Mkuu wangu
THE BIG SHOW, sitaki kuwa mnafiki katika hili... ni Waislamu wenyewe ndio tunapotosha dini yetu. Kule Mombasa aliuawa Sheikh, kuona hivyo, Sheikh Ilunga akawahamasisha Waislamu kwamba Kuran imetoa ruhusa ya kisasi na hivyo, kv Sheikh ameuawa basi Waislamu wa Mombasa nao badala ya kuchoma magari moto, waue padri au askofu... akafanya reference Surat Baqara 178! Ni matumaini yangu unasoma Koran..., Surat Baqara 178 inaanza kwa kusema "Enyi mlioamini! Mmepewa rukhsa kulipa kisasi katika waliowaua... muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke...." na mwisho wa aya hiyo inamalizia "Na atakayeruka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu iumizayo"
Mkuu wangu ikiwa ulienda Madrasa na ukatulia bila shaka unafahamu Koran ilikuja kidogo kidogo kwa miaka zaidi ya ishirini kwavile baadhi ya Aya zilikuwa zinashuka kuja kukemea au kufunza jambo fulani! UKisoma Koran bila kufahamu historia ya kila aya, lazima utatafsiri ndivyo sivyo! Kwa mfano, Aya niliyoitaja hapo juu ilikuja kukemea tabia za Waarabu wa wakati ule... ilivyokuwa, mathalani kv NasDaz mimi ni hoe hae, ikitokea kwamba mathalani nimeua Housegirl wa JK, kwa tabia za Waarabu wakati ule wangesema kv JK Family ni royal family, basi House Girl wao ni sawa na Baba mwenye nyumba wa familia ya NasDaz! Kwahiyo, ingewaje nimeua Housegirl, ktk kulipiza angeuawa baba yangu!! Au tuseme ingekuwa Riziwan ananiua mimi... kwa tabia zao wakati ule, wangesema kv Riz1 ni from Royal family na NasDaz alieuawa ni hoe hae, basi wao wangetoa labda Shamba Boy ili ahukukumiwe. Kutokana na tabia hiyo ambayo ilienea miongoni mwa Waarabu, ndipo ikashuka Surat Baqara 178 na kusema "Mtumwa kwa Mtumwa" na "Muungwana kwa Muungwana" na si ten kujifanya hawa ni untouchable na wale ndo wasio na haki! Lakini Baqara 179 inamalizia " mtakuwa nao uhai katika kulipiza kisasi enyi mlioamini" Hapa sababu ikiwa wazi kabisa kwamba ikiwa unafahamu kwamba ukiuawa nawe utauawa, basi lazima utaogopa tu!!
Lakini Sheikh Ilunga baada ya kuuawa yule Sheikh wa Mombasa, yeye akasema basi akamatwe Padri nae auawe! Lakini lazima tukumbuke kwamba hukumu zote ktk Uislamu zina taratibu zake... mathalani, ingawaje hukumu ya Mwanamke mzinzi ni kupigwa mawe hadi kufa huwezi kufanya hivyo hadi patokee mashahidi wannne wenye kuheshimika na kumuogopa Mungu washuhudie kwamba mwanamke huyu amezini... Sasa Ilunga anapohamasisha watu wakamate padri wauwe kwa kutumia taratibu zipi? Haidhuru, hata Koran iliyaona hayo mapema ndio maana ikamalizia "Na atakayeruka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu iumizayo!" Huwezi kusikia Sheikh ameuawa kisha nawe ukakurupuka ukaenda kuua Padri ukasema ndivyo Koran inavyosema.... huko ni kuvuka mipaka ya KOran na wala sioni aibu kusema tuache kupotosha maandiko yetu wenyewe!
Haya turudi kwa hao Boko Harama!! Hivi kweli mnaamini watu kama wale wanapigani dini? NI wapi na lini Uislamu umefundisha kupita kuua watu wasio na hatia? Hivi ni Uislamu gani unakamata mabinti wadogo unaenda kuwaua? Ni mara ngapi Boko Haram kule kwao wameshambulia shule na kuua watoto... ndo Uislamu unavyosema hivyo?
Sasa ikiwa Boko Harama na Sheikh ILunga wanapitisha mipaka ya yale yaliyosemwa kwenye Koran, basi kwa hakika wote ni sawa! Hili silionei haya kulisema hata kama nitaonekana Kafri.