Tanzia: Mwanajamvi afariki Dunia.

Tanzia: Mwanajamvi afariki Dunia.

Pole kwa wafiwa na wanajf wote kwa ujumla. Mungu amlaze mahala pema peponi na ampe pumziko la milele
 
kufa ni faida na kuishi ni kristo,
Mungu amtie nguvu mjane wa marehemu pia na watoto
 
Nimepigiwa simu jioni hii, dakika kadha zilizopita kuwa Mwanajamvi mwenzetu anayekwenda kwa ID ya wasaimon amefariki dunia muda kama dakika 45 zilizopita, katika hospitali ya Selian hapa Arusha, na sasa hivi ndiyo anaingizwa chumba cha ubaridi.
:A S cry::A S cry:

Taarifa hizo zinasema kuwa amenguka akiwa katika harakati za kuonana na Daktari, akiwa amesindikizwa na baba yake mzazi.

Wasaimon alijiunga na jamvi 6.10.2010.

Binafsi nilikuwa nafahamiana sana na wasaimon, alikuwa ni mtu wa kutoa ushauri wa hekima sana kuhusiana na maisha ya miaka hii, na alikuwa mpiganaji asiyechoka, akitumikia kampuni mojawapo ya Tours mjini Arusha. Naelekea msibani, nitawajuza kinachojiri.
wasaimon alivinjari hapa majukwaani hadi juzi 14.01.2012, na naambiwa kuwa hadi jana alikuwa mzima wa afya.
Ameacha Mke na watoto 3.

Mungu Ilaze Roho ya Marehemu wasaimon Mahala Pema Peponi.
RIP BRODA,kwanza anabahati amekufa amejulikana,sisi wengine tukifa hakuna atakaejua,maana nji hii wakikujua basi hata watoto wako watakuwa hatarini.
 
Poleni sana ndugu zangu wana jamvi na familia ya Wasaimoni Mungu mwenye neema nyingi awafute machozi na katika kipindi hiki kigumu
 
Mwanga wa milele umwangazie ee baba raha ya milele umpe APUMZIKE KWA AMANI AMINA
 
Back
Top Bottom