu kama ni Mpenda Sadaka, Mwongo, Anaabudu Sanamu (pesa, usherati, mchawi ). Anatumia Nguvu za Giza kutuliza Mapepo si kuyatoa n.k

Hawa wahubiri wapo hapa Tanzania na tunawafahamu..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom