Tatizo lipi unatamani litatuliwe katika tasnia ya IT Tanzania?

Mambo vipi wanajamvi?

Tasinia ya IT (Information Technology) au TEHAMA kama alivyonikaririsha mwalimu wangu Mzee Malima wakati ananicholea CPU kwenye ubao.

Niliipenda hivyo hivyo japo nilifundishwa kibishi kwa kuwa niliamini nikifika chuo nitafundishwa kila kitu kwa ufasaha.

Kama ilivyo elimu ya Tanzania, mwalimu wako wa shule ya msingi atakwambia "Utaelewa zaidi ukifika secondary' wa secondary atakwambia " utaelewa zaidi ukifika A level"

Yaani kama kuku na vifaranga vyake "Mtanyonya kesho, mtanyonya kesho"

Ukifika A level unajikuta mda mwingi utatumia kujifunza mwenyewe au kufundishwa na wana walio cover mapema. Impact ya mwalimu ni 20%.

Unatoka hapo na concept zako chache za Electronics kisha unafika chuo kwa furaha ukiamini sawa maswali yako yote kuhusu IT yanaenda kujibiwa.

Personally swali langu kubwa lilikua ni hili?

Computer inafanyaje kazi?

Umeme unaopita kwenye wires na switches unazalisha vipi picha na video ninayoona kwenye screen yangu?

Ina play vipi mziki?

Inahifadhi vipi kumbukumbu?

Website na App zinahifadhi vipi data za watumiaji wake

YouTube inajuaje video unazozipenda

Google inafanya kazi vipi?

Ila nilichokiona chuo at least kwa course niliyochukua (Computer Science) ni masikitiko

Na ni chuo kizuri, japo siku hizi nasikia kimepata jina jipya la jalalani

Sipendi, sipendi mtanie chuo changu

Japo ufundishaji wake nahisi unaendana kabisa na hilo jina at least kwa course niliyosoma.

Hapa ndipo nilipokuja kugundua kwanini ma IT Watanzania sio competitive.

Hawa solve matatizo yoyote ya maana kwenye jamii. Wavivu wa kujifunza top-notch technologies

Jibu ni kwamba wengi wao hawana Msingi mzuri wa IT au Computer Science

Sitosahau nilivyofundishwa database kwa kuchorewa table moja tu ubaoni. Sikuelewa hata kilichokua kinafundishwa pale.

Hakuna mstari wowote wa codes ulioandikwa. Hata illustration ndogo ya vipi database ina communicates na application na kuleta taarifa zote kwa mtumiaji. But Mungu hamtupi mja wake.

Kwa kuwa nilikua na kitu ya kujifunza nikapata walimu wapya. Community ya Computer Science ilinipokea nikapata walimu wapya

YouTubers, strangers wa stack over flow, Documentations za open source software na libraries.

Tech Talks, na most of all CS50 channel ya YouTube

Ukichanganya na kidogo nilichokua nacho, now I know a lot katika career yangu japo still najifunza kitu kipya kila siku

Hitimisho langu ni kwamba vyuo vya Tanzania, havifundishi IT.

Vinatoa tu degree zisizo na maana yoyote

Tutorials chache za YouTube ni worth than 1.5M unaliyolipa kwa mwaka Chuoni

WIZI MTUPU

Lengo la uzi huu ni kupeana ushauri nini kifanyike kuikoa sekta hii

Na tatizo lipi ungependa ma IT wa Tanzania walitatue

Note: sijasema IT wote sio competitive

Wapo wachache the best of the best
Mkuu,Umeongea kwa uchungu mpaka unatia huruma
 
ila instagram ni python na django ambayo imeandikwa entirely na python, au nasema uongo ndugu yangu...
Yah....Backend yake ni Python
Ila Mobile Framework iliyotumiwa ni React Native

Pia sio lazima utumie Python na Django Ku design App kama Instagram

Unaweza tumia Server side language yoyote ile kwa kazi hio + React Native

Kwa JavaScript developer anaweza leverage power ya Nodejs na kutumia JavaScript kama server side language pia

So anakua na uwezo wa kufanya vingi kwa language moja tu
 
Best idea kaka...
Airbnb like App
Yah hii idea natamani sana kufanyia kazi ila mtaji sina. Ila ni idea ambayo ukiifanyia kazi vizuri ukaweka na revenue models ndani ukaipromote kwa kasi basi unamenya life within no time. Ukipata na wadhamini wakubwa tu umetoka kimaisha kibongo bongo!

Unakula just 3% tu kwenye kila muamala. Ukiwaingiza watu wenye maghorofa ya mjini yale kwenye mfumo we ni kumenya tu!

Target ni East Africa tu, wakiikubali kama M-Pesa we ni mtu mwengine.
 
Mzizi wa fitina upo kwenye Payment System....App part sio shida
Hakuna Payment Mature itakayo weza ku integrate na Service

Na ku design yako from the scratch ni cost
Labda uwatumie hao Mobile Operators
 
Swali zuri,

Kama ndio kwanza unaanza na area ya programming uliyoipenda ni Mobile Apps Programming kulingana na swali lako

Nakushauri uanze na JavaScript
(Au kama una passion zaidi tujifunze Typescript)
Japo ni rahisi Ku shift from JavaScript to Typescript baadae

Faida ya kujifunza JavaScript ni kwamba utaitumie pande zote mbili
Frontend na Backed

Kama haupo familiar
Frontend ndio huo muonekano wa App yako,hicho mtumiaji anachokiona na kukishika....User Interface

Then Backend ni nyuma ya pazia ya app yako
Logics ya app ndipo ilipo...

Advantage nyingine ya JavaScript ni kwamba Cross platform Mobile App Framework ambayo ni popular kwa sawa inatumia JavaScript au Typescript kama lugha mama

Na App kama Facebook , Skype na Instagram zimetengenezwa entirely na hio Framework

Inaitwa React Native nitakuwekea links zake kama utahitaji

Baada ya kujifunza JavaScript, jifunze
Nodejs na React Native

Hio ndio njia ya kuwa Mobile App developers bora kwa sasa

Usisahau pia Basics za Web
Kama HTML na CSS

Haswa CSS
Hii inatumika Ku style web page lakini kwa kutumia React Native kuna similar concept ya kustyle app yako katika mtindo aina ya CSS
Karibu sana
 
Mzizi wa fitina upo kwenye Payment System....App part sio shida
Hakuna Payment Mature itakayo weza ku integrate na Service

Na ku design yako from the scratch ni cost
Labda uwatumie hao Mobile Operators
Hapo ndipo inabidi kukaa na wadau wa M-PESA wakikubali una embed code tu ndani inakuwa mtu anaweza lipia tu direct kupitia system. Later unaomba na mabenki wakikubali nao freshi tu as long as its a profitable business!
 
Swali zuri,

Kama ndio kwanza unaanza na area ya programming uliyoipenda ni Mobile Apps Programming kulingana na swali lako

Nakushauri uanze na JavaScript
(Au kama una passion zaidi tujifunze Typescript)
Japo ni rahisi Ku shift from JavaScript to Typescript baadae

Faida ya kujifunza JavaScript ni kwamba utaitumie pande zote mbili
Frontend na Backed

Kama haupo familiar
Frontend ndio huo muonekano wa App yako,hicho mtumiaji anachokiona na kukishika....User Interface

Then Backend ni nyuma ya pazia ya app yako
Logics ya app ndipo ilipo...

Advantage nyingine ya JavaScript ni kwamba Cross platform Mobile App Framework ambayo ni popular kwa sawa inatumia JavaScript au Typescript kama lugha mama

Na App kama Facebook , Skype na Instagram zimetengenezwa entirely na hio Framework

Inaitwa React Native nitakuwekea links zake kama utahitaji

Baada ya kujifunza JavaScript, jifunze
Nodejs na React Native

Hio ndio njia ya kuwa Mobile App developers bora kwa sasa

Usisahau pia Basics za Web
Kama HTML na CSS

Haswa CSS
Hii inatumika Ku style web page lakini kwa kutumia React Native kuna similar concept ya kustyle app yako katika mtindo aina ya CSS
Asante sana ndugu....
Huu muongozo naanza kuutumia.

"Na App kama Facebook , Skype na Instagram zimetengenezwa entirely na hio Framework

Inaitwa React Native nitakuwekea links zake kama utahitaji"
Naomba hizo links...
 
TCRA iwe inasajili vifaa(smartphones) ili hata ukiibiwa iwe rahisi kublock na kuitrack kuliko ilo swala lipelekwe polisi na polisi watake pesa kabla ya kazi
Hii mkuu inafanyika automatically unapowasha simu yako na inakua associated na line uliyotumia. Sema mara nyingi watu huwa hawaripoti/kuchukulia maanani wanapopoteza devices zao na kuripoti tu kuwa wamepoteza line. Siku ngoja upoteze simu alafu usitoe ripoti kisha simu yako ikatumiwa kufanyia uhalifu, ndo utajua TCRA in mkono mrefu.
 
Asante sana ndugu....
Huu muongozo naanza kuutumia.

"Na App kama Facebook , Skype na Instagram zimetengenezwa entirely na hio Framework

Inaitwa React Native nitakuwekea links zake kama utahitaji"
Naomba hizo links...
Take your time Jifunze JAVASCRIPT tu
Top to bottom....

Uwe deep kwenye hio Language

Utanishukuru....

Java haina future achana nayo
 
Hapo ndipo inabidi kukaa na wadau wa M-PESA wakikubali una embed code tu ndani inakuwa mtu anaweza lipia tu direct kupitia system. Later unaomba na mabenki wakikubali nao freshi tu as long as its a profitable business!
Kwa mpesa huna haja hata ya kukaa nao......utawafaidisha

Wame expose api endpoints zao
Pita nazo
Then customers wako watatumia hio Gateway itakayo consume api za Mpesa....

Mpesa wenyewe watakufata muonge in case app ime gain momentum
 
hawatanishtaki mkuu!
 
Mkuu ishu sio IT ishu ni computer science pure ITs knows nothing or little about codding, ok nasoma RUAHA CATHOLIC UNIVERSITY , (second year).
 
Back
Top Bottom