Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
TATHMINI YA AWALI YA UVURUGAJI WA MCHAKATO WA UCHAGUZI KWENYE HATUA ZA KUCHUKUA FOMU, KUREJESHA NA UTEUZI NA MWELEKEO WA ACT WAZALENDO KWENYE UCHAGUZI HUU.
A. Utangulizi
Kama tulivyoeleza awali, Chama chetu kupitia Kikao cha Kamati Kuu kilidhamiria kushiriki uchaguzi wa marudio ulioitishwa kwenye Jimbo la Buyungu na Kata 79 nchi nzima. Tuliweka bayana kwamba tutagombea kwenye maeneo kadhaa ya kimkakati kwetu na tutafanya hivyo kwa kushirikiana na wenzetu wa vyama vingine vya upinzani. Imani yetu ni kuwa uchaguzi huu si tu utakuwa jukwaa la kitaifa la kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu mwelekeo wa nchi yao bali utakuwa ushahidi mwingine wa kufilisika kisera na kimvuto kwa Chama cha Mapinduzi na kutokubalika kwake kwa wananchi.
Dalili za haya yote zimejionesha kwenye hatua za uchukuaji fomu, urejeshaji wa fomu hizo na uteuzi wa wagombea. Ni dhahiri kwamba CCM haiku tayari kushindana na vyama vya upinzani kwenye majukwaa na sanduku la kura. Bila haya, chama hicho kupitia vyombo vya dola kimeamua kutumia mbinu za kinyang'anyi na kihuni kuhakikisha kwamba kinapita bila kupingwa kwenye kata mbalimbali.
B. Uchambuzi wa Awali wa Dosari Kwenye Hatuaza Uchukuaji wa Fomu, Urejeshwaji wa Fomu na Uteuzi wa Wagombea;
C: Kisa cha Tunduma: Wagombea wote wa Upinzani Wapokonywa Uraia.
Huko Tunduma, vyombo vya dola vimetumika kuwatisha, kuwakamata na kuwaweka ndani wagombea wa upinzani kwa malengo kwamba wasiweze kuchukua fomu.
Kwa wale waliofanikiwa kuchukua fomu, Idara ya Uhamiaji imewatangaza kuwa wagombea wote nane si raia wa Tanzania na hivyo hawana sifa ya kugombea. Hata wagombea wetu watatu (Kata za Kaloleni, Mpemba na Mwakakati) walipopeleka vielelezo na vitambulisho kuthibitisha uraia, msimamizi wa uchaguzi aligoma kuvipokea.
D. Kiini cha Tatizo:
E. Wito na Hatua za Kuchukua:
F. Mwelekeo wa Chama kwenye Uchaguzi:
Hadi pazia la kurejesha fomu linafungwa, Chama chetu kilikuwa kimeamua kusimamisha wagombea kata 20. Wagombea wanne kati ya hao (Tunduma na Tarime) wamefanyiwa njama na kutoteuliwa.. Tunaendelea kufanya mazungumzo na wenzetu wa vyama vingine baada ya kila chama kufahamu kwa hakika kata walizofanikiwa wagombea wake kuteuliwa ili kuachiana maeneo ya kimkakati na kuwa na mkakati wa pamoja kukabiliana na vitendo vya uvurugaji wa uchaguzi.
Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi
ACT Wazalendo
17 Julai 2018.

- Muda mwingi, Wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi walifunga ofisi zao baada ya wagombea wa CCM kupewa fomu na kuzirejesha. Lengo ni kuhakikisha wapinzani hawapati au kurejesha fomu kwa wakati.
- Kwenye baadhi ya maeneo, Chama cha Mapinduzi kilitumia mtandao wake au vyombo vya dola kuwatisha watia nia wa vyama vya upinzani ili wasichukue fomu.
- Vyombo vya dola vilitumika kuwakamata baadhi ya watia nia wa vyama vya upinzani na kuwaweka mahabusu ili wasiweze kurejesha fomu.
- Wagombea wa upinzani kutangazwa kuwa si raia ili kunyimwa sifa ya kugombea kama ilivyotokea hukoTunduma. Tutaelezea hapa chini.
- Wagombea wa upinzani kushambuliwa na kupokonywa fomu wakati wa kuzirejesha.
- Wagombea wa upinzani waliopitishwa kuendelea kutishwa na kufuatiliwa na vyombo vya dola ili kuwanyima amani ya kufanya kampeni.
- Tume ya uchaguzi kutotoa ushirikiano wa kutosha kuhusu malalamiko haya na mengine yanapowasilishwa kwake.
C: Kisa cha Tunduma: Wagombea wote wa Upinzani Wapokonywa Uraia.
Huko Tunduma, vyombo vya dola vimetumika kuwatisha, kuwakamata na kuwaweka ndani wagombea wa upinzani kwa malengo kwamba wasiweze kuchukua fomu.
Kwa wale waliofanikiwa kuchukua fomu, Idara ya Uhamiaji imewatangaza kuwa wagombea wote nane si raia wa Tanzania na hivyo hawana sifa ya kugombea. Hata wagombea wetu watatu (Kata za Kaloleni, Mpemba na Mwakakati) walipopeleka vielelezo na vitambulisho kuthibitisha uraia, msimamizi wa uchaguzi aligoma kuvipokea.
D. Kiini cha Tatizo:
- Kiini cha tatizo ni kithiri kwa makada wa CCM walioteuliwa kwenye nafasi za Ukuu wa Wilaya na Ukurugenzi. Wateule hawa wanapigana kufa na kupona kuhakikisha kwamba CCM kinajitwalia ushindi uchaguzi kwenye kata zote kwa namna yoyote ile hata kwa hila kama tunavyoshuhudia.
- Kuporomoka kwa kukubalika kwa CCM na serikali ya awamu ya tano kunakipa wasiwasi chama hicho kuweza kuwakabili wapinzani kwenye uchaguzi na kuwashinda. CCM kimekuwa chama chakavu kwa fikra na uwezo ambacho hakiwezi tena kushinda hata kata bila mbeleko ya dola.
E. Wito na Hatua za Kuchukua:
- Chama chetu kitasimama kidete kwa njia za kisheria kuhakikisha kwamba wagombea wetu waliopokwa uraia wao na CCM kwa uchu wa madaraka wanapata haki yao.
- Chama chetu kitashirikiana na vyama vingine vya upinzani kuhakikisha kwamba wapinzani tunatuma ujumbe madhubuti kabisa kwa CCM kuwa tumechoka na ubakaji wao wa demokrasia.
- Tunatoa wito kwa waangalizi wa ndani kufuatilia kwa karibu vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa misingi ya kidemokrasia ulioshamiri kwenye uchaguzi huu wa marudio hata kabla ya kampeni kuanza.