Tanzia: Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia

Tanzia: Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia

pole kwa familia, siku hizi hamna wandishi kabisa, Kezilahabi riwaya zake nzuri sana. Wapo wengi sana ila sijui hawaandiki!
Hamna waandishi siku hizi,Na hata Riwaya zao hazisisimui.
 
'take them inside' akimaanisha wawekwe lupango
Eeeh, wacha Bhwanah! Kweli?

Mbona kazi ipo nchi yetu hii? Huyo ni waziri wa elimu, sio?

Kwani kulikuwa na shida gani ya kuongea Kiswahili hapo, si hao ni wachina, kiingereza cha nini kama hakipandi.
 
Raha ya Milele umpe ee...Bwana na Mwanga wa Milele umuangazie..

Apumzike kwa Amani...Ameen.
 
Marehemu amemaliza fujo zake hapa duniani,maisha hayana maana kwa sababu tuna zaliwa ilitufe, mtu anapo zaliwa tu huanza kukisaka kifo. Maisha ni kifo cha polepole, MWANGA WA MILELE MPE EE BWANA.
Looh, Du!

Philosophia hii:

"...hapa duniani maisha hayana maana..."
"...tunazaliwa ili tufe..."

Yaani, maana ya 'kuzaliwa' ni 'kufa'.

Mbona hapo tayari kuna 'maana' mkuu Junior Lecturer, yaani 'kuzaliwa' maana yake ni 'kufa', au sio?

Nakubaliana nawe kwamba "Maisha ni kifo cha polepole" kwa spidi mbalimbali, wengine hata dakika haitimii, wanaondoka. Baadhi ni miaka na miaka, lakini kwa sasa haizidi miaka 120.

Tutajitahidi sana kuahirisha mauti kwa njia mbali mbali kwa ufahamu wetu wa sayansi, au hata kuhamia sayari nyingine, lakini kifo kiko palepale, au?

'Genetic engineering,' /'cloning' haviwezi kutupatia jibu tuepuke kifo kama tunavyokijua?

Turudi mwanzo wa bandiko lako: kama "maana ya kuzaliwa ni kufa", basi tuzuie 'kuzaliwa'! Tutakuwa tumekishinda kifo!

Samahani kwa mjadala wa ajabu sana huu.

Kezilahabi apumzike kwa amani... hili nalo linaweza kuzua mjadala mkubwa!
 
Ama hakika Prof.Euphrase Kezilahabi ni nguzo ambayo imeanguka na mhimili uliopotea. Tutakukumbuka
 
Kaptula la Max (Anasawiri Hali halisi ya viongozi walioshika madaraka kuwa madaraka hayawakai vilivyo Bali yanawapwaya)
 
Apumzike kwa amani mzee wetu[emoji120][emoji120]









SHIMBA YA BUYENZE

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimesikitika sana aisee...

Alikuwa mfuasi mzuri wa falsafa ya Existentialism na kama aliiishi falsafa hiyo basi atakuwa amefanya fujo zake kwa amani na ridhiko katika dunia hii yenye fujo za kila aina na sasa ameenda zake...

Binadamu siye yaani hovyo kabisa !!!
 
Kazi ya Muumba haina makosa. So kachukua kiumbe chake - RIP Prof. ila umetuachia Prof wa Elimu, aliongea kiingereza cha kufoke wachina mpaka nikazimia. 'take them inside' akimaanisha wawekwe lupango😱
😂😂😂kwa hyo amrudishe tumpe huyu au?
 
Back
Top Bottom