Sina cha kujipendekeza kwao kwavile hawana cha kunipa lakini haitatokea hata siku moja ktk maisha yangu nikatetea watu kama Sheikh Ilunga, Al Shabab, Boko Haram na wengine kama hao! Kama adhabu yangu itakuwa ni kutupwa motoni, am ready to take the chance kuliko kutetea ujinga!!
Kwamba Uislamu unatukanwa mimi nafanya nini; labda nikuulize ulitarajia nifanye nini... kwahiyo ulitaka nami nifunge kibwebwe nianze kutukana Ukristo ili kuwaaminishia nyinyi kwamba nami ni Mwislamu safi... unafiki si ada yangu! Humu jamvini si mara moja wala mara mbili, nimeshapata hadi kuhitilafiana na watu wanaokashifu Uislamu, lakini naangalia mazingira! Haiwezekani mimi niwatetee wauaji kwa jina la Uislamu kisha mtu autukane Uislamu halafu mimi nije juu... na ndio maana hata kwenye Koran imesemwa wazi, usiwatukanie dini yao wasije wakaitukana dini yako. Lakini yote kwa yote, wakati unaamini kwamba najipendeza kwa hao unaowaita makafiri, jaribu kwanza kuisoma Signature yangu ndipo utabaini NasDaz ni mtu wa aina gani!