Hamjambo wana JF
Ningependa kupata ushahuri toka kwenu. Kwa almost mwezi mmoja sasa mwenzenu sipati usingizi. Ulianza kupotea mwezi wa tatu kati kati nilipoanza competition fulani kubwa tu. Nilifikiri ni uoga wa competition na nikapuuza. wakati huo nilikua nalala kwa saa 1 ao 2, alafu usingizi unakata, naupata tena asubuhi mapema. :frown:
Baada ya wiki 2 matokeo yakatangazwa na nikadhani nitapata usingizi ila ndio ikawa mbaya zaidi. Sasa silali kabisa, mchana nashindwa ku-concentrate kwa kazi yangu, nakua na hasira. Usiku nikilala ni dakika chachetu alafu najigeuza usiku kucha. Sasa hivi nimefikia hatua mbaya: sitaki kuona mtu, usiku ukija nakua na hasira na nadhani imeanza ku-affect personal relation yangu. :angry:
Kama kuna mtu ana idea yoyote naomba msaada coz kinacho fata hapa ni kuomba leave nika jifungie chumbani hadi usingizi utakapo patikana. Asanteni kwa msaada.