Tatizo la kuanguka ghafla

Twin_Kids

JF-Expert Member
Feb 25, 2016
3,065
4,621
Ni tumaini langu wote mu wazima wa afya.
Kama mada ilivyo hapo juu,leo nimekuja kuomba msaada.
Nina ndugu,mwana mama mtu mzima. Kwa mda wa miaka 10 sasa,ana tatizo la kuanguka. Kwa siku inaweza tokea zaidi ya mara tatu. Na si kwamba ni kila siku,inaweza ikapita hata wiki au wiki mbili. Na si kifafa. Akianguka inakuwa kama vile kapatwa na kizuguzungu,lakini akirudi katika hali yake,anakuwa hakumbuki kama hali hiyo imemtokea.

Kwa yeyote anayejua mtu wa kusaidia,tafadhali naomba tuwasiliane inbox. Kila tulipojaribu wanadai watatibu,wanaishia tu kula pesa basi.
 
Sidehams chorea hiyo. Aende hospital akatibiwe. Ingawa wanaweza wakasema hana shida. But this is a very common complications ya Rheumatic fever.

Sent from my Infinix X672 using JamiiForums mobile app
 
Ni tumaini langu wote mu wazima wa afya.
Kama mada ilivyo hapo juu,leo nimekuja kuomba msaada.
Nina ndugu,mwana mama mtu mzima. Kwa mda wa miaka 10 sasa,ana tatizo la kuanguka. Kwa siku inaweza tokea zaidi ya mara tatu. Na si kwamba ni kila siku,inaweza ikapita hata wiki au wiki mbili. Na si kifafa. Akianguka inakuwa kama vile kapatwa na kizuguzungu,lakini akirudi katika hali yake,anakuwa hakumbuki kama hali hiyo imemtokea.

Kwa yeyote anayejua mtu wa kusaidia,tafadhali naomba tuwasiliane inbox. Kila tulipojaribu wanadai watatibu,wanaishia tu kula pesa basi.

KUPOTEZA FAHAMU

Kupoteza fahamu ni kitendo kinachotokea kutokana na sababu mbalimbali kwenye mwili. Mara nyingi sababu hizi hupelekea ubongo kutokupata oksijeni na chakula cha kutosha.

Ili kufikia mwelekeo au hitimisho la sababu halisi inayosababisha mtu kupoteza fahamu ni muhimu sana mhusika kusikilizwa kwa makini sana kwani maelezo huchangia kutambua ni kiungo au mfumo gani wa mwili wenye kasoro.

1: Kupata historia kamili ya maisha ya mgonjwa

2: Mazingira ambayo hupelekea mtu kupoteza fahamu.

3: Hali ambayo mhusika hujiaikia kabla ya kupoteza fahamu.

4: Hali ambayo mhusika huwa nayo wakati wa kupoteza fahamu

5: Muda ambao mhuaika huchukua mpaka fahamu kurejea.

6: Hali ambayo mgonjwa huwa nayo baada ya kurejea kwenye fahamu zake.

7: Vipimo hutegemea na yale atakayong'amua mtaalamu wa afya.

8: Tiba hutegemea na kilichofikiwa kama tatizo la msingi.

Hapa chini ni baadhi ya kasoro kwenye mwili zinazoweza kusababisha mtu kupoteza fahamu:

1: Kasoro ya mapigo ya moyo (juu vs chini).

2: Kasoro ya maumbile ya moyo valvu.

3: Kasoro ya mishipa ya damu kuwa midogo/stenosis.

4: Tatizo la presha kuwa juu vs chini.

5: Tatizo la mishipa ya fahamu kwenye ubongo.

6: Tatizo la sukari kuwa juu au chini.

7: Kupoteza fahamu kutokana na hali au mazingira. Mfano: usipokunywa maji ya kutosha, stress, uoga vs panic, njaa, matumizi ya pombe, kujisaidia haja ndogo na kukohoa kwa nguvu nk.

8: Kubasiliaha mkao au mwelekeo wa mwili. mfano: kutoka kulala kwenda kukaa au kusimama.

9: Shida kwenye mishipa ya moyo.

10: Kutanuka kwa moyo na kufeli

11: Kipanda uso/migraine

12: Kuongezeka kwa preasure kwenye eneo la ubongo/fuvu kwa kuongezeka chochote, mfano: majimaji nk.

13: Matumizi ya baadhi ya dawa

NB: Kwa kuangalia wigo wa matatizo husika ni vyema mhusika kufikishwa kwenye kituo cha afya na kusikilizwa vyema na daktari/ukimpata bingwa wa magonjwa ya ndani(physician), kufanyiwa ukaguzi na vipimo mwafaka ni vyema sana.

Ni vizuri mgonjwa huyu kuandamana na mtu aliyewahi kumuona akipoteza fahamu kama ikiwezekana pia au anaejua vyema historia ya maisha yake.
 
Shukrani kwa wote mliotoa maono. Hii issue ilimtokea miezi 3 baada ya kujifungua. Leo hii hospitali zote walichokifanya,wamempa dawa za kifafa. Hapa,ni kwamba kuanguka kwake,hudodonka taratibu kiasi kwamba hajawahi kuumia. Sema tu baada ya miaka 3 tangu augue,aliwahi kuanguka jikoni na akaungua.
Hiyo hali ikimtokea,haelewi chochote. Hata umfinye,haumii. Hata haichukui mda kuisha. Wakati mwingine akiwa na kitu mkononi,utaona tu ameachia,akiwa amekaa kwenye kiti,hasa cha plastic,utaona kajiegesha,hadondoki. Na badae kama dakika 10-15 au 20, akili zinarudi. Ukimuuliza,anakumbuka vizuri alichokuwa anafanya kabla ya kuanguka. Na anakwambia mwili mzima unakuwa umelegea sana,anajihisi uchovu wa hali ya juu. Lakini hapo hapo maisha ataendelea. Akianguka,povu,kujikojolea, hapana.
 
Afanye CT SCAN ya kichwani, atakua na kovu huyo kwenye ubongo, kabla ya hili tatizo ukute kuna sehemu alipigisha kichwa akaona amepona ila kumbe lilileta athari kwenye ubongo ikaweka kovu, ambalo kuna mda linakata mawasiliano....
 
Asante mkuu. Hiyo kitu ilifanyika matokeo yakaonyesha hana tatizo. Mpaka tunafikia hatua ya kutafutia kwa wale madoctor wa vijijini,tulihangaika sana,tena sana
 
Shukrani kwa wote mliotoa maono. Hii issue ilimtokea miezi 3 baada ya kujifungua. Leo hii hospitali zote walichokifanya,wamempa dawa za kifafa. Hapa,ni kwamba kuanguka kwake,hudodonka taratibu kiasi kwamba hajawahi kuumia. Sema tu baada ya miaka 3 tangu augue,aliwahi kuanguka jikoni na akaungua.
Hiyo hali ikimtokea,haelewi chochote. Hata umfinye,haumii. Hata haichukui mda kuisha. Wakati mwingine akiwa na kitu mkononi,utaona tu ameachia,akiwa amekaa kwenye kiti,hasa cha plastic,utaona kajiegesha,hadondoki. Na badae kama dakika 10-15 au 20, akili zinarudi. Ukimuuliza,anakumbuka vizuri alichokuwa anafanya kabla ya kuanguka. Na anakwambia mwili mzima unakuwa umelegea sana,anajihisi uchovu wa hali ya juu. Lakini hapo hapo maisha ataendelea. Akianguka,povu,kujikojolea, hapana.

Sawa, kuna mambo yanahitaji ufatiliaji:

1: CT scan bado pia uko mbali kwenye issue ya kifafa, huwezi kukikanusha kwani kuna vitu bado unaweza uvikose kutokana na uwezo wa CT.

2: MRI vs EEG: pia unaweza kupata majibu chanya au hasi. Maana MRI pia lazima kuwe na physical damage na nyingine ni kwenye mishipa ya fahamu, EEG ina wastani wa 65-70 baada ya tukio ili kupata na hapo ufanye resting vs stress EEG. Sijui kama vilifanyika.

2: Presha yake wakati wa ujauzito ilikuwaje?

3: Alifanya ECHO Vs ECG?

NB: Kifafa si lazima mtu aanguke, atoe mapovu, atoe mkojo au choo, apoteze fahamu na kurusha mikono na miguu.

Kuna aina mbalimbali za vifafa, mfano: kuna absence seizure ambayo mtu hupigwa na bumbuwazi tu, au kung'ata sehemu ya nguo kama kishikizo au kukodoa tu macho.

Kama wataalamu walishawishika hivyo, ni vyema kuzingatia na kuona baada ya kuanza dawa kama kulikuwa na maendelei chanya kwani kuna wakati wataalamu wanafanya maamzi kwa kutumia waliyoyapata kwa mgonjwa/ clinical findings kuliko majibu ya kipimo na inaruhusiwa kwa kujega hoja za kitaalamu.

Pia kuzingatia vitu vya kuepuka ili kupima maendeleo yake kama: kutumia tiba ipasavyo, kutokutumia pombe, kuepuka mwanga mkali, kupumzika vyema, stress, uchovu wa kupindukia nk.

Hii haikuzuii kuendelea kupata maoni mbadala, lakini hakikisha kutoa taarifa kamili za mgonjwa kwa yule unaempatia nafasi ya kulitizama upya. Utoe historia kamili ya hadithi ilivyoanza, kilichofanyika na maendeleo yake/ utofauti baada ya kuanza tiba na sasa.
 
Shukrani kwa wote mliotoa maono. Hii issue ilimtokea miezi 3 baada ya kujifungua. Leo hii hospitali zote walichokifanya,wamempa dawa za kifafa. Hapa,ni kwamba kuanguka kwake,hudodonka taratibu kiasi kwamba hajawahi kuumia. Sema tu baada ya miaka 3 tangu augue,aliwahi kuanguka jikoni na akaungua.
Hiyo hali ikimtokea,haelewi chochote. Hata umfinye,haumii. Hata haichukui mda kuisha. Wakati mwingine akiwa na kitu mkononi,utaona tu ameachia,akiwa amekaa kwenye kiti,hasa cha plastic,utaona kajiegesha,hadondoki. Na badae kama dakika 10-15 au 20, akili zinarudi. Ukimuuliza,anakumbuka vizuri alichokuwa anafanya kabla ya kuanguka. Na anakwambia mwili mzima unakuwa umelegea sana,anajihisi uchovu wa hali ya juu. Lakini hapo hapo maisha ataendelea. Akianguka,povu,kujikojolea, hapana.
hii hali imeshawahi kunitokea kama mara tatu ila ilikuja ikaacha yenyewe nadhani ilisababishwa na stress kuzidi naona toka nimeweza ku-handle stress na kupuuza baadhi ya mambo akilini ndo hiyo kitu imeacha.

Ikitokea mtu unaona kabisa hapa naondoka na unaweza hadi kutanguliza mikono ili usianguke vibaya ila fahamu zinapotea then unahisi mwili kama una ganzi unatekenya tekenya unakuwa na ile feeling kama ya mtu aliealalia mkono kwa muda mrefu then hauchukui muda unarudi kuwa sawa na unakuwa na kumbukumbu kwamba umeanguka, Ila hujui umeanguka kwa muda gani ila kwa mimi nilihisi ni kama nilikuwa nachukua sekunde kama 5 nazinduka.
 
Ni tumaini langu wote mu wazima wa afya.
Kama mada ilivyo hapo juu,leo nimekuja kuomba msaada.
Nina ndugu,mwana mama mtu mzima. Kwa mda wa miaka 10 sasa,ana tatizo la kuanguka. Kwa siku inaweza tokea zaidi ya mara tatu. Na si kwamba ni kila siku,inaweza ikapita hata wiki au wiki mbili. Na si kifafa. Akianguka inakuwa kama vile kapatwa na kizuguzungu,lakini akirudi katika hali yake,anakuwa hakumbuki kama hali hiyo imemtokea.

Kwa yeyote anayejua mtu wa kusaidia,tafadhali naomba tuwasiliane inbox. Kila tulipojaribu wanadai watatibu,wanaishia tu kula pesa basi.

Lazima uanguke tu kwa wanaume ulotembea nao we malaya
 
Atakuwa ama anasumbuliwa na High Blood Pressure au ana upungufu mkubwa sana wa haemoglobin kwenye damu. Mpeleke kwa dakari haraka sana usije ukampoteza
 
Back
Top Bottom