TANZIA: Mzee Mangula apata pigo

TANZIA: Mzee Mangula apata pigo

Harusi + Msiba... Kwa mila za kabila fulani huwa kuna walakini.......
 
Kufa ni faida na kuishi ni kristo cha msingi ni kujiandaa maana hakuna ajuaye saa yake...
 
Mungu amtie nguvu mzee MANGULA katika kipindi hichi kigumu.
BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
 
Kufa ni faida na kuishi ni kristo cha msingi ni kujiandaa maana hakuna ajuaye saa yake...

iseee.!!!
siku nyingi sijaenda kanisani.

kweli kuishi ni Kristu kufa ni faida. alazwe Mahali pema peponi Amina.!!
 
sio nemala ni neema.. nilimtangulia darasa moja shule ya msingi nyakahoja mwanza
 
Kila kitu kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake. Wakati wa kuzaliwa na wakati wa KUFA.
 
Innalillah waina-ilaih rajiun.

kumbe kuruani inaweza kuandikwa kwa kiswahili!!!!
kwa kuwa mungu hashindwi kitu, ataelewa tu tunapomuomba kwa stail hii!!!!! rip binti mangula, ukifika kwa sir god mwambie atuhurumie na kutuondolea majanga ya chama cha mdingi wako.

semeni AMEN!!!!!
 
Hizi ni baadhi ya sifa za marehemu NEMELA MANGULA, binti wa makamu mwenyekiti wa CCM, bw. Phillip Mangula, aliyefariki jana tarehe 18/08/2013:-

1. Mpole
2. Mtaratibu
3. Mchapa kazi
4. Ana akili
5. Ana adabu/heshima
6. Anapenda ushirikiano
7. Kiongozi
8. Msikivu
9. Mshauri mzuri
10. Hana makuu
11. Hajikwezi
12. Ana upendo
14. Mpiganaji
15. Hatumii kilevi
16. Msomi
17. Mtetezi wa 'wanyonge'
18. Mwanadiplomasia
19. Mwanajamii
20. Mpenda amani
21. Mpatanishi
22. Rafiki wa wote
23. Mwafrika halisi kwa umbo, ngozi, sura na tabia
24. Mfuasi wa utamaduni wa kiafrika

Kuna la kujifunza hapo? RIP Nemela. Pole Mangula. Namba 26-30 mpo? Ingawa nikiri nakichukia chama cha 'ccm', huyu binti kama angekuja kugombea kwenye nafasi ya kisiasa ningefikiria kumsapoti.

LICHA YA SIFA ZOTE HIZO NZURI NIZIJUAZO KUHUSU YEYE, KAFA. Wakati kila mtu akisikitia kufa akiwa binti mdogo hata kabla ya 'thirties'. Kama jamii sasa tujitazame. Madhara ya uovu kama ufisadi, wizi, rushwa, uzembe na jamii isiyotii kanuni za msingi na sheria yanatugusa wote chadema na ccm, wakristo kwa waislamu, maskini kwa matajiri. Tuviangalie vifo vya wananchi wetu hasa vijana. Je, vilipaswa kutokea? Je, mifumo yetu inatulinda au inasadia kueendeleza na kutetea uovu? Nemela hakupaswa kugongwa. TUREKEBISHE MIFUMO YETU YOTE YA MAISHA. RIP, once again, NEMELA
 

RIP NEMELA


PICHA: NEMELA MANGULA (KUSHOTO) AKIWA NA WAZAZI WAKE, KATIKATI NI BABA YAKE AMBAYE PIA NI MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TAIFA, MZEE PHILIP MANGULA.
 
Back
Top Bottom