Tatizo lipi unatamani litatuliwe katika tasnia ya IT Tanzania?

Kuchwizzy

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
1,070
2,299
Mambo vipi wanajamvi?

Tasinia ya IT (Information Technology) au TEHAMA kama alivyonikaririsha mwalimu wangu Mzee Malima wakati ananicholea CPU kwenye ubao.

Niliipenda hivyo hivyo japo nilifundishwa kibishi kwa kuwa niliamini nikifika chuo nitafundishwa kila kitu kwa ufasaha.

Kama ilivyo elimu ya Tanzania, mwalimu wako wa shule ya msingi atakwambia "Utaelewa zaidi ukifika secondary' wa secondary atakwambia " utaelewa zaidi ukifika A level"

Yaani kama kuku na vifaranga vyake "Mtanyonya kesho, mtanyonya kesho"

Ukifika A level unajikuta mda mwingi utatumia kujifunza mwenyewe au kufundishwa na wana walio cover mapema. Impact ya mwalimu ni 20%.

Unatoka hapo na concept zako chache za Electronics kisha unafika chuo kwa furaha ukiamini sawa maswali yako yote kuhusu IT yanaenda kujibiwa.

Personally swali langu kubwa lilikua ni hili?

Computer inafanyaje kazi?

Umeme unaopita kwenye wires na switches unazalisha vipi picha na video ninayoona kwenye screen yangu?

Ina play vipi mziki?

Inahifadhi vipi kumbukumbu?

Website na App zinahifadhi vipi data za watumiaji wake

YouTube inajuaje video unazozipenda

Google inafanya kazi vipi?

Ila nilichokiona chuo at least kwa course niliyochukua (Computer Science) ni masikitiko

Na ni chuo kizuri, japo siku hizi nasikia kimepata jina jipya la jalalani

Sipendi, sipendi mtanie chuo changu

Japo ufundishaji wake nahisi unaendana kabisa na hilo jina at least kwa course niliyosoma.

Hapa ndipo nilipokuja kugundua kwanini ma IT Watanzania sio competitive.

Hawa solve matatizo yoyote ya maana kwenye jamii. Wavivu wa kujifunza top-notch technologies

Jibu ni kwamba wengi wao hawana Msingi mzuri wa IT au Computer Science

Sitosahau nilivyofundishwa database kwa kuchorewa table moja tu ubaoni. Sikuelewa hata kilichokua kinafundishwa pale.

Hakuna mstari wowote wa codes ulioandikwa. Hata illustration ndogo ya vipi database ina communicates na application na kuleta taarifa zote kwa mtumiaji. But Mungu hamtupi mja wake.

Kwa kuwa nilikua na kitu ya kujifunza nikapata walimu wapya. Community ya Computer Science ilinipokea nikapata walimu wapya

YouTubers, strangers wa stack over flow, Documentations za open source software na libraries.

Tech Talks, na most of all CS50 channel ya YouTube

Ukichanganya na kidogo nilichokua nacho, now I know a lot katika career yangu japo still najifunza kitu kipya kila siku

Hitimisho langu ni kwamba vyuo vya Tanzania, havifundishi IT.

Vinatoa tu degree zisizo na maana yoyote

Tutorials chache za YouTube ni worth than 1.5M unaliyolipa kwa mwaka Chuoni

WIZI MTUPU

Lengo la uzi huu ni kupeana ushauri nini kifanyike kuikoa sekta hii

Na tatizo lipi ungependa ma IT wa Tanzania walitatue

Note: sijasema IT wote sio competitive

Wapo wachache the best of the best
 
Nipe ushauri.

Ili niweze kutengeza apk kama Whatsapp, facebook, au android app yoyote ile. Nisome code language ipi/zipi.
 
Mifumo ya vyuo vyetu huwa ni kukariri madesa ya mwalimu na kupass. Unaweza kuta mwanafunzi toka anaingia mwaka wa kwanza hadi anamaliza hajawahi kugusa kitabu. Muda wote na notisi za mwalimu na past papers.

Vyuo vya bongo ukisema usome vitabu unafeli vibaya mno. Kwanza mwalimu hatoi mtihani humo anatoa kwenye notsi na past paper. Pili huwezi kimbizana na kasi ya mwalimu ukisoma kitabu. Utajikuta upo nyuma sana.

Kuwe na namna ya kuwafanya wanafunzi wapate maarifa yao kutoka kwenye vitabu na si madesa ya waalimu na past papers. Mi nafikiri hapo tutatoa watu wenye uelewa sana. Watu wanaojua misingi ya vitu wanavyosomea.
 
Tatizo lipi unatamani litatuliwe katika tasnia ya IT Tanzania?

Mashirika yote ya simu yawezeshe kutoa pesa kupitia pc na sio tu simu kama nina access ya pc na simu imebiwa kuwe na portal itakayowezeshajambo hilo.

Kwa maana hiyo kama sina pesa ya kula na nimeibiwa simu wakati nafanya mchakato. Basi jirani anaweza nichapa wifi hotspot kisha natoa pesa kwa wakala kama Kawa.
 
Nipe ushauri.....
Ili niweze kutengeza apk kama Whatsapp, facebook, au android app yoyote ile.... Nisome code language ipi/zipi.
Swali zuri,

Kama ndio kwanza unaanza na area ya programming uliyoipenda ni Mobile Apps Programming kulingana na swali lako

Nakushauri uanze na JavaScript
(Au kama una passion zaidi tujifunze Typescript)
Japo ni rahisi Ku shift from JavaScript to Typescript baadae

Faida ya kujifunza JavaScript ni kwamba utaitumie pande zote mbili
Frontend na Backed

Kama haupo familiar
Frontend ndio huo muonekano wa App yako,hicho mtumiaji anachokiona na kukishika....User Interface

Then Backend ni nyuma ya pazia ya app yako
Logics ya app ndipo ilipo...

Advantage nyingine ya JavaScript ni kwamba Cross platform Mobile App Framework ambayo ni popular kwa sawa inatumia JavaScript au Typescript kama lugha mama

Na App kama Facebook , Skype na Instagram zimetengenezwa entirely na hio Framework

Inaitwa React Native nitakuwekea links zake kama utahitaji

Baada ya kujifunza JavaScript, jifunze
Nodejs na React Native

Hio ndio njia ya kuwa Mobile App developers bora kwa sasa

Usisahau pia Basics za Web
Kama HTML na CSS

Haswa CSS
Hii inatumika Ku style web page lakini kwa kutumia React Native kuna similar concept ya kustyle app yako katika mtindo aina ya CSS
 
Mifumo ya vyuo vyetu huwa ni kukariri madesa ya mwalimu na kupass. Unaweza kuta mwanafunzi toka anaingia mwaka wa kwanza hadi anamaliza hajawahi kugusa kitabu. Muda wote na notisi za mwalimu na past papers...
Wazo zuri mkuu

Kibaya kwenye IT vitu vinabadilika kila siku

Kila siku kuna technology mpya

Sawa unapofundisha watu kupitia notes zako za miaka hio unamjenga vipi mwanafunzi na soko la ajira?

Kwanini usimpe msingi mzuri wa kujifunza hizi technology zinazokuja na kuondoka kwasababu msingi wa Computer Science na IT ni uleule owe Havard au Udsm.
 
Nataka....kuwe na soko la pamoja la Tanzania ambapo mtu anaweza kuagiza mizigo kwa reja reja na jumla kutoka kariakoo.
-Iwepo sehemu ya kulipia kwa njia ya mitandao ya simu, bank, bitcoin.

-Sehemu ya negotiation...
-Suchagua njia ya usafirishaji as ....gari train,ndege,...na vingine
-sehemu ya kutrack mzigo umefikia wapi
-kodi ya mzigo kama ipo
- Sehemu amabayo mnunuzi anaweza kuweka comment.....kwa mfano ninataka rangi gani na ngapi na size...hivo hivo kwa items nyingine

  • Somments na rating kwa muuzaji...ili kucontrol quality
  • Sehemu ya kufungua mashtaka./disputes..ikiwezekana refunds zitolewe kama ulichagiza sicho
  • Kuwe na privacy kiasi kwamba matapeli hayawezi kukwapua hela kwenye account za watu
  • Product imfikie mlengwa mlangoni...hii itasumbua coz hatuna adresses za majumbani, ila nilisikia wanampango wa kutengeneza zip codes itasaidia hapa

Kuna mtu ataniuliza mbona kikuu, alibab, aliexpress wanafanya hivo?

Mimi nataka watanzania wanaofanya manunuzi kupitia simu za mikononi,instagram,watsapp watumie njia rahisi, secure na efficent...maswala ya kuambiana njoo inbox sio poa ,mara unauziwa bei tofauti na wateja wengine ni shida

Wabongo ..tuna matatizo likiki kwenye kuaminiana..nashauri kwenye posts za product uweke nafasi kubwa kuruhusu enough description ya item, ikiwezekana iwekwe video sio lazima picha.

Mawazo yangu ni vague, lakini naamini utachukua kitu.
 
Naamini Tanzania kuna vijana wenye uwezo mzuri sana wa kuiboresha kwa nyanja ya IT lkn mazingira huwa ni magumu kwa nchi yetu mfano.

Hapo nzega kuna issue ya walimu kusign na kuripoti taarifa za ufundishaji kupitia tablet.
Changamoto ya elimu ya kuzitumia
Umeme na mtandao zimekuwa shida.
 
Kuwe na online ballot system watu waweze kupiga kura popote walipo muda wowote within time frame na hizi ballot ziwe na live feeds ya matokeo yanayoendelea watu wawe wanajua right away nan anaongoza na nani haongozi
 
Nataka....kuwe na soko la pamoja la tanzania ambapo mtu anaweza kuagiza mizigo kwa reja reja na jumla kutoka kariakoo....
Wazo zuri sana mkuu....hata Mimi nawaza kama wewe.

Changamoto kubwa ya online business Tanzania.

Sio kuaminiana....hata Ulaya hakuna atakaye kuamini kwenye pesa

Tatizo kubwa ni Payment Gateway itakayofanya kazi yenye Escrow like Architecture.

(Yaani malipo yanafanyika baada ya pande mbili kuridhiana)

Huu mfumo ukiwepo uta revolutionized Online businesses za Tanzania

Huu ndio mzizi wa yote

Hizo Amazon, Aliexpress au Alibaba zilianza hio mifumo ikiwepo so hawakua na haja ya Ku design payment system zao mpaka pale walipokua wakubwa na kuanza kujitegemea
 
Swali zuri,

Kama ndio kwanza unaanza na area ya programming uliyoipenda ni Mobile Apps Programming kulingana na swali lako

Nakushauri uanze na JavaScript
(Au kama una passion zaidi tujifunze Typescript)
Japo ni rahisi Ku shift from JavaScript to Typescript baadae

Faida ya kujifunza JavaScript ni kwamba utaitumie pande zote mbili
Frontend na Backed

Kama haupo familiar
Frontend ndio huo muonekano wa App yako,hicho mtumiaji anachokiona na kukishika....User Interface

Then Backend ni nyuma ya pazia ya app yako
Logics ya app ndipo ilipo...

Advantage nyingine ya JavaScript ni kwamba Cross platform Mobile App Framework ambayo ni popular kwa sawa inatumia JavaScript au Typescript kama lugha mama

Na App kama Facebook , Skype na Instagram zimetengenezwa entirely na hio Framework

Inaitwa React Native nitakuwekea links zake kama utahitaji

Baada ya kujifunza JavaScript, jifunze
Nodejs na React Native

Hio ndio njia ya kuwa Mobile App developers bora kwa sasa

Usisahau pia Basics za Web
Kama HTML na CSS

Haswa CSS
Hii inatumika Ku style web page lakini kwa kutumia React Native kuna similar concept ya kustyle app yako katika mtindo aina ya CSS

ila instagram ni python na django ambayo imeandikwa entirely na python, au nasema uongo ndugu yangu...
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom