Tanzia: Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia

Tanzia: Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia

Pumzika kwa Amani Prof hakika vichwa maji na wale waliojifanya wamevaa kaptula la marx umewaacha.Mawazo yako yataishi (Kivuli kinaishi) Msalimie Shaaban Robert mwambie Tawasifu yake maisha yangu baada ya miaka 50 tunaendelea ingawa bado haijatimia,ukimuona Edwini Semzaba mwambie wakuu wa Shule siku hizi nao wamegeuka Magoswe,mpe hai nyingi Ben Mtobwa mzee wa pesa zinazonuka mwambie watu wanatanua nazo huku,bila kumsahau Elvis Musiba mzee wa njama.Wàsalimie waandishi wote ikiwezekana muendeleze fani katika Ulimwengu mwingine.Wasalamu.
Bila kumsahau Ngalimecha Ngahyoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisoma Rosa Mistika mwaka 1977 pia nikampa babu yangu asome.Mwaka 1978 nikasoma Dunia uwanja wa fujo mhusika mkuu Tumaini.
Nitamnukuu msomi Dennis kwenye kitabu alisema Dunia uwanja wa fujo kila mtu duniani amekuja kuleta fujo zake.Kuna fujo za amani na fujo za siasa.Alitoa mifano mingi ya wanasiasa kina Marx,Hitler,YESU fujo za neno la mungu na upendo.
Hakika Kezilahabi naye amekuja na fujo zake za kuelimisha Jamii kifasihi mungu amlaze pema peponi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwandishi Nguli wa Kazi za Fasihi ya Kiswahili Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia. Tutamkumbuka Kezilahabi kwa kazi zake kama Rosa Mistika, Uwanja wa Fujo, Kaptula la Marx, Nagona na Mzingile! Alitetea Mashairi ya Kisasa!

Hakika, Jabali limeanguka! Tumeondokewa pakubwa.

Pumzika kwa amani Euphrase Vincent Mfunzi Bagaza Tilibuzya Kezilahabi😭😭

Soma; Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu
====

Zaidi Soma:
1. Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu
RIP Prof...
 
Ningependa kujua kama alitajirika kutokana na hivyo vitabu.
 
R.I.P kazelahabi
Nilitamani siku moja nikuone ukiwa hai.
Kazi ya mola haina makosa
 
Ooh prof jamani poleni familia yake pole nchi kupoteza msomi nguli kama huyu upumzike kwa amani professor kezilahabi vitabu vyako nilivisoma, rest in eternal peace.[emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom