Tatizo la Ng'ombe ni kumpuuza Kupe maishani

Tatizo la Ng'ombe ni kumpuuza Kupe maishani

Kupe hana jeuri wala uwezo wa kusababisha homa na kukondeana kote kunakomtesa ng'ombe,ng'ombe ni mkubwa kwa umbo na anaweza kumkandamiza kwenye mti au ukuta kupe akafa, tatizo ni kufikiri hana madhara makubwa maishani mwake na kumbe homa zote na vifo vingi ni vya kupe.

Kwa upande mwingine watanzania wanachukulia kirahisi rahisi mambo kama RICHMOND, IPTL, EPA, MEREMETA, nk makupe yanayofadhiliwa na CCM hawayatazami kwa jicho stahiki, wanacheka nayo huku wanayaita ndugu, rafiki, kada, mwenzetu nk.

Tunapumbazwa na ugali wa muhogo yunaoupata kila jioni kabla ya kulala bila kuitazama elimu yetu, afya ya Jamii,miundo mbinu ya barabara, utawala bora nk.

Dharau yetu hii kwa kupe imeleta homa kali na kukongoloka kwa maendeleo ya watanzania, siku ng'ombe akichachamaa kwa wiki moja tu asimpe kupe damu ndo kiama cha makupe kitakapo wadia.

INYIMENI KURA CCM SERIKALI ZA MITAA NA SERIKALI KUU MUONE KAMA HAIJAFA NDANI YA MWAKA MMOJA.

Hakutakuwa na kasuku Nape Nauye,Kupe Kinana,nk na nchi itarejesha afya yake tena.

Datz why huwa nakuita "My 3rd Role Modal" baada ya Mhe.Mbowe na Lema wa Arusha Mkuu Alphonce Mawazo
 
Last edited by a moderator:
Hao akina Mbowe si ndo makupe hatari wenye njaa ya kuua ng'ombe ndani ya wiki tu?
 
Watanzania tunatakiwa kuwa aggressive kudai haki zetu maana wakati mwingine tunatambua kwamba mambo hayaendi lakini hakuna wa kuchukua hatua. Naamini kila moja ana nafasi ya kufanya mabadiliko kuanzia kwenye familia zetu tusikubali kulea uovu kisa tu aah hainihusu sana hii au wengine watalifanyia kazi. Ni mambo mengi yako ovyo kwa kuwa hata wasomi tumekubali status quo. Rasilimali ziko nyingi but inatumika vibaya.

Let us be part of the change we want to enjoy. Play your role it can be done

kweli mkuu, kila mtu ananafasi yake kuansia kwenye familia kama kuingia barabarani kuingia imetushinda hata kuweka vema tofauti na ccm nayo litushinde, mimi ndugu zangu usukumani nikigundua wewe ni ccm na nikakukalisha ukangangania ccm basi tusifahamiane....haiwezekani unyanyasike kiasi hicho mfano unalima pamba halafu ccm wanakuja kukupangia bei mbaya zaidi unaweza kuta mwaka jana ilikuwa 1500 mwaka huu wakaamua iwe 700 bila kujali gharama ulizotumia mbaya zaidi huwa wanalazimishwa kulima na vitisho chungumzima...
angalia walicho fanyiwa kwenye operesheni tokomeza watu wameuwawa wakatu majabgili ni akina kina wanawake wamebakwa na mbaya zaidi wakisha bakwa wanasokomezwa chupa sehemu za siri halafu -------- anaiunga mkono ccm...
 
Hao akina Mbowe si ndo makupe hatari wenye njaa ya kuua ng'ombe ndani ya wiki tu?

tatizo watu tunakuwa na nahaba ya kijinga leo tunaipigia chapuo chadema ni kwasababu angalau ina simamia inacho kisema lakini na wao wakiingia wakabadilika tunatupa kule, nchi hii hakuna mwenye haki miliki na wananchi wanapaswa kulitambua hilo wajue haki zao, angalia USA hawaangalii uso ukiwaambia nitawafanyia hiki ndani ya miaka 4 ikiisha hujafanya wanakusubili utakuja kuwaambia ulisema utafanya 1,2,3,4,5 mangapi umefanya na kwa ubora gani na mangapi umeshindwa na kwanini wanaamua hawakupi miaka 50 ya blah blah ahadi 98 utekelezaji 30% na bado kikwete anaendelea kutoa ahadi huku akiwa amebakiza mwaka mmoja magogoni...
 
kweli mkuu, kila mtu ananafasi yake kuansia kwenye familia kama kuingia barabarani kuingia imetushinda hata kuweka vema tofauti na ccm nayo litushinde, mimi ndugu zangu usukumani nikigundua wewe ni ccm na nikakukalisha ukangangania ccm basi tusifahamiane....haiwezekani unyanyasike kiasi hicho mfano unalima pamba halafu ccm wanakuja kukupangia bei mbaya zaidi unaweza kuta mwaka jana ilikuwa 1500 mwaka huu wakaamua iwe 700 bila kujali gharama ulizotumia mbaya zaidi huwa wanalazimishwa kulima na vitisho chungumzima...
angalia walicho fanyiwa kwenye operesheni tokomeza watu wameuwawa wakatu majabgili ni akina kina wanawake wamebakwa na mbaya zaidi wakisha bakwa wanasokomezwa chupa sehemu za siri halafu -------- anaiunga mkono ccm...
Umesomeka sana
 
Leo tunajadli mambo haya makubwa wengine wanaleta ushabiki,iko siku inakuja tutakutana ama misituni tukikimbia machafuko au kwenye makambi ya wakimbizi ndo tutajuta
 
Back
Top Bottom