TANZIA: Mzee Kitwana Kondo afariki dunia


Ni matumaini yangu makubwa angalau katika Msiba huu Mheshimiwa Rais wa JMT Dkt. Magufuli atakuwepo / atahudhuria.
 
Inna lillahi wainna ilaihi rajiuun. Nakukumbuka mzee Kitwana Kondo uliyekuwa huna elimu kabisa ya kuwa meya wa Dar. Nakukumbuka hasa kwa ule ufisadi wako wa kuuza open spaces za jiji! Na hasa ile kali uliyotaka kuwauzia kina Dewji open space ya mnazi mmoja bila aibu!!!! Dewji alishaanza kuizungushia uzio mchana kweupe. Baada ya wananchi kuwashikia mabango halmashauri ya jiji hatimaye serikali ikaingilia kati na kufuta mkataba ule wa kifisadi.
 

Stara haiuzwi Dukani!

Sifa na Kigezo cha kuwa Meyor mpaka Leo ni kujua kusoma na kuandika lakin umeamua kumuadhiri Maiti kwa Matusi ya Reja reja!

1963 Mzee KK anamaliza Shahada yake USA Babu yako ( age mate wa KK) Pengine hata kuandika Jina lake Kafa hawezi

Mola akusamehe na Ndugu wa Mzee Kondo pia wakusamehe Inshallah!
 
R I P Mzee Kondo, tunakukumbuka kwa mengi hasa hili la wanafunzi kumuita Mzee wa wakati huo "shemeji"
Mkuu umenikumbusha mbali, nilikuwepo wakati huo wasichana wa Jangwani wakimuita Mzee R shemejiiiii kila msafaa unapopita pale nilkuwa Azania. Wale mabinti walikuwa mapacha mmoja akahamishiwa Uk.
 
RIP mayor mstaafu wa jiji la Dar es salaam
 
Mwenyezimungu amsamehe makosa yake na sisi pia.

Acha dhihaka wewe,Mungu anasamehe Marehemu?Omba toba ukiwa hai,Acha ibada za mizimu,Eti amsamehe,muda wa msamaha ni wakati ukiwa hai jombaa!
 
Abudist,
Ingetosha kwa mimi kukunyamazia kimya lakini nimeona vyema nikufahamishe
lile ambalo wewe hulijui.

Mzee Kondo amekaa darasani vizuri yeye ni mhitimu wa Howard University,
Marekani.

Mzee Kondo bila shaka kwa yale mafunzo yake katika Idara ya Usalama ya
Kiingereza alikuwa bingwa wa kumpoteza yeyote asimjue.

Nakueleza haya kwa kuwa mimi Mzee Kondo alikuwa baba yangu kwa hiyo
nimekuwa karibu na yeye, nimemfahamu vizuri na nimejifunza mengi kutoka
kwake.

Kwanza alikuwa na ujuzi mkubwa sana wa lugha ya Kiingereza lakini hakupenda
watu walijue hili.

Mzee Kondo alikuwa anaijua vyema historia ''ancient,'' na ''modern.''

Nakumbuka siku moja alipotushangaza mimi na wenzangu alipotupa historia ya
Oliver Cromwell.

Siku nyingine alitushangaza tena alipotupa historia ya Saddam Hussein na Abdul
Karim Kassim
aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iraq.

Mzee Kondo alikuwa hodari wa kuhifadhi nukuu za wasomi wakubwa neno kwa neno
kwa lugha zote, Kiingereza na Kiswahili.

Mzee Kondo akimpenda sana mshairi, Muyaka bin Haj (1776 - 1840) na alihifadhi
beti zake nyingi.

Ajabu ni kuwa Kitwana Kondo ukimchukulia kuwa, ''hamna kitu,'' hatokukatisha tamaa
alipenda, kile Waingereza wanaita, ''to play dumb,'' yaani kujifanya mbumbu, ikiwa wewe
utamchukulia hivyo.

Abdudist, wewe kama wengi wa mfano wako umelambwa kichogo na baba yangu.
Mwisho ningependa kukunasihi kuwa maiti haisemwi vibaya.

Tumwache mzee wetu apumzike kwa amani.
 
Haichachi,
Ahsante ndugu yangu lakini taratibu tutafahamishana ukweli.
 
Reactions: OTG
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…