Tanzia: Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia

Tanzia: Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia

"Walimwita kakulu. Sasa bado tunamwita kakulu na wajao watamwita vivyo hivyo. Ukweli wake umezingirwa na ukungu wa kisasili. Hakuna mtu aliyewajua barabara wazazi wake. Kuwako kwake kulianza kama mzaha. Yasemekana kuzaliwa kwake kulikuwa kwa ajabu wakati alipokuwa tumboni mwa mama yake alisikika mara nyingi akiingilia mazungumzo ya mama yake na wanawake wengine"

Kezilahabi (1991:1)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwandishi Nguli wa Kazi za Fasihi ya Kiswahili Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia. Tutamkumbuka Kezilahabi kwa kazi zake kama Rosa Mistika, Uwanja wa Fujo, Kaptula la Marx, Nagona na Mzingile! Alitetea Mashairi ya Kisasa!

Hakika, Jabali limeanguka! Tumeondokewa pakubwa.

Pumzika kwa amani Euphrase Vincent Mfunzi Bagaza Tilibuzya Kezilahabi😭😭

Soma; Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu
====

Zaidi Soma:
1. Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu
Pumzika kwa amani E.Kezilahabi. Utakumbukwa daima.
 
Aliyolilosoma hilo li kaptula la Marx basi atupe yaliyomo nasi tumuenxi kwa hilo limkaptula
 
You will go on the cell today
Tafsiri: utawekwa rumande leo?

Jamani hapana.
Huyu ni mtu niliyeheshimu sana utendaji wake wa kazi siku za nyuma. Nikaamini amepikwa na kuiva ipasavyo.

Wizara ya elimu imemwonyesha kupwaya sana, na sasa kutafuta kujitutumua ndio kunamfunua aonekane alivyo mtupu!
 
81695180_10218922723751858_929645847312859136_n.jpg
 
Bageshi. Pitia uzi huu...

Wabheja Bhageshi.
 
Ni kweli kabisa ukimwita Prof. Kezilahabi kuwa Jabali hukosei.

Alikuwa msanii haswaa.

Hongereni Wakerewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sema poleni maana kisha iaga dunia.
Namkumbuka ktk moja ya majadiliano yake alikuwa akijaribu kuelezea maana ya 'thinking' Ilikuwa ni burudani kutulazimisha kuelewa jambo kivingine wakati miaka yote tumekuwa tukiamini tunafahamu. Alikuwa ni Profesa!
 
Kwanini Wakerewe? Kwanini usiseme Watanzania au Waafrika - tuache kupanda basi la ukabila - Kezilahabi hakuwa mkabila
Unajua maana ya Ukabila?

Ni nani amesema Kezilahabi alikuwa mkabila?

Kwenye shindano linalohusisha Wasanii au Wanamichezo wa Afrika Mashariki akishinda Mtanzania inawezekana kabisa Mkenya au Myuganda kusema hongereni Watanzania na sio Hongereni Waafrika japo Mshindi ni Mtanzania na Mwafrika pia.

Je huo utauhitaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwandishi Nguli wa Kazi za Fasihi ya Kiswahili Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia. Tutamkumbuka Kezilahabi kwa kazi zake kama Rosa Mistika, Uwanja wa Fujo, Kaptula la Marx, Nagona na Mzingile! Alitetea Mashairi ya Kisasa!

Hakika, Jabali limeanguka! Tumeondokewa pakubwa.

Pumzika kwa amani Euphrase Vincent Mfunzi Bagaza Tilibuzya Kezilahabi😭😭

Soma; Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu
====

Zaidi Soma:
1. Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu
MNAANDIKA KWA UMAHIRI MTAHISI WAKATI ANAUMWA MLIFIKA HOSPT

RIP PROF
 
Back
Top Bottom