Tatizo ni CCM kupoteza jimbo la Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo ni CCM kupoteza jimbo la Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Rula, Nov 2, 2011.

 1. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  WanaJF kwa heshima na taadhima naomba tujadili juu ya tatizo la vurugu zinazolikabili jiji la Arusha kila mara. Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa vurugu katika jimbo hili la Arusha zilianza wakati wa kutangaza matokeo.

  Kwa walio Arusha ni mashahidi wa hili, ilitumika nguvu nyingi sana hadi Mh. G. Lema kutangazwa mshindi! Nakumbuka Mbowe na Ndesamburo walikuja kuokoa jahazi katika hili. Wakati watu wakishangilia nilishawahi kupost thread inayosema Dr. B. Burian angekwenda kupinga matokeo hayo mahakamani lakini watu walipuuza.

  Leo hii Mbunge G. Lema anapambana na kesi mahakamani juu ya kutumia lugha chafu na kukiuka taratibu nyingine za uchaguzi ambayo matokeo yake ni kutengua matokeo. Sipendi kuwa mwanahistoria ila ninachokusudia kuwafikishia ni hili, CCM IKUBALI MATOKEO YA ARUSHA NA IACHE MBINU CHAFU za nje ya majukwaa. Tangu CCM ishindwe jimbo la Arusha imekuwa ikihuzunika kama vile imeshindwa uchaguzi wa urais na kuja na mbinu nyingi za kuondoa amani katika jimbo hili ili G. Lema aonekane ni mbunge mhuni ambaye hana utulivu na kila kukicha yeye na makesi. Ukiangalia hili linathibitishwa na kesi alizonazo Lema ambazo nyingine ni kama hazina msingi na zenye msingi zinaachwa, mf ulio wazi ni issue ya umeya.

  Kutokana na hali jinsi ilivyo inawezekana kabisa G. Lema akashindwa kesi hii na kuvuliwa ubunge kama Nape alivyojitamba kuwa wametoka Igunga sasa kambi zitahamia Arusha! Tatizo mpaka leo halijaeleweka ni nini mpaka CCM inaling'ang'ania jimbo hili kwa udi na uvumba, sasa endapo hili litatokea natoa wito kwa CDM kufanya maamuzi magumu kwa kumuomba Dr. Slaa aje agombee ubunge ili kuhakikisha jimbo hilo haliangukii mikononi mwa CCM na kuwa salamu kwa CCM kushindwa uchaguzi hata kabla ya kura kupigwa.

  Hivyo
  inaonekana Arusha pasipo na mashika tatizo ni CCM kushindwa uchaguzi uliopita wa ubunge na si Lema kama wengi wanavyodhani. Nachelea kusema Arusha kuna siri kubwa sana ya kimaslahi iliyojificha ambayo inaleta haya yote, na ninawahakikishia kama Lema atamaliza miaka mitano ya ubunge wake itakuwa ni ya mikiki mikiki hivi hivi ili akigombea 2015 aonekane ni mbunge ambaye han utulivu.

  Nawasilisha wakuu,
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  You might be right kwa maana ya mbinu ya ccm kumfanya Lema aonekane hafai, but the way I see wananchi wa Arusha wako mbali mno kiuelewa! mbali zaidi ya hata wananchi wa Igunga so itakuwa ngumu still CDM watashinda, hata hivyo Lema anapaswa kuwa extra careful, sawa unapambana na mfumo dhalimu lkn lazima kuwe na ustahimilivu/utulivu wakati wa same mapambano,,,kuna staha flani inayotarajiwa kutoka kwa MBUNGE despite all injustices!
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Hili janga la makesi ilishaonekana kama unavyosema,,,,,,,,ubambikizaji wa kesi lukuki kwa (MB) tangu awali ilikuwa wazi kbs! Lakini nakwambia ktk mtazamo wangu wa kusoma alama ya nyakati hakika sisiem wakikomboa hili jimbo labda hawa Wafu wafufuke

  (1) Hayati Edward Moringe Sokoine

  (2) Hayati Julias Kambarage Nyerere

  (3)Hayati Abeid Karume

  Na waje waendeshe kampeni hapa kwa chama cha CCM na tofauti na hapo yani nakwambia hawa mapapa walijiwekeza ktk kila corner ya A town kwa makampuni na hata kutuulia viwanda kisa wajineemeshe wao,,,,,,,,,,,,,,yani wasikiage jimbo la Arusha Mjini kwa WAKOMBOZI wengine tu!

  Na kama ulivyokwisha sema ya kwamba wanaweza wakamrundikia kesi sisiso na mbele wala nyuma,,,,,,hapo ndipo patakuwa patamu na itakuwa fundisho kwao na wengine waigao. Hebu tuwasubiri na wadau maana najua wamo wamejaa na wenye kutaka mabadiliko.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Arusha ni jimbo la maslahi kwa mafisadi.

  Lakini pia Kijana G.Lema ni mwiba mbaya sana pale mjengoni Dodoma, si kwa spika, si kwa mawaziri, si Waziri Mkuu, haogopwi mtu!

  Hivyo kuna Mpango-Mkakati ambao baadhi yA watu hawalali wakikesha kubuni mbinu mpya za kumtia matatizoni Lema.
  Safari ni ndefu, na inahitaji uvumilivu.

  Ni kweli Dr.Slaa anaweza kushinda kirahisi Arusha, lakini uwepo wa Lema kama Mbunge wa Arusha na kama mwanaharakati Bungeni una hamasa ya pekee nchini!
  Naamini nchi hii nzima imeshachota mafunzo mengi kutokana na harakati, matamshi na mafunzo adimu anayotoa Lema!
  Lakini zaidi ni Ujasiri wake na kukataa kuburuzwa, ambapo asilimia 97 ya wabunge hawana guts hizo!

  Tanzania na Arusha zinamuhitaji Lema, na natabiri shida kubwa sana mbele ya safari iwapo maadui watafanikiwa kumtoa kwenye nafasi hiyo kwa mkono uliofichama na siasa za kichawi.
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Nakwambia wamekutana na kisiki cha Mpingu!
   
 6. N

  Ngoiva Lewanga Senior Member

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pamoja na maslahi binafsi, lazima tutambue kuwa mratibu wa hayo mambo yote ''lowassa''. Anajitahi kumuandaa ''kimada'' chake kwa uchaguzi ujao. Tusimtafute mchawi yuko wapi, huku unakula naye.
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hilo nalo limeongeza chuki kubwa sana juu ya Lema hasa pale alisema kuwa PM amedanganya bunge na kulazimika spika kumtupia taulo PM maana alikuwa uchi. Hakuishia hapo wakati akiwasilisha bajeti kivuli Wizara ya Mambo ya Ndani aliongea mengi yalioishitusha serikali na kuifanya imkodolee jicho la umakini. Zaidi ya yote kwa jinsi alivyo na maono na uhamasishaji wa ukombozi wa taifa hili basi ndiyo imekuwa shida tupu.
   
 8. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba G Lema ndie anasababisha vurugu kwa hulka yake ya kutoamini ktk sheria na taratibu. Mbunge inabidi awe mfano kwa anaowaongoza na kazi ya kwanza ya kiongozi ni kuhubiri amani ili maendeleo ya kweli yaweze kupatikana.

  Kama hakuna amani kwa anaowaongoza basi huyo mbunge hana uongozi. Kwa kifupi Lema atachokwa si muda mrefu na wapiga kura wake.
   
 9. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  G lema ndo jesh la polisi?
  Yeye ndo cCM?
  Yeye ndo OcD KUBERI?
   
 10. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni hidden technique inayotumiwa na CCM kumpaka matope lakini mwisho wake utakuwa aibu. Kuhusu kuhubiri amani ambako umekuhusianisha ma maendeleo huo ni uongo wa mchana. Kabla ya Lema alikuwepo Felix Mrema yaani miaka kumi yake Arusha ni kama haikuwa na mbunge yaani hakukuwa na maendeleo mpaka Arusha ilinyang'anywa hadhi ya jiji! Na kama ni vurugu basi zisiwe za upande mmoja na tafsiri yake ieleweke siyo hawa wakimsindikiza mgombea wao toka mahakamani wameandamana lakini UVCCM hawajaandamana.
   
 11. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sehemu niliyo bold tena kuwaita wananchi panya ni lazima kuna mtu anampa kiburi au ndiyo kutekeleza siasa za maelekezo kwamba hakikisha fulani hafurukuti.
   
 12. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja..ccm wanaumia sana kukosa jimbo la Arusha mjini na wana2mia mbinu nyingi chafu kumchafua mbunge wetu.Mungu mlinde mbunge wetu
   
 13. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Lema has shown by example how one needs to fight for his own right but he still needs much support from other members. Most of the so called pro-democracy activists are merely vocal only when in the social media but so trepid in the outside world. Lema's voice is not sufficient enough to represent the entire oppressed community meaning that more people should come out boldly and prop him up in his battle against what explicitly seems to be persecution by the government on its own citizens.
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Miaka mitano iliyopita hatukuwa na watu dizaini ya Lema lakini leo wapo, hivyo ni matarajio yangu sauti yake ni mwanzo wa uamsho wa ujinga uliowajaa wengi. Baada ya muda si mrefu watakuja wapiganaji wengine na kuendelezea haya yaliyoanzwa na akin Lema.
   
 15. F

  Froida JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  You are so right needs more support support
   
 16. S

  Straight JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu chadema hata 2simamishe jiwe Arusha magamba hawawez shinda... Ndo iwe Dr Slaa
   
 17. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kabla ya uchaguzi wa mwisho wa mwaka jana,wateule wachache walibatizwa jina la vigogo wa nchi hii walijitwalia ardhi tena kwa kuwachangisha waheshimiwa wavuja jasho wa nchi hii ili waweze kupimiwa maeneo ya ardhi.ushindi katika jimbo la Arusha ni ushindi kwa wanyonge walio wengi toka kwenye mikono dhalimu ya mafisadi.

  Waliahirisha kuvigawa viwanja hivyo wakiamini vitakuwa sumu kwenye uchaguzi,lakini wananchi walijua nini ni batili na kuwanyima kura mafisadi waliotaka kujimilikisha ardhi waliyopewa wananchi wa Arusha na mwenyezi Mungu.

  Chuki imeendelea kutawala miongoni mwa wana magamba.Hakika maslahi kwa wateule wachache yamepingwa kwa nguvu kubwa na wana wa Arusha hali wakijua haki ya mtu haidhulumiwi,bali huchelewa tu,na haki siku zote haiombwi hunyakuliwa kama kifaranga cha kuku kinaponyakuliwa na mwewe.
   
 18. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  CCM ni ufalme uliofitinika wenyewe, msingi wake umejaa nyufa na wajenzi wake wanagawana nondo. Huwa napata taabu sana kuona watu wanai-support. Nawaambia wazi, CCM haiwezi kushinda uchaguzi bila kuhonga na kulindwa na dola.

  CCM wafanye wafanyavyo, uchaguzi wa Ubunge urudiwe, hawatashinda Arusha! Kama walihonga pilau na fedha Igunga, wakapiga risasi na kuwatisha watu na hata kuua Igunga na wakaponyoka kwa taabu, hapa Arusha hata walete vifari vipite barabarani hawatashinda KAMWE!
   
 19. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  I'm like this post! Hata sisiem wakimleta Pinda awe mpinzani hapa A town na CDM wakaweka ile Aravat ya Crashwise nawaambia CDM wanashinda kama wanamsukuma mlevi wa chang'aa vile!
   
 20. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi nilidhani Arusha ipo chini ya CCM, kuchukua jimbo ni kuchukua halmashauri siyo kuchukua kiti cha bunge..... CCM au CDM wakitaka wanaweza kuwa na mbunge wa kuteuliwa ambaye ni mwana Arusha na akawa as effective as the elected MP.
   
Loading...