Tanzia: Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia

Mwandishi Nguli wa Kazi za Fasihi ya Kiswahili Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia. Tutamkumbuka Kezilahabi kwa kazi zake kama Rosa Mistika, Uwanja wa Fujo, Kaptula la Marx, Nagona na Mzingile! Alitetea Mashairi ya Kisasa!

Hakika, Jabali limeanguka! Tumeondokewa pakubwa.

Pumzika kwa amani Euphrase Vincent Mfunzi Bagaza Tilibuzya Kezilahabi😭😭

RIP Prof.
 
Pumzika kwa Amani Prof hakika vichwa maji na wale waliojifanya wamevaa kaptula la marx umewaacha.Mawazo yako yataishi (Kivuli kinaishi) Msalimie Shaaban Robert mwambie Tawasifu yake maisha yangu baada ya miaka 50 tunaendelea ingawa bado haijatimia,ukimuona Edwini Semzaba mwambie wakuu wa Shule siku hizi nao wamegeuka Magoswe,mpe hai nyingi Ben Mtobwa mzee wa pesa zinazonuka mwambie watu wanatanua nazo huku,bila kumsahau Elvis Musiba mzee wa njama.Wàsalimie waandishi wote ikiwezekana muendeleze fani katika Ulimwengu mwingine.Wasalamu.
 
Apumzike kwa Amani Marehemu Kazilahabi,Hakika tasnia ya Uandishi imepoteza Mwandishi Nguli.
pole kwa familia, siku hizi hamna wandishi kabisa, Kezilahabi riwaya zake nzuri sana. Wapo wengi sana ila sijui hawaandiki!
 
Mwandishi Nguli wa Kazi za Fasihi ya Kiswahili Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia. Tutamkumbuka Kezilahabi kwa kazi zake kama Rosa Mistika, Uwanja wa Fujo, Kaptula la Marx, Nagona na Mzingile! Alitetea Mashairi ya Kisasa!

Hakika, Jabali limeanguka! Tumeondokewa pakubwa.

Pumzika kwa amani Euphrase Vincent Mfunzi Bagaza Tilibuzya Kezilahabi😭😭
RIP Mzee Kezilahabi
 
Mwandishi mashuri wa riwaya nchini Tanzania, Profesa Euphrase Kezilahabi ameaga dunia.

Edmund makaranga Kangi, ambaye ni mpwa wa marehemu, amethibitisha kuwa Profesa Kezilahabi ameaga dunia akiwa jijini Dar es Salaam.

Kezilahabi alizaliwa mwaka 1944, alikuwa akifanya shughuli zake nchini Botswana kisha baada ya kuugua alirejea nyumbani Tanzania ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.

Profesa Kezilahabi amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Profesa Kezilahabi anaelezwa kuwa kielelezo cha aina yake cha uandishi bora, vitabu alivyoviandika vilisomwa sana nchini Tanzania na nje ya Tanzania

Source : BBC
 
AYU. :14:1
Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.

AYU. :14:2
Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.

Pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki kwa kumpoteza mpendwa wao ila kuna tumaini ipo siku tutaonana tena Kristo ajapo mara ya pili
 
Pumzika kwa amani msezawe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rosa mistika, ilileta ugomvi mkubwa na kanisa katoriki, RIP nguli/gwiji la fasihi afrika na dunian-prof kezilahabi,kazi zako zimejenga jamii😭
 
Prof. upumzike kwa amani. Nakumbuka nyakati zile ukiwa mmoja wa familia jirani pale Darajani UD.

Poleni sana wanafamilia. Hakuna msiba uliozoeleka wala hakuna umri ambao twasema ni halali mwanafamilia kututoka na hasa kwa mwanadamu ambaye alikuwa bado very productive kama marehemu.

Lakini machozi yenu yafutwe kwa tumaini letu katika Kristo.

Ufunuo 21:4
He will wipe away every tear from their eyes, and death shall be no more, neither shall there be mourning, nor crying, nor pain anymore, for the former things have passed away."
 
Back
Top Bottom