Tatizo la Ng'ombe ni kumpuuza Kupe maishani

Tatizo la Ng'ombe ni kumpuuza Kupe maishani

Joined
Sep 10, 2013
Posts
335
Reaction score
478
Kupe hana jeuri wala uwezo wa kusababisha homa na kukondeana kote kunakomtesa ng'ombe,ng'ombe ni mkubwa kwa umbo na anaweza kumkandamiza kwenye mti au ukuta kupe akafa, tatizo ni kufikiri hana madhara makubwa maishani mwake na kumbe homa zote na vifo vingi ni vya kupe.

Kwa upande mwingine watanzania wanachukulia kirahisi rahisi mambo kama RICHMOND, IPTL, EPA, MEREMETA, nk makupe yanayofadhiliwa na CCM hawayatazami kwa jicho stahiki, wanacheka nayo huku wanayaita ndugu, rafiki, kada, mwenzetu nk.

Tunapumbazwa na ugali wa muhogo yunaoupata kila jioni kabla ya kulala bila kuitazama elimu yetu, afya ya Jamii,miundo mbinu ya barabara, utawala bora nk.

Dharau yetu hii kwa kupe imeleta homa kali na kukongoloka kwa maendeleo ya watanzania, siku ng'ombe akichachamaa kwa wiki moja tu asimpe kupe damu ndo kiama cha makupe kitakapo wadia.

INYIMENI KURA CCM SERIKALI ZA MITAA NA SERIKALI KUU MUONE KAMA HAIJAFA NDANI YA MWAKA MMOJA.

Hakutakuwa na kasuku Nape Nauye,Kupe Kinana,nk na nchi itarejesha afya yake tena.
 
Hakika umenena mkuu suala la elimu kwa mpiga kura ndio kila kitu nilazima tuwakumbushe wapiga kura maumivu ya kuhongwa kanga, kofia na ubwabwa kwa siku moja then maumivu tunayapata kwa zaidi ya miaka mitano

Tukifanikiwa kuwaelewesha hilo twende tudai mabadiriko ktk tume ya uchaguzi, kudai usawa kati ya mpiga kura na mpigiwa kura, serikali kuboresha miundombinu na vitendea kazi ktk chaguzi mbalimbali. Tukifanikuwa hayo hata tusipopiga kampeni yoyote bado ccm itatoka madarakani.

Kila lakheri mlioko ktk nafasi za uwajibikaji kwaajili ta demokrasia.

BACK TANGANYIKA
 
Hakika umenena mkuu suala la elimu kwa mpiga kura ndio kila kitu nilazima tuwakumbushe wapiga kura maumivu ya kuhongwa kanga,kofia na ubwabwa kwa siku .moja then maumivu tunayapata kwa zaidi ya miaka mitano

Tukifanikiwa kuwaelewesha hilo twende tudai mabadiriko ktk tume ya uchaguzi, kudai usawa kati ya mpiga kura na mpigiwa kura, serikali kuboresha miundombinu na vitendea kazi ktk chaguzi mbalimbali. Tukifanikuwa hayo hata tusipopiga kampeni yoyote bado ccm itatoka madarakani.

Kila lakheri mlioko ktk nafasi za uwajibikaji kwaajili ta demokrasia.

BACK TANGANYIKA
Kila mtanganyika aamuke sasa, tupige kelele za uamusho mijini na vijijini ili watu wetu waamuke
 
Tatizo ni wanasiasa nyie, almost wote mnasema yaleyale na wote mkipata nafasi mnageuka makupe tuu. Sioni nani wa kumwamini na wala siabudu siasa. Makupe yamejaa ccm, cdm, nccr, tlp n.k so hatuchagui chama tunachagua mtu. Ni mtazamo tuu!!
 
Hii nimeipenda mno, kweli huu uhusiano wa ngombe na kupe ndio tuliokuwa nao wa-tz na viongozi wa sasa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tatizo ni wanasiasa nyie, almost wote mnasema yaleyale na wote mkipata nafasi mnageuka makupe tuu. Sioni nani wa kumwamini na wala siabudu siasa. Makupe yamejaa ccm, cdm, nccr, tlp n.k so hatuchagui chama tunachagua mtu. Ni mtazamo tuu!!

Naheshimu msimamo na mtazamo wako ndugu
 
Tatizo ni wanasiasa nyie, almost wote mnasema yaleyale na wote mkipata nafasi mnageuka makupe tuu. Sioni nani wa kumwamini na wala siabudu siasa. Makupe yamejaa ccm, cdm, nccr, tlp n.k so hatuchagui chama tunachagua mtu. Ni mtazamo tuu!!

kuwafananisha vyama vingine na madhila ya ccm ni ukandamizaji na uvivu .
 
Tatizo ni wanasiasa nyie, almost wote mnasema yaleyale na wote mkipata nafasi mnageuka makupe tuu. Sioni nani wa kumwamini na wala siabudu siasa. Makupe yamejaa ccm, cdm, nccr, tlp n.k so hatuchagui chama tunachagua mtu. Ni mtazamo tuu!!

Kwanini mchague watu walewale wenye sifa zilezile wakufanya yale yale, wakati tofauti?

Shida yetu kubwa watanzania ni MFUMO, hata tukichagua watu wazuri kiasi gani bado hawawezi kuleta mabadiriko yenye tija kwa Taifa letu. Leo hii huwezi kununua Suruali mpya huku ndani umevaa pichu ya zamani tena ikiwa chafu ikitoa harufu mbaya Halafu ukadai eti umekuwa mpya kwasababu ya suruali uliyo vaa...Hapana hatuendi hivyo.....

Safisha ndani ya kikombe ili na nje yake ipate kuwa safi.....Nikwakufanya hivyo ndipo utatembea kifua mbele huku ukijidai kwamba umekuwa mpya kwasababu ya kuvaa Pichu mpya na suruali mpya. Tuondoe mfumo huu kandamizi ulioshindwa tangu uhuru wa taifa letu ndipo tutakapo baini uzuri wa mabadiriko.

BACK TANGANYIKA
 
Kupe hana jeuri wala uwezo wa kusababisha homa na kukondeana kote kunakomtesa ng'ombe,ng'ombe ni mkubwa kwa umbo na anaweza kumkandamiza kwenye mti au ukuta kupe akafa,tatizo ni kufikiri hana madhara makubwa maishani mwake na kumbe homa zote na vifo vingi ni vya kupe.

Kwa upande mwingine watanzania wanachukulia kirahisi rahisi mambo kama RICHMOND,IPTL,EPA,MEREMETA,nk makupe yanayofadhiliwa na ccm hawayatazami kwa jicho stahiki,wanacheka nayo huku wanayaita ndugu,rafiki,kada,mwenzetu nk.

Tunapumbazwa na ugali wa muhogo yunaoupata kila jioni kabla ya kulala bila kuitazama elimu yetu, afya ya Jamii,miundo mbinu ya barabara, utawala bora nk.

Dharau yetu hii kwa kupe imeleta homa kali na kukongoloka kwa maendeleo ya watanzania, siku ng'ombe akichachamaa kwa wiki moja tu asimpe kupe damu ndo kiama cha makupe kitakapo wadia.

INYIMENI KURA CCM SERIKALI ZA MITAA NA SERIKALI KUU MUONE KAMA HAIJAFA NDANI YA MWAKA MMOJA.

Hakutakuwa na kasuku Nape Nauye,Kupe Kinana,nk na nchi itarejesha afya yake tena.

lugha ya picha uliyotumia haiendani na muktadha wa ujumbe unaotaka kuufikisha.

mara kupe hasababishi homa, mara kupe anasababisha homa sasa ndo nini

kwa hisani ya Honolulu chukua hii

CCM ni kama kupe
NG'OMBE anapelekwa machinjioni, kupe hana habari
NG'ombe anachinjwa, kupe hana habari

NG'OMBE anachunwa, kupe hana habari
NGOZI inawambwa, kupe hana habari
NGOZI ikianza kukauka he! ndo kupe anashtuka

CCM INAKUFA NA WANA CCM HAWANA HABARI,
 
[FONT=times new
roman]Kupe hana jeuri wala uwezo wa kusababisha homa na
kukondeana kote kunakomtesa ng'ombe,ng'ombe ni mkubwa kwa umbo na
anaweza kumkandamiza kwenye mti au ukuta kupe akafa, tatizo ni kufikiri
hana madhara makubwa maishani mwake na kumbe homa zote na vifo vingi ni
vya kupe.

Kwa upande mwingine watanzania wanachukulia kirahisi rahisi mambo kama
RICHMOND, IPTL, EPA, MEREMETA, nk makupe yanayofadhiliwa na CCM
hawayatazami kwa jicho stahiki, wanacheka nayo huku wanayaita ndugu,
rafiki, kada, mwenzetu nk.

Tunapumbazwa na ugali wa muhogo yunaoupata kila jioni kabla ya kulala
bila kuitazama elimu yetu, afya ya Jamii,miundo mbinu ya barabara,
utawala bora nk.

Dharau yetu hii kwa kupe imeleta homa kali na kukongoloka kwa
maendeleo ya watanzania, siku ng'ombe akichachamaa kwa wiki moja tu
asimpe kupe damu ndo kiama cha makupe kitakapo wadia.

INYIMENI KURA CCM SERIKALI ZA MITAA NA SERIKALI KUU MUONE KAMA HAIJAFA
NDANI YA MWAKA MMOJA.

Hakutakuwa na kasuku Nape Nauye,Kupe Kinana,nk na nchi itarejesha afya
yake tena.
[/FONT]

Dah!! Nimekuelewa kaka
 
lugha ya picha uliyotumia haiendani na muktadha wa ujumbe unaotaka kuufikisha.

mara kupe hasababishi homa, mara kupe anasababisha homa sasa ndo nini

kwa hisani ya Honolulu chukua hii

CCM ni kama kupe
NG'OMBE anapelekwa machinjioni, kupe hana habari
NG'ombe anachinjwa, kupe hana habari

NG'OMBE anachunwa, kupe hana habari
NGOZI inawambwa, kupe hana habari
NGOZI ikianza kukauka he! ndo kupe anashtuka

CCM INAKUFA NA WANA CCM HAWANA HABARI,
Nashukuru comrade lakini ungesoma context nzima badala ya msitari mmoja mmoja...nimesema kupe hana uwezo wa kumdhuru ng'ombe kama ng'ombe asingemdharau kupe....wazo zima ni namna kitu kinyonge kinavyoweza kudhuru chenye nguvu kisichojitambua
 
Mchana umeendelea sana kwa CCM, lakini usiku nao umekaribia, hiki chama kitakufa tu watake wasitake, viashilia/indicators are obvious. Kuna kosa kubwa wameshalifanya kwenye swala la Katiba mpya, wanatamani siku zirudi nyuma wasahihishe lakini haiwezekani. Hata hivyo sisi watanzania tumezidi kuendekeza upole/submissiveness, we are walking the ball to the goal instead of running, mbinu zaidi zinatakiwa kulitoa hili dudu CCM
 
hivi ubunge ni jimbo gani tena????
 
hii naweza nikaita thread ya mwaka,
pamoja sana kamanda Alphonce Mawazo , kamanda SONGOKA pia una wazo zuri japo mantiki ya kamanda mawazo iko tofauti kidogo na yako, ya kwako ni njia tu mojawapo yakutokomeza kupe japo wakati kupe anaangamizwa kwa njia uliyosema ni kupe huyo huyo anaitesa ng'ombe kama hoja ya kamanda mawazo inavyojieleza.
 
Last edited by a moderator:
Mchana umeendelea sana kwa CCM, lakini usiku nao umekaribia, hiki chama kitakufa tu watake wasitake, viashilia/indicators are obvious. Kuna kosa kubwa wameshalifanya kwenye swala la Katiba mpya, wanatamani siku zirudi nyuma wasahihishe lakini haiwezekani. Hata hivyo sisi watanzania tumezidi kuendekeza upole/submissiveness, we are walking the ball to the goal instead of running, mbinu zaidi zinatakiwa kulitoa hili dudu CCM
" We are walking the ball to the goal"kweli hatuwezi kufunga kamwe...
 
  • Thanks
Reactions: MC
The giants are deeply in sleep...let the vultures fatten.Kuwasaidia hawa ng'ombe wa bongo ni kazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom