Tanzia: Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia

Tanzia: Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia

Pumzika kwa Amani Prof hakika vichwa maji na wale waliojifanya wamevaa kaptula la marx umewaacha.Mawazo yako yataishi (Kivuli kinaishi) Msalimie Shaaban Robert mwambie Tawasifu yake maisha yangu baada ya miaka 50 tunaendelea ingawa bado haijatimia,ukimuona Edwini Semzaba mwambie wakuu wa Shule siku hizi nao wamegeuka Magoswe,mpe hai nyingi Ben Mtobwa mzee wa pesa zinazonuka mwambie watu wanatanua nazo huku,bila kumsahau Elvis Musiba mzee wa njama.Wàsalimie waandishi wote ikiwezekana muendeleze fani katika Ulimwengu mwingine.Wasalamu.
Yani ma LEGEND kama hawa sijui kama watakuja kutokea tena zile kazi zao zimeandikwa kitaalam sana kwanini taifa siku hizi halizalishi watu wa namna hii TUKI sijui Takiluki wamelala tu
 
Eeeh, wacha Bhwanah! Kweli?

Mbona kazi ipo nchi yetu hii? Huyo ni waziri wa elimu, sio?

Kwani kulikuwa na shida gani ya kuongea Kiswahili hapo, si hao ni wachina, kiingereza cha nini kama hakipandi.
You will go on the cell today
 
kaptula la max shati la mao sikumbuki vizuri ha ha ha hah haha ha literature tamu sana
 
Yani ma LEGEND kama hawa sijui kama watakuja kutokea tena zile kazi zao zimeandikwa kitaalam sana kwanini taifa siku hizi halizalishi watu wa namna hii TUKI sijui Takiluki wamelala tu
mi huwa najiuliza sipati jibu, siku hizi hawaandiki, mtu unasoma aya moja unaona hamna kitu.
Zaman waliandika bwana,mfano Haji Gora Haji ata shule hajaenda lakin hayo mashairi yake huamini
 
Nisimlie kidogo basi hiki kitabu. Maana title tu ni kiboko.
Bageshi. Pitia uzi huu...

 
Nakubaliana nawe kabisa. Watanzania kusoma vitab n tatizo.
Gamba la nyoka!

Moja ya kazi nzuri kabisa ya Fasihi kutoka kwa huyu Prof.

Bahati mbaya aliandikia jamii ya watu wasio na utamaduni wa kusoma vitabu ama kupenda vya kwao.

R.I.P Prof.
 
Mwenyezi MUNGU amjalie pumziko la amani, Profesa. Kwang mim ndiye mtunzi namba moja tanzania
 
Back
Top Bottom