TANZIA: Mzee Kitwana Kondo afariki dunia

Mzee Kondo alisomea mambo ya strategic studies aka usalama huko Howard University

ALLAH AMREHEM
 
Acha dhihaka wewe,Mungu anasamehe Marehemu?Omba toba ukiwa hai,Acha ibada za mizimu,Eti amsamehe,muda wa msamaha ni wakati ukiwa hai jombaa!

Kwa hiyo kwa elimu yako ya dini tunapaswa kufanya nini kwa marehemu wetu....ie baba na mama wamefariki unawazika tu bila ya kuwaombea....au kuwaombea marehemu ni ibada ya mizimu....milango ya kumuombea iko wazi.iliyofungwa ni pamoja na ile ya yeye kujiombea wakati amekwisha kufa.
Hebu nawe tupe darsa kidogo maana elimu ni pana.
 
RIP Mzee wetu KK. Miaka ile ya themanini KK alikuwa nguzo ya Dar katika pande zake zote
 
Ni matumaini yangu makubwa angalau katika Msiba huu Mheshimiwa Rais wa JMT Dkt. Magufuli atakuwepo / atahudhuria.
Mkuu hayo matumaini yako makubwa hivyo yanatokana na nini labda kwa mfano??
 
Marehemu ndiyo mwenye Mkoa wake wa Dar es Salaam halafu ndiyo Msela na Mtoto wa mjini namba moja wa Jiji hili.
Ni kweli Mkuu wangu,
Ila Jamaa nae atajifanya ndie mwenye Nchi, so akifikiria Mwenye Nchi v/s Mwenye Mkoa obviously atapotezea tu kama alivyopotezea Kagera, Arusha etc
 
Wadau Kwema?

Kuna tetesi kua Mbunge wa zamani wa Kigamboni na Meya wa Jiji la Dar es salaam Bwana Kitwana Kondo (KK) amefariki Dunia Mchana huu; kuna mwenye taarifa zaidi ya hii kitu?

Alikuwa amelazwa hospitali ya Hindu Mandal

======
UPDATE:
======

Toka kwa Tunkamanin,

Inna lillahi wainna ilaihi rajiuun.

Mzee Kitwana Kondo, KK amefariki dunia jioni hii katika Hospitali ya Hindu Mandal. Atazikwa kesho 25/5/2017 In Shaa Allah

Wakati wa uhai wake, Kitwana Kondo aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Kigamboni na Meya wa Jiji la Dar es Salaam.


Ni hivi karibuni alitembelewa na Ndg. Edward Lowassa > Mzee Edward Lowassa amtembelea Mzee Kitwana Kondo hospitali ya Hindu Mandal

Aidha, unaweza kusoma pia > Hotuba ya Al Hajj Kitwana Kondo, Mbunge wa Kigamboni mwaka 1999 Bungeni Dodoma

R. I. P Mayor
 
Ni kweli Mkuu wangu,
Ila Jamaa nae atajifanya ndie mwenye Nchi, so akifikiria Mwenye Nchi v/s Mwenye Mkoa obviously atapotezea tu kama alivyopotezea Kagera, Arusha etc

Huyu mzee utoto wa mjini ulifika sehemu ukagonga mwamba...utoto wa mjini una kiasi.RIP Kitwana Kondo...he had all the time on earth to make peace with is GOD
 
"INNA LILLAHI WAINNA ILAIHI RAAJIUN"
Hakika taifa halitakusahau Mzee wetu Kitwana Kondo.

1495756121865.jpg


Ulikua mzalendo mwenye mapenzi ya dhati na Taifa letu katika kipindi chako chote cha utumishi Kuanzia Ulipokua Meya wa jiji la Dar es salaam, MB Kigamboni,M/kiti wa bodi ya Korosho na nafasi nyinginezo.

Vijana wako tutayaenzi kwa vitendo mazuri yote uliyoyafanya katika kipindi chote cha uhai wako.

R.I.P [HASHTAG]#MswahiliHalisi[/HASHTAG] [HASHTAG]#KitwanaKondo[/HASHTAG]
 
Mtaa wa mtitu nilishafika kwake tumecheza sana kwenye mti nadhani wa mpera hivi na kina Hamisi chizi
 
Back
Top Bottom