Tathmini: M4C Fundraising Dar wapi hapakuwa sawa na nini Kifanyike

Tathmini: M4C Fundraising Dar wapi hapakuwa sawa na nini Kifanyike

M4C ilikuwa kichaga zaidi nazani hata wewe umeona wengi waliopewa nafasi ya kuzungumza chochote ni wakaskazini.
2.mbowe aliponda kutangaza nia za ubuge au urais lakini kuna watu wawili wametangaza nia za ubunge serengeti na kwa mh chami.
3.kauli za kibabe za lema juu ya makampuni ya simu kana kwamba anahisa.
4.kauli ya nassari kwamba Tz ni laini sana kama maini
5!mwenyekiti mbowe kamaliza kuongea lakini bado kuna jamaa wanaendelea kuongea
6.mtangazaji hajui chochote hata jina la chama

Shughuli nzima ilikuwa haijapangiliiwa vizuri. Ni lazima muwe na ujumbe mahsusi ili kuweza kuwa convince watu mnachokifanya na sio kuropoka against CCM. Tell us your M4C story. Acheni lugha za kihuni. Jifunzeni protocol! Sio kila mtu anaongea kwa vile tu ni mashuhuri. Sasa kwanini anaaanza kuongea Mbowe, Lema halafu Nasari why not vice versa??? Mwisho amefunga Mkiti, Nasari anaingia kusoma message.

Inaonekana Mbowe ana ubabe fulani hivi...kila saa anajiongelea yeye...halafu anasema sisi wasomi ni waoga. Mind your language Mkiti na hizo speech zako uwe umeziandika. Watu wameandaa shughuli stick to the basics siyo kuanza kubeza watu.

Uongozi wa kitaifa ulikaribishwa na wa CHADEMA Dsm matokeo yake mkadominate shughuli yote na MC-uso wa Dada Rose ulikuwa unaonyesha she is just not happy....

Lema alikuwa amekunywa? anaambiwa aongee experience ya Arusha anatupa ishu za London sijui magari? Mara nisiporudi mimi anakuja Dr Slaa...lol
jipangeni sawasawa:A S 465:
 
slaa alikuwa moro akipambana,mbowe alikuwepo dar.zitto lazima abaki bungeni hawawezi kuliacha bunge bila kiongozi

mkuu ni busara kupongeza pala mazuri yanapofanyika na kukosoa makosa ya maksudi. Zitto kachemsha sana. When he does good we both feel good and vice versa is true.
 
Hiyo star tv hawakuitangaza hiyo shughuli kabla,next time nashauri watoe matangazo hata kwenye radio maarufu na magazeti,na pia lema,mbowe,nasari walijitahidi sana
 
Si busara sana kulalamika kwa mapungufu yaliyojitokeza katika tukio la leo na si vibaya kupongeza na kudumisha yote mazuri katika tukio hili hapo SERENA HOTEL.

Nini Tathmini yako Mpenda mbadiliko na nini kifanyike siku zijazo?

Mkuu mi ntaku Pm nikupe nini Kifanyike..waze wakucopy na kupaste wameshatega antena zao au unataka nimwage mchele?
 
Nimeangalia hiyo M4C Star TV nilichokiona ni vituko vitupu ubabe wa kijinga wa Lema, anasema makambuni ya simu mkituhujumu tutapita mitaani tutakusanya kadi zenu tutazitupa chooni.

Nassari naye anasema nchi hii ni laini kama maini, Lema kaishachagua kabisa Chopa kabla ya michango.

Wizi mwingine kupiga picha na Mbowe Sh50,000

Halafu kwa nini simu zote za kuchangia zilikuwa zinatoka Arusha, na Kilimanjaro, sikusikia simu kutoka mikoa mingine.

Like Govt Like citizen....tunahitaji Majawabu siyo Majibu yaliombatana na kulalamika
 
Joyce Mukya (Mb) alikuwa anaboa, kama alijua anakuja kwenye hiyo shughuli, alipaswa awe ameshaongea na hao aliokua anawaita "watu wangu" wa arusha, na pale alitakiwa aje kuwakilisha tu. It was like amekurupuka hivi. Otherwise, mengine ni ya kawaida tu

Ni mh. lkn anaushamba(joyce) kwa mbaliiii! lack of exposure, kwa kuwa ilikuwa fundrising kupokea na kutoa taarifa mbali*2 ulitakiwa kujizuia wee mwenyewe usiiboe audience...siku ya jana mihemuko ya uchangiaji ni lazma na ingetoka palepale, kwa athari na ridhimz ya wachangishaji(washereheshaji)ndo maana nzma na msingi wa FR(FUNDRISING) ROSE mm namkubali sana sio mwoga. kuna watangazaji wa hovyo nyie achani,, rose na akina jenerali ulimwengi bomba.. akina gondwe, yule jamaa wa clouds domodomo wale magamba tu
 
Niseme ukweli kabisa...Shughuli ya jana ilikuwa poorly organized. Namnukuu Mwakitwange "Leo ndio nimejua kufanya kazi na wanasiasa". Lema, Nassari na Joyce Mukya walizidi mno kumuingilia MC na kutofuata ratiba. ni kama vile hakukuwa na ratiba na ndio maana hata ufungaji haukuwa mzuri
 
Joyce Mukya (Mb) alikuwa anaboa, kama alijua anakuja kwenye hiyo shughuli, alipaswa awe ameshaongea na hao aliokua anawaita "watu wangu" wa arusha, na pale alitakiwa aje kuwakilisha tu. It was like amekurupuka hivi. Otherwise, mengine ni ya kawaida tu
Point, pamoja na Dogo Janja. In fact tukio zima lilikuwa la kustukiza, labda kama walikuwa wanapima uwezo wao wa kumobilize watu at emergency cases.
 
Niseme ukweli kabisa...Shughuli ya jana ilikuwa poorly organized. Namnukuu Mwakitwange "Leo ndio nimejua kufanya kazi na wanasiasa". Lema, Nassari na Joyce Mukya walizidi mno kumuingilia MC na kutofuata ratiba. ni kama vile hakukuwa na ratiba na ndio maana hata ufungaji haukuwa mzuri

Sina shaka kamati ya Maandalizi watakuwa wameyaona haya na kuyachukua kama sehemu ya kuboresha Kampeni hizi endelevu. Ila na hakika kabisa hata MEDIA Coverage jana haikuwa katika kiwango kama nilivyohadharisha hapo mwanzo.

Sikumuona Muongozaji wa matangazo ya TV na kama alikuwepo basi alikuwa QUITE sana ama ni dhaifu katika kazi yake, Nikilinganisha na mabo nilivyokuwa nikyaona pale NAURA SPRING Arusha, Kamanda Yahya Mohamed alikuwa anapanda ngazi na kushuka na alidhibiti nidhamu ya Stage, MC na mtangazaji wake. Hakuna mtu aliyepanda pale juu bila idhini yake.

Pia niliona walikuwa na mtiririko mzuri wa matukio na washereheshaji walipata muda wao kutawala jukwaa na kuhamasiha shughuli za uchangiaji tofauti na jana sikuona muongozo wowote na mara kadhaa MC alikatizwa sana na zile panda shuka za Makamanda. hakika matukio kama haya yanahitaji Nidhamu ya hali ya juu bila kuangaliana usoni.

Ni hatua nzuri na inahitaji kuendelezwa kwa kufanyiwa ukarabati pale tulipokosea jana


ADIOS
 
Mkuu mapato na matumizi ni muhimu kuwekwa hadharani ili kujenga imani na hamasa kwa wachangiaji na wanachama at large
 
Pongezi sana kwa kufanikisha hilo zoezi kwa usalama.

Ushauri wangu kwenu ni huu:

1.Kabla ya kuanza mkutano kuwepo na mchanganuo wa fedha za awali zilivyotumika. Hii itasaidia kuongeza uwazi na kuongeza hamasa kwa watoaji kuamini kuwa wanachokitoa kinatumika ipasavyo.

2.Halafu ningependekeza iwe ni hafla maalum ambayo itakuwa na tiketi maalum ambazo zitatangazwa kwenye vyombo vya habari kwa muda usiozidi mwezi au wiki mbili tu kabla ya tukio lenyewe.

Hitimisho: Natoa pongezi za Dhati kwa Wote Walioshiriki....

N.B:Msingi wa chama chochote Duniani ni kusikiliza maoni, ushauri kutoka kwa Wanachama wake....''J. K. Nyerere
 
It was not well organised,the majority are not informed about the concerned event,poorly bogus mc(lema)kaskaziniasm dominance,wish I could see our becoming president the powertiller zitto zuberi kabwe kwani mambo yote yangekua barabara kabisa kwani jamaa ni mtaalam wa organisation,function ya watu wachache imewashinda ,je ile ya lekadutigite kigoma aliyoorganise jamaa ya maelfu ya watu mngeweza?next time mwambieni awafundishe topic on how to organise a functions,acheni kujifanya wajuzi wakati mko empty headed!
 
Nawapongeza sana kwa wanayoyafanya. ushauri wangu ni;

  1. Waweke matangazo ya kuhamasisha uchangiaji, na kukumbusha namna ya kuchangia kwenye vyombo vya habari kama TV, redio na magazeti
  2. Waombe nafasi JF, kuwe na sticky thread inayokuwa updated mara kwa mara juu ya hali ya uchangiaji, nini kimechangiwa, kimechangiwa na watu wangapi, nini kinahitajika, na kuhamasisha watu wachangie
  3. Mtu akichangia kwa m-pesa, ajibiwe kwa msg, ikionyesha hadi wakati huo ameshachangia kiasi gani (hiyo namba yake), akaunti ina kiasi gani, kimechangiwa na watu wangapi, na akaribishwe na kuombwa kuendelea kuchangia
  4. Afisa habari, ama ikiwezekana katibu mkuu awe anaongea na waandishi wa habari, angalau mara moja kwa mwezi, akitoa taarifa, pamoja na mambo mengine, progress ya M4C (wamefanya mikutano mingapi, wanachama wangapi wapya wamejiunga, nini malengo ya sasa na ya baadae juu ya M4C, atoe almanac ya mikutano kwa kipindi cha mwezi mmoja unafuata), lakini pia atumie wasaa huo kuhamasisha wananchi wachangie M4C.
 
Muendelezo wa kuchangia m4c ni mzuri isipo kuwa maandalizi ya shughuri hayatakiwi kufanywa kwa kushtukiza kama hii. Huu ulitakiwa kuwa hata mpango wa majuma matatu au hata mwezi, kuiandaa shughuri kuwa katika viwango vya uhakika kuanzia uandaaji, ma mc wabobezi na kuhamasisha sana kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Lakini lingine kubwa next m4c contributions gathering iwe inatoa mrejesho wa kilicho changwa na jinsi kilivyotumika. Mfano leo wangeweza ku breaka down mapato ya m4c Arusha na matumizi yake then impact yake kwa ujumla kwenye chama.

Muhimu.
Waziri kivuli wa fedha ambae pia ana cheo cha unaibu katibu mkuu kutokujihusisha na mambo ya chama kwenye fund rising ambayo naamini ni moja ya mambo muhimu na miongoni mwa majukumu ya pamoja ni dosari kubwa kwake. Hawezi kuwa raisi kwa kuota kwenye vyombo vya habari! Apambane ili chama kiopate fedha kifike kule anakota azipate kura za uraisi.

Mkuu hapo kwenye bold umenena. nilitamani nikugongee LIKE 100.
Kama anaweza kukimbia majukum ya chama akaweza kuwahi mahojiano redioni halafu issue kubwa kama hii haonekani. Nahisi anajiandaa kuwa mgombea binafsi.
 
It was not well organised,the majority are not informed about the concerned event,poorly bogus mc(lema)kaskaziniasm dominance,wish I could see our becoming president the powertiller zitto zuberi kabwe kwani mambo yote yangekua barabara kabisa kwani jamaa ni mtaalam wa organisation,function ya watu wachache imewashinda ,je ile ya lekadutigite kigoma aliyoorganise jamaa ya maelfu ya watu mngeweza?next time mwambieni awafundishe topic on how to organise a functions,acheni kujifanya wajuzi wakati mko empty headed!

You have a personality syndrome. This is about doing things not about who is doing it. With or without Zitto M4C is here, will be here and there to achieve its moral and material objective
 
You have a personality syndrome. This is about doing things not about who is doing it. With or without Zitto M4C is here, will be here and there to achieve its moral and material objective

Zitto kakosa mvuto, so he has to slow down as chadema frontliner until he resolve his corruption allegation.
 
Back
Top Bottom