TANZIA: Rock City Wing

TANZIA: Rock City Wing

Ahsante dada mkubwa, tunamshukuru Mungu hata kwa hili. Kesho saa tisa alasiri tutampumzisha mpendwa wetu
pole sana mdogo wangu ram
Mungu akupe faraja kwa msiba uliokupata...
RIP binamu...
Pamoja sana Rock city
 
Last edited by a moderator:
Tunawashukuruni nyote kwa kutufariji JF Rock City Wing...

Leo ndio tunampumzisha dada yetu mida ya alasiri... :rip: :rip: :rip: Dada Martha!
 
  • Thanks
Reactions: ram
Habari zenu wadau wa Jamii Forums..

Nasikitika kuwataarifu kuwa member mwenzetu dada ram amefiwa na binamu yake.

Msima upo Butimba jirani na Magereza (Mwanza). Naomba tuungane
kumfariji dada ram na wale walioko hapa jijini Mwanza tunaweza kwenda kumpa pole....

"Bwana alitoa na Bwana ametwaa
jina lake lihimidiwe"

Habari ziwafikie WanaJF wote walioko Jijini Mwanza na nje ya Mwanza, wana Rock City Wing wote ThinkPad, Home First, TrueLove, Elizabeth Dominic, Rock City, Mzee Gedeli......

UPDATES

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya jumanne katika makaburi ya Iseni - Nyegezi.

Marehemu alikuwa Mwalimu katika shule ya Iseni na mwanafunzi wa mwaka wa 3 katika Chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT)...

Kwa wanaJF walioko hapa Jijini Mwanza tunaweza kuungana na dada yetu ram siku ya mazishi. Eneo la msiba ni Butimba kwenye kona ya kuelekea Gereza la Butimba.

MORE UPDATES:

Ibada itaanza majira ya saa sita mchana, safari ya kuelekea malaloni itafuatia saa saba na nusu mchana kisha mazishi yatafanyika saa tisa alasiri. WanaJF walioko Mwanza wanaweza kujumuika nasi..

Aksante kwa taarifa Charminglady. Nipo njiani naja kujiunga nanyi.
 
Pole sana dada ram, mitihani tumeumbiwa bin adamu
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: ram
RIP binamu. Poleni familia. Mungu awajalie faraja kuu
 
  • Thanks
Reactions: ram
Pole kwa kumpoteza mmoja wa wapendwa wako,mwenyezi Mungu akupe faraja wew na familia yote ktk kipind hich kigumu
 
Habari zenu wa JF.....

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu kwa mambo mengi anayotufanyia katika maisha yetu, Kipekee nina mshukuru Mungu hata kwa mavuno aliyoyavuna shambani mwake.

Pili niwashukuru wanaJF wote kwa kuungana nami katika msiba huu ulinipata wa kumpoteza ndugu yangu, mdogo wangu na rafiki yangu mkubwa Mwl Martha. Hakika mmekuwa faraja kubwa kwangu na JF rocky city wing, nawashukuru sana sana, nilichojifunza ni kuwa JF ni zaidi ya mtandao bali ni familia ya watu tusiofahamiana (kwa member wengi) lakini ni watu tunaoishi kwa upendo, umoja na mshikamano, Mungu awabariki wote.

Shukrani zangu nyingi zimwendee, ndugu yangu, rafiki yangu na mdogo wang charminglady, kwanza kwa kuleta taarifa hizi hapa lakini pia kwa kushiriki nami kwa kila hatua katika msiba huu, Mungu akubariki sana CL na ninakushukuru sana sana mamii

Mwisho lakini sio kwa umuhimu, nawashukuru JF rock city wing kwa upendo, umoja na mshikamono mliouonesha kwangu tangu mlipopoata taarifa hizi za msiba, mmekuwa nami bega kwa bega hadi jana tulipohitimisha safari ya mdogo wetu Mwl Martha, Mungu awabariki jamani, sina cha kuwalipa ila Mungu atawalipa

Ahsanteni wote, pamoja sana....!
 
Asante kushukuru mamie...... :welcome: :welcome:
 
Back
Top Bottom