Tatizo la maji Hai Mjini

ldd

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
790
128
Aslalekum,

Naleta mada hii ya shida ya maji hapa Bomang'ombe na viunga vyake. Anayesimamia huu mradi (Engineer Shoo) ndio tatizo sijui kwanini hajiongezi.

Kwa mkoa wa Kilimanjaro kukosa maji miezi mitatu au miwili mfulilizo hii ni kudhibitisha kwamba huyu ndugu yetu Shoo huu mradi umemshinda na nivema Trustees or Serekali mkatafuta namna yakuuendesha huu mradi, huyu Bwana sidhani kama hata anaelewa wilaya ya siha (Kwa wasomali) hakuna shida ya maji ambayo katutengenezea watu wa Boma.

Huyu ni jipu tumbueni mapema au huu mradi uchukuliwe na Muwasa!

Thanks
Mkerekaji
 
Mkuu wa wilaha ya Hai jinsi alivyo mpenda sifa hajasikia hiyo Kero? Aite vyombo vya habari aanze kuwafokea ma engineer wa maji na kuwaambia polisi wawakamate wakalale ndani.
 
Mkuu wa Wilaya ya Hai na Mbunge wa Wilaya ya Hai waliahidi kutatua tatizo la maji miezi tu ya kwanza mbunge atakapokuwa amechaguliwa, sasa hivi maji yamekuwa kero sana Bomang'ombe, mliangalie hili suala ni tatizo kubwa sana.
 
Yaani hapo subirini hotuba nzuri ya mabilioni yaliyotengwa kutatua kero hiyo. Tena ataletwa na waziri wa maji, asutwe mpaka alie halafu aombe msamaha kwa wananchi.

Mtapiga makofi, mtasifu, mtaabudu na kusujudu, serikali imefulia kwa sasa Ni kuwapigeni tu saundi
 
Kitendo cha kuiba kura, jiwe aombe radhi tu, kimejidhiirsha sana, kinakosesha raha, ujasili, heshima, utu, kinadharulisha sana, kwa sasa hata mtendaji akiiba unamwangalia anayekemea uovu huo, unaona wote sawa tu, hamna mwenye haki ya kukemea wezi kwa kuwa wote wezi na wapo hapo kwa njia ya wizi, ni dharau sana, hata ukali wake sasa hivi unadharaulika!
 
Mkuu wa Wilaya ya Hai na Mbunge wa Wilaya ya Hai waliahidi kutatua tatizo la maji miezi tu ya kwanza mbunge atakapokuwa amechaguliwa, sasa hivi maji yamekuwa kero sana Bomang'ombe, mliangalie hili swala ni tatizo kubwa sana.
Na bado shame on those CCM
 
Back
Top Bottom