Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,316
- 10,782
Soma Zaburi 17.
Sala ya kuomba kuokolewa kutoka kwa wadhalimu.
Mstari wa 10 hadi 14:
Adui wa nafsi yangu wanaonizunguka,wameshupaza mioyo yao,vinywa vyao vinasema kwa kiburi. Sasa wametuvizia,wametuzingira pande zote; wameyakaza macho yao ili watuangushe chini. Wanafanana na simba atamaniye kurarua,kama wana simba wanyemeleao mafichoni. Simama, ee BWANA,uwakabili,uwaangushe chini; kwa upanga wako uokoe nafsi yangu na mwovu. Waangamize kwa upanga wako; kwa mkono wako, Bwana,waangamize;waondoshe ulimwenguni katika ujana wao. Wajaze matumbo yao kutoka hazina yako,wana wao washibe pia na wawaachie akiba yao wana wao.
Zaburi hii ni lalamiko la mtu aliyeshtakiwa kwa uongo,anamwomba Mungu,hakimu wa haki,kumthibitisha yeye na kuwaadhibu washtaki wake wabaya.