Inna lillahi wainna ilaihi rajiuun. Nakukumbuka mzee Kitwana Kondo uliyekuwa huna elimu kabisa ya kuwa meya wa Dar. Nakukumbuka hasa kwa ule ufisadi wako wa kuuza open spaces za jiji! Na hasa ile kali uliyotaka kuwauzia kina Dewji open space ya mnazi mmoja bila aibu!!!! Dewji alishaanza kuizungushia uzio mchana kweupe. Baada ya wananchi kuwashikia mabango halmashauri ya jiji hatimaye serikali ikaingilia kati na kufuta mkataba ule wa kifisadi.
Abudist,
Ingetosha kwa mimi kukunyamazia kimya lakini nimeona vyema nikufahamishe
lile ambalo wewe hulijui.
Mzee Kondo amekaa darasani vizuri yeye ni mhitimu wa Howard University,
Marekani.
Mzee Kondo bila shaka kwa yale mafunzo yake katika Idara ya Usalama ya
Kiingereza alikuwa bingwa wa kumpoteza yeyote asimjue.
Nakueleza haya kwa kuwa mimi
Mzee Kondo alikuwa baba yangu kwa hiyo
nimekuwa karibu na yeye, nimemfahamu vizuri na nimejifunza mengi kutoka
kwake.
Kwanza alikuwa na ujuzi mkubwa sana wa lugha ya Kiingereza lakini hakupenda
watu walijue hili.
Mzee Kondo alikuwa anaijua vyema historia ''ancient,'' na ''modern.''
Nakumbuka siku moja alipotushangaza mimi na wenzangu alipotupa historia ya
Oliver Cromwell.
Siku nyingine alitushangaza tena alipotupa historia ya
Saddam Hussein na
Abdul
Karim Kassim aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iraq.
Mzee Kondo alikuwa hodari wa kuhifadhi nukuu za wasomi wakubwa neno kwa neno
kwa lugha zote, Kiingereza na Kiswahili.
Mzee Kondo akimpenda sana mshairi,
Muyaka bin Haj (1776 - 1840) na alihifadhi
beti zake nyingi.
Ajabu ni kuwa
Kitwana Kondo ukimchukulia kuwa, ''hamna kitu,'' hatokukatisha tamaa
alipenda, kile Waingereza wanaita, ''to play dumb,'' yaani kujifanya mbumbu, ikiwa wewe
utamchukulia hivyo.
Abdudist, wewe kama wengi wa mfano wako umelambwa kichogo na baba yangu.
Mwisho ningependa kukunasihi kuwa maiti haisemwi vibaya.
Tumwache mzee wetu apumzike kwa amani.