Inaelekea wewe ni Mwislamu mwenzangu lakini usiyetawaliwa na jazba za kijinga kama wengine! Labda nikuulize jambo moja ndugu yangu, uliwahi kuiona ile video ya Sheikh Ilunga aliyozungumza baada ya Sheikh mmoja kule Mombasa kuuawa? Sheikh Ilunga anasema kwamba kwenye video husika kwamba, akiuawa Sheikh mmoja, msivunje magari bali tafuteni padri au askofu muueni....!!! Sasa nikuulize ndugu yangu, hata kama Kuran inasema mtu akiua nae auawe, ndivyo inapaswa kufanya kama alivyokuwa anasema Sheikh Ilunga? Ndivyo tafsiri ya Al Baqara 178 inachomaanisha? Kisha, kwenye muhadhara ule anaendelea kwamba anapouawa Sheikh nyie mnaamua kuvunja magari vioo ni dalili ya kushindwa... kwa maoni yake, na tafsiri zake ambazo siamini kwamba ndiyo usahihi. yeye alitaka wana-Mombasa watafute Padri nae auawe utafikiri hata kwenye Usilamu hakuna taratibu za hukumu.