DOKEZO Serikali iweke usawa pale inapotoa fursa yoyote kwenye ngazi ya Elimu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kwako Serikali yangu pendwa.

Niliamua kukaa kimya ila baada ya kuona mambo yameanza kuniendea vibaya kabla sijaanza chuo imenibidi niikumbushe serikali yangu pendwa.

Kitendo cha Serikali Kuondoa Ada kwa Vyuo vya Sayansi na Teknolojia ambavyo ni DIT, MUST na ATC alafu Vyuo vingine vyenye kufundisha Kozi za Sayansi na Teknolojia ila kwa uchache hii sio sawa kabisa.

Kwanza ingekuwa vizuri wakaweka wazi ni nini hasa wamezingatia mpaka wanafunzi wa hapo wasilipe na wakati kuna vyuo vingine vya Serikali Mfano MNMA na baadhi wanafundisha baadhi ya Kozi za Sayansi na Teknolojia. Ikiwa kama Mwanafunzi anasoma Kozi ya IT na ICT huko MUST, ATC na DIT alafu halipi Ada, sasa kwa nini hawa waliopangiwa Vyuo tofauti na hivyo mlivyo visamehe Ada kwamba walipe Ada wakati wote tunasoma IT, ICT & Computer Science.

Hii sio haki kabisa na ni vizuri mkashauriana upya kama nia yenu ni Kuwasamehe wanaosoma IT, ICT & Computer Science basi ni vizuri mkafanya kwa Wanafunzi wote wanaosoma hizo kozi kwa Vyuo vyote vya kati vya serikali. Na kama haiwezekani kwa nini msitupangie hivyo vyuo?

Mfano mimi nilijaza chuo kimoja wapo kati ya hivyo ila mkanipeleka mnapotaka nyie ila Kozi ni ileile, hamjiulizi kwa nini kachagua sehemu fulani, hamjiulizi naishije huku nyumbani au nakulaje 😓 Au hivyo vyuo ni vya watoto wavigogo ?

Nasemaje nasemaje hii sio sawa kabisa na ni vizuri mkaweka usawa kila sehemu mana mnatukatisha tamaa sie wengine nakujiona hatuna umuhimu zaidi ya watoto wa vigogo huko MUST, DIT na ATC.

Ahsanteni.
 
Pole janja langu, Huo mfumo umeanza lini na unawalenga haswa watu gan? Wale wa Tamisemi au Wote waliochaguliwa katika vyuo husika?
 
Back
Top Bottom