Kukosekana kwa baadhi ya Makamanda kusichukuliwe kama kigezo cha kuonyesha umoja au uhai wa CHADEMA. Kumbukeni hizi ni Kampeni endelevu za Kanda kwa kanda, Kaskazini washamaliza, jana ilikuwa Pwani, Kanda ya ziwa wanafanya maandalizi, watafuata kusini na hatimaye kilipo kitovu cha kutunga sheria.
Kamanda Mbowe alikuwa pale kama mgeni rasmi, sawa tu na ambavyo kanda ya ziwa wakiamua mgeni rasmi awe PhD na Mbowe asiwepo.
Kukosekana kwa Makamanda wengine ZZK, Sugu, Msigwa, Mnyika, Mdee na wengineo hakumaanishi kuzorotesha nguvu ya CDM. CDM ni nguvu ya Umma na si kiongozi mmoja mmoja, wao ni watia hamasa tu na kuelekeza njia sahihi.
Utashangaa watu leo humu wameshupaa na Slaa, Zito jamani hawa si Chama. Kama alivyosema Mbowe ''NIKIFA MSILIE WEKENI MAITI YANGU PEMBENI NA ENDELEENI NA HARAKATI ZA UKOMBOZI''. Kwa unayefahamu kiswahili fasaha huu ujumbe haumaanishi kwamba itelekezeni maiti yangu basi iliwe na wanyama HAPANA bali yeye si Chama hata akifa au kutoka CDM itabaki na mapambano yataendelea kwa kuwa Chama hiki ni nguvu ya UMMA.
ADIOS