Mr Zed
New Member
- Dec 20, 2020
- 3
- 1
Habarini wakuu! kabla sijaenda kwenye hoja yangu kama kichwa kinavyojieleza nitoe shukrani zangu za pekee kwa Mwenyezi Mungu anipae uhai, Wakuu ni wiki ya pili sasa tangu nilipoanza kupata tatizo la maumivu ya tumbo eneo lote la kitovu pamoja na pembeni kidogo upande wa kulia wa tumbo usawa na kitovu.
Siku mbili baada ya kuanza tatizo girl friend wangu alinishauri nitumie dawa ya kienyeji ya U.T.I akidhani ndo litakuwa tatizo baada ya yeye kwenda hospital akaambiwa ana hilo tatizo nilitumia hiyo dawa ya kienyeji siku 4 mfululizo 1x3 kila siku lakini hali iliendelea kuwa vilevile, siku ya 6 niliamua kwenda dispensary moja ya chuo kikuu kimoja huku kanda ya ziwa nikapimwa choo pamoja na mkojo lakini niliambiwa sina tatizo lolote ingawa haja kubwa ilikuwa lain sana mithili ya mtu anaeharisha lakini doctor aliniambia ni hali ya kawaida tu na kwamba hakuna tatizo lolote kwa mjibu wa vipimo.
Nilipewa flagly kusaidia, nilitumia kwa muda wa siku tatu bila mafanikio kabisa niliendelea kupata haja kubwa laini sana na maumivu ya tumbo yasiyo na miungurumo siku iliyofuata nilirudi hospital kupima tena, doctor alinipima tena vipimo vilevile lakini hakukuta tatizo alinipa dawa fulani hivi zimeandikwa kwa kifupi diclof kwa ajiri ya kupunguza maumivu lakini sijaona mafanikio toka juzi hadi leo ni siku ya tatu.
Basi leo nimejaribu kumpigia simu doctor fulani ni rafiki yangu akanishauri niende hospitali kubwa kwa ajiri ya vipimo zaidi. Wakuu hali yangu siyo mbaya sana ispokuwa nakosa raha kabisa kwani tumbo linauma mfululizo hadi sek 10 hadi 15 ndipo linaachia nakutulia kabisa kama vile hakuna shida yoyote baada ya muda kidogo tena linabana.
Nimejaribu kufanya jitihada binafsi kama vile kutumia maji ya uvuguvugu, matunda na mboga za majani kwa wingi pamoja na kuhakikisha nakula chakula laini lakini juhudi zangu hazijazaa matunda kabisa.
Naombeni ushauri wakuu pengine shida inaweza ikawa ni nini maana tumbo bado linauma ingawaje si mfululizo sana lakini pia naanza kusikia maumivu kwa mbali kifuani upande wa kulia ahsanteni.